NA HAJI NASSOR, DAR-ES-SALAAM@@@@
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk. Tulia Ackson, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, jioni ya leo Septemba 28, 2024
kwenye hafla ya 15 ya kuwakabidhi tunzo waandishi wa habari mahiri.
Tunzo hizo ambazo zimekuwa zikiandaliwa na Baraza la Habari
Tanzania ‘MCT’, kwa mwaka wa 15, tokea zilipoanzisha mwaka 2009, zinatarajiwa
kufanyika ukumbi wa AGA KHAN DIAMOND JUBILEE eneo la Upanga jijini
Dar-es Salaam.
Akitoa taarifa hiyo jana, Katib Mtendaji mpya wa ‘MCT’ Ernest
Sungura, alisema matayarisho yote yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa mgeni rasmi huyo.
Alisema, Spika huyo ndie atakaemkabidhi mshindi wa jumla kwa
mwaka 2023/2024, huku washindi wingine mbali mbali wakikabidhi zawadi na tunzo
zao, na wageni mashuhuri waalikwa.
Alieleza kuwa, katika hafla inayofanyika jioni hii ya leo,
kutakuwa na mambo kadhaa mazuri ikiwa ni pamoja na zawadi kwa mwandishi nguli
aliyefanya vyema zaidi katika maisha yake ya kihabari.
Akizungumzia kuhusu zoezi
hilo, alisema Majaji saba wa Tuzo za
Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) wamehitimisha kazi ya kutathmini
ubora na weledi wa kazi zipatazo 1,135 na kuwateua waandishi wa habari 72
watakaoingia katika kinyang’anyiro cha kumtambua mshindi wa kwanza, wa pili na
wa tatu na mshindi wa jumla.
Kati ya waandishi wa habari 72, wanaume ni 45
(sawa na 62.5%) na wanawake 27 (sawa na 37.5%). Kati ya wateule hao, wateule 14
(19%) wanatoka katika runinga; 13 (18%) wanatoka vyombo vya mtandaoni, redio 20
(28%) na wateule 25 (35%) wanatoka kwenye magazeti.
Wateule wamepatikana kwa kukidhi vigezo vya
ubora ambavyo ni pamoja na ukweli, usahihi, uanuai, haki, kina, utafiti,
ubunifu, uvumbuzi, upekee, uchambuzi, uwajibikaji, ufichuaji maovu, uadilifu,
uwasilishaji unaoeleweka na uchunguzi. Ifahamike pia kwamba vigezo maalum
vilitumika kuzingatia aina tofauti ya vyombo vya habari kama vile redio,
televisheni, magazeti na habari za mitandaoni.
Kabla ya kutaja majina ya wateule hao 72 ni
muhimu ifahamike kwamba kinyang’anyiro cha kumtambua mshindi wa kwanza, wa pili
na wa tatu na mshindi wa jumla kwa makundi 20 ya kushindaniwa kitakuwa jioni ya
leo.
Alifafanua kuwa, moja ya jambo la kipekee
katika kilele cha kinyang’anyiro hicho ni pamoja na kusikia kutoka kwa jopo la
majaji kuhusu viwango vya uandishi wa habari za magazeti, redio, televisheni na
mitandaoni kwa habari zilizohusu uwekezaji wa kampuni ya DP world katika
bandari za Tanzania, habari kuhusu Ngorongoro na wamasai na kuhusu maporomoko
ya Hanang.
Jambo la pili la kipekee ni kumshuhudia Waziri
wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Jerry Silaa
akizindua Jarida la Tuzo na Tuzo magazine ambayo yanajikita kuhamasisha umahiri
katika sekta mbalimbali Tanzania na nje ya Tanzania. Kwa kuanzia majarida hayo,
moja la Kiswahili na lingine la Kiingereza yatabeba maudhui ya tuzo za umahiri
wa uandishi wa habari Tanzania (EJAT).
