NA HAJI NASSOR, DAR-ES SALAAM@@@@
WANACHAMA wa Baraza la Habari Tanzania MCT, wamemchagua Rais mpya
wa Baraza hilo, Jaji Mstaafu: Bernad Luanda, kupitia mkutano mkuu wa 26,
uliofanyika Septemba 27, 2024 ofisi za ‘MCT’ Tegeta nje ya jiji la Dar-es Salaam.
Kati ya wanachama hai 29, waliohudhuria mkutano huo, waliomchagua rais huyo ni wanachama 27, kura moja ikimkataa na moja iliharibika, ambapo kisha Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Nicholaus Mwaibale alimtangaaza.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, Katib Mtendaji mpya wa baraza hilo
Ernest Sungura, alisema kwa sasa baraza linakuja kivingine, lengo likiwa ni
lile lile la kuwanoa waandishi wa habari.
Alisema,
kuanzia mwakani, MCT itakua na mradi mkubwa unaojulikana kwa jina la ‘WAJIBIKA’ambao
utakuwa wa miaka saba.
Alisema,
mradi huo wa paund milioni 30, utagusa karibu kila eneo, ikiwemo kuwajengea
uwezo hata waandishi wa habari mmoja mmoja, kupiti vyombo vyao.
Alieleza
kuwa, jingine ambalo litafanyika mwakani, ni sherehe kubwa na za aina yake, ya
mafanikio ya ‘MCT’ kwa miaka 30, tokea lilipoanzishwa mwaka 1995.
Katibu
Mtendaji huyo mpya, aliwataka wanachama wenye madeni, ambayo kwa mwaka huu
yamefikia shilingi milioni 167, kulipa haraka, ili kulipa uhai baraza hilo.
‘’Wanachama
ambao wana deni la kufikia miaka 10, ni wengi na ndio maana, linafikia wastani
wa shilingi million 167, fedha ambayo yengetusaidia, katika utendaji wa kazi zetu,’’alifafanua.
Aidha
Katibu huyo Mtendaji, aliwapongeza waandishi wa habari kutoka kisiwani Pemba,
kwa kujitokeza kwa wingi, katika kuwasilisha kazi za kutafuta mshindi wa tunzo
za uhamiri wa mwandishi wa habari Tanzania ‘EJAT’, mwaka 2023/2024.
Nae
Makamu wa Rais wa ‘MCT’ Yussuf Khamis, alisema anajivunia umoja na mshikamano, uliopo
baina ya wanachama na watendaji wa MCT.
Hata
hivyo, alisisitiza haja kwa wanachama wenye madeni, kusawazisha, ili kuona ‘MCT’
haitegemei mno fedha za wafadhili, katika kujiendesha kwake.
Akiwasilisha
ripoti ya fedha, ya mwaka 2023, ‘CPA’ Happiness Nkya, alisema walipata mapato
ya shilingi bilioni 1.1, ambapo ni punguzo la shilingi milioni 600,
ikilinganishwa na shilingi bilioni 1.6 za mwaka 2022.
Alieleza
kuwa, kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 1.0 ni za wafadhili na shilingi million
38 ni michango ya ndani, ikiwemo ada ya mwanachama wa MCT.
Hata
hivyo, alisema katika ukaguzi uliofanyiwa, wamepata hati safi, jambo
linaloonesha kuendelea kufuatwa kwa taratibu za manunuzi na matumizi.
Baadhi
ya wanachama akiwemo mwandishi Jabir Idrissa kutoka Zanzibar, alisema ujio wa
baraza huru la habari la serikali, isiwe sababu ya MCT kujiondoa.
‘’Hapa
chakuzingatia tupate uzoefu katika baadhi ya nchi, kuona wanakwenda vipi,
wanapokuwa na baraza la habari la serikali na lile binafsi kama MCT,’’alifafanua.
Nae
rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania ‘UTPC’ Keneth Simbaya,
alimpongeza Katibu Mtendaji mpya wa MCT kwa maono yake, katika kulivuusha
baraza hilo.
Nae
Issaya Kisibuli kutoka Gazeti la Jibu la Maisha, aliomba wanachama ambao wanamadeni,
kufuatiliwa kwa kina, ili waeleze sababu na misimamo yao.
Wakati
huo huo, mkutano huo umewapitisha wanachama wapya kadhaa, ikiwemo blog ya Pemba
tody, Bahari Media, Trust Media Agency, Star Tv, Pemba ya leo blog, star tv
pamoja na Redio free Afrika.
Mwisho
Comments
Post a Comment