Skip to main content

WAZIRI PEMBE ALIPA RAI 'IAA' KUFIKIA MALENGO YAO




 Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amelitaka Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), kuongeza  jitihada katika usimamizi na kuhakikisha malengo ya chuo ya muda mrefu na muda mfupi yanafikiwa kama ilivyokusudiwa.

Waziri Riziki ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Baraza jipya la Uongozi wa Chuo hicho iliyofanyika katika Ukumbi wa IAA, Arusha.

Amesema Chuo cha Uhasibu Arusha kimeamua kujitofautisha na vyuo vyengine kwa namna mbalimbali ikiwemo kuanzisha mitaala ya kipekee mfano mitaala ya uanagenzi (apprenticeship), kuanzisha mitaala inayoandaa wataalam wanaoweza kujiajiri na kuajiri wengine, kutengeneza miundombinu na mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia.



Hivyo ametoa rai kwa Baraza hilo kuhimiza juhudi za kuboresha ubora wa elimu inayotolewa na chuo, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mitaala itakayoanzishwa katika kipindi cha utekelezaji wa majukumu yao ili inaendelea kuwa mfano katika kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kutoa wasomi watakao ongeza nguvu katika kutatua changamoto katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Mhe Riziki amefahamisha Baraza la Uongozi ni chombo muhimu katika kuhakikisha usimamizi bora wa shughuli za chuo, kuimarisha utawala bora, na kusimamia utekelezaji wa mikakati inayolenga kuboresha elimu na huduma zinazotolewa na chuo.





Aidha amewakumbusha umuhimu wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya uwazi, uwajibikaji, na ushirikishwaji wa wadau wote kwani  itasaidia kujenga mazingira ya kuaminiana na kushirikiana kwa karibu katika kufanikisha malengo ya chuo chao.

Sambamba na hayo Mhe.Riziki amewataka kuhakikisha wanasimamia maadili na misingi imara na uwajibikaji  kwa menejimenti na Wanafunzi kwa ujumla ili kuona Taifa la Tanzania linaendelea kusimamiwa vizuri.

Amesema kupitia baraza hilo, ana matumaini kuona maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali, ikiwemo ubunifu katika ufundishaji, utafiti wenye tija, na ushirikiano na wadau wa ndani na nje ya nchi.

Vile vile Mhe. Riziki amewapongeza wajumbe wapya kwa kuteuliwa kuwa sehemu ya Baraza hilo la Uongozi ambapo amesema uteuzi wao ni ishara ya imani kubwa ya Serikali na wananchi. Hivyo amewataka  kutumia ujuzi na uzoefu wao katika kushauri na kusimamia mambo mbalimbali ya Chuo kwa manufaa ya Wanafunzi, Wafanyakazi, na jamii kwa ujumla.

Mhe.Riziki ametumia fursa hiyo kuwaomba kila mmoja kwa nafasi yake kuendelea kuhubiri amani ya nchi na kuunga mkono juhudi za viongozi wakuu wa nchi Dr. Samia Suluhu Hassan na Dr. Hussein Mwinyi katika kuona wanalinda na kuisimamia amani ya nchi na maendeleo kwa ujumla.

Naye Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Prof. Eliamani Sedoyeka, ameelezea mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kuwa ni pamoja na Ujenzi na uboreshaji wa miundombinu katika Kampasi za Arusha, Babati, Dodoma na kuanza kwa hatua za ujenzi katika Kampasi ya Songea pamoja na  ongezeko la mitaala,  Wanafunzi na Wafanyakazi.


Akitoa shukurani zake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Dkt. Mwamini Tulli amemuhakikishia Mhe.Riziki kuwa wataendelea kusimamia maadili na uwajibikaji katika chuo hicho ili malengo yaweze kufikiwa, huku akimshukuru Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan, kwa Kuendelea kumuamini kuongoza kwenye nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Baraza hilo kwa awamu ya pili.

Baraza la chuo cha Uhasibu Arusha limezinduliwa rasmi  tarehe 8/04/2025  likiwa na wajumbe 12, na litafanyakazi zake kwa muda wa miaka mitatu. 

MWISHO

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...