Aidha ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza kazi
za kihabari kwa EJAT 2023 zimeongezeka hadi 1,135 kutoka kazi 893 za EJAT 2022.
EJAT 2020 kazi zilikuwa 396 na EJAT 2021 kazi zilikuwa 608.
Taasisi zinaounda
Kamati ya Maandalizi ni Wakfu wa Vyombo vya Habari (TMF), Chama Cha Waandishi
wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri (TEF), HakiElimu, Umoja
wa Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), Umoja wa Klabu za
Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari
Tanzania (MOAT), Sikika, Misa – Tan na Twaweza.
Sasa nimalizie kwa kusoma
orodha ya wateule wa EJAT 2023 pamoja na vyombo vyao:
NA. |
JINA |
JINSIA |
CHOMBO |
MKOA |
1 |
Thomas Masalu
Lunyalo |
M |
Mazingira FM |
Mara |
2 |
Abdallah
Bakari Nassoro |
M |
Nipashe |
Mtwara |
3 |
Jacob Mogesi
Musenda |
M |
The Citizen |
Dar es Salaam |
4 |
Marco Maduhu |
M |
Shinyanga
Press Club |
Shinyanga |
5 |
Salum Vuai
Issa |
M |
Zanzibar Leo |
Zanzibar |
6 |
Jackline
Victor Kuwanda |
F |
The Chanzo |
Dodoma |
7 |
Stanslaus
Lambert |
M |
Swahili 360 |
Dar es Salaam |
8 |
Zacharia
Nyamoga |
M |
IPC Mkombozi
TV |
Iringa |
9 |
Irene
Mwakalinga |
F |
TBC1 |
Iringa |
10 |
Said Ally
Sindo |
M |
Storm FM |
Geita |
11 |
Joshua
Stephen |
M |
Nukta |
Dar es Salaam |
12 |
Samweli
Mpogole |
M |
Highlands FM |
Mbeya |
13 |
Shekha
Suleiman |
F |
ZBC |
Pemba |
14 |
Abel Kilumbu |
M |
Dar 24 |
Dar es Salaam |
15 |
Khamis
Mohamed |
M |
Zanzibar Leo |
Zanzibar |
16 |
Abdiel
Jumanne Siffi |
M |
UFM |
Dar es Salaam |
17 |
Julius
Maricha Maricha |
M |
The Citizen |
Dar es Salaam |
18 |
Eliya Solomon |
M |
Mwanaspoti |
Dar es Salaam |
19 |
Huwaida
Nassor Moh’d |
F |
As Salaam FM |
Zanzibar |
20 |
Rehema Evance
Mwaikema |
F |
UTV |
Simiyu |
21 |
Philip
Mwihava Mwihava |
M |
Clouds FM |
Dar es Salaam |
22 |
Zourha John
Malisa |
F |
Mwananchi |
Dar es Salaam |
23 |
Linus Ananias
Gamarwa |
M |
TBC |
Dodoma |
24 |
Catherine
Sekibaha |
F |
Pangani FM |
Pangani Tanga |
25 |
Herieth
Makwetta |
F |
Mwananchi |
Dar es Salaam |
26 |
George
Helahela |
M |
Mwananchi |
Dar es Salaam |
27 |
Esau Ezra
Ng’umbi |
M |
Nukta Habari |
Dar es Salaam |
28 |
Benson
Eustace Jacob |
M |
UTV |
Kagera |
290 |
Mariamu Ally
Abdallah |
F |
Pangani FM |
Tanga |
30 |
Adam Gabriel
Hhando |
M |
CG FM |
Tabora |
31 |
Sanula
Renatus Athanas |
M |
Nipashe |
Dar es Salaam |
32 |
Elizabeth
Edward Kusekwa |
F |
Mwananchi |
Dar es Salaam |
33 |
Pamela
Nasphory Chilongola |
F |
Mwananchi |
Dar es Salaam |
34 |
Rodgers Simon |
M |
ITV |
Dar es Salaam |
35 |
Mukrim
Mohamed Khamis |
M |
KTV TZ Online |
Zanzibar |
36 |
Ephrahem
Edward Bahemu |
M |
Mwananchi |
Dar es Salaam |
37 |
Mkwaji Reuben
Masatu |
F |
UTV |
Dar es Salaam |
38 |
Lukelo
Francis Haule |
M |
The Chanzo |
Dar es Salaam |
39 |
Benjamin
Mzinga |
M |
ITV |
Dar es Salaam |
40 |
Dickson
Shukran Kanyika |
M |
RFA |
Njombe |
41 |
Hamisi
Makungu Hamisi |
M |
Pangani FM |
Pangani Tanga |
42 |
Halfan Chusi |
M |
Nipashe |
Dar es Salaam |
43 |
Kelvin Paul
Matandiko |
M |
Mwananchi |
Dar es Salaam |
44 |
Waryoba Musa
Waryoba |
M |
Montessory
Tanzania |
Mwanza |
45 |
Anna
Peter Mbuthu |
F |
TBC |
Arusha |
46 |
Egan Salla |
M |
BBC |
Dar es Salaam |
47 |
Imma Rashid
Mbuguni |
M |
Majira Online |
Dar es Salaam |
48 |
Haika E.
Kimaro |
F |
The Citizen |
Mtwara |
49 |
Margareth
Msafiri Geddy |
M |
TBC Safari |
Dar es Salaam |
50 |
Yohana Chance
Challe |
M |
Mwanaspoti |
Mbeya |
51 |
Mgongo
Kaitira Mafuru |
M |
Mwananchi |
Mwanza |
52 |
Mercy Yasin
Mbaya |
F |
UTV |
Dar es Salaam |
53 |
Imani Raphael
Makongoro |
F |
Mwananchi |
Pwani |
54 |
Fatma
Abdallah Chikawe |
F |
UTV |
Dar es Salaam |
55 |
Brown Benny
Mbwawa |
M |
Wasafi FM |
Mbeya |
56 |
Ayoub Stanley
Nyondo |
M |
Shamba FM |
Iringa |
57 |
Warioba
Igombe Warioba |
M |
Uhuru |
Mara |
58 |
Salome
Gregory Sumbya |
F |
The Citizen |
Dar es Salaam |
59 |
Veronica
Natalis Mataba |
F |
DW Swahili |
Arusha |
60 |
Saa Mbwana
Zumo |
F |
Pangani FM |
Pangani Tanga |
61 |
Said Ali
Ngamba |
M |
Uyui FM |
Tabora |
62 |
Lugendo
Madege |
M |
UFM |
Dar es Salaam |
63 |
Anna Potinus |
F |
Mwananchi |
Mwanza |
64 |
Christina
Mwakangale |
F |
Nipashe |
Dar es Salaam |
65 |
Rauhiya M
Shaban |
F |
Bomba FM |
Zanzibar |
66 |
Hazla Omary
Quire |
F |
The Tanzania
Times |
Arusha |
67 |
Lucy Patrick
Samson |
F |
Nukta |
Dar es Salaam |
68 |
Mohamed
Hammie Rajabu |
M |
Habari Leo |
Dar es Salaam |
69 |
Amina
Deogratias Semagogwa |
F |
Radio Kwizera |
Kigoma |
70 |
Hellen
Nachilongo Mkisi |
F |
The Citizen |
Dar es Salaam |
71 |
Alfred
Bulahya Jakuba |
M |
Dodoma FM |
Dodoma |
72 |
Waziri Iddi
Suka |
M |
Tumaini TV |
Dar es Salaam |
Hongereni sana kuingia katika kinyang’anyiro
cha Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2023.
Ernest S. Sungura
Mwenyekiti
Kamati ya Maandalizi ya EJAT
2023
Comments
Post a Comment