VYOMBO vya habari
nchini vimetakiwa kuibua matatizo mbalimbali yanayohusiana na afya ya uzazi kwa
wanawake na wasichana jambo ambalo husababisha wanawake wengi kutojiunga na
huduma ya afya ya uzazi.
Akifungua mafunzo ya
siku tatu kwa vyombo vya habari kwa niaba ya Mkurugenzi wa chama cha
waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA ZNZ, mjumbe wa bodi ya
Chama hicho Shifaa Said Hassan, alisema ni wajibu kwa waandishi kufatilia na
kuandika matatizo yanayowakabili wanawake hususani wanapotaka kujiunga na
huduma hizo ili waweze kujua njia bora na salama.
“Licha ya kuwepo kwa sera na seheria
zinazosisitiza umuhimu wa mwanamke kupata huduma hizo lakini inaonekana
asilimiia kubwa ya kundi hilo hawana uelewa wa kutosha juu ya matumizi sahihi
ya huduma hiyo hivyo kupitia vyombo vya habari itakuwa chachu ya kuwaelekeza na
kufikia malengo ya kuimarisha afya zao,”Shifaa Said, amesma.
Aidha aliwaomba waandishi wahabari kuwa kusikiliza kwa makini
mafunzo wanayopata kwa lengo la kuyafanyia kazi ipasavyo ili yalete tija kwa
jamii na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake
mkufunzi na Mwandishi Mkongwe wa mafunzo
hayo Salim Said Salim alisema wanawake wengi na watoto wanakosa haki zao za
msingi ikiwemo kukosa lishe bora malezi ya pamoja baina ya mke na
mume, hali ambayo husababisha jamii kukosa kizazi kisicho bora.
Amesema
waandishi wahabari lazima wafatilie na
kuibua ishu ambazo zinahusiana na haki ya afya ya uzazi na badala yake
wasiridhike na kufunguliwa kwa vituo vya afya.
“Nawasisitiza waandishi wahabari kufanya
uchunguzi juu ya huduma zinazotolewa kama kuna madaktari wa kutosha, dawa za
kutosha ili kwenda sambamba na mahitaji ya wananchi katika kupata huduma bora,”Salim
Said Salim,Mkufunzi.
Akiwasilisha mada ya
afya ya Uzazi na malezi ya watoto katika Uislamu Mjumbe wa Baraza la Maulamaa
kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibarm Sheikh Khamis Abdulhamid Khamis amesema katika
kuwalea watoto ni jukumu la wazazi kuzingatia umri wa mtoto tokea siku anayozaliwa
mpaka kufikia baleghe na kuendelea kujenga ukaribu na kuwafatilia katika nyendo
zao.
‘’Katika malezi ya
watoto, ni wajibu wa wazazi kushirikiana kwa pamoja kujuwa tabia za watoto wao.
Watu wanaoshirkikana nao kama vile marafiki, ni lazima kuwachagulia marafiki
wema, hii itawasaidia hata makuzi yao, na pia husaidia kuimarisha afya ya uzazi
na malezi kwa mtoto kwa mujibu wa kitabu kitukufu cha qur ani kupitia aya
mbali mbali za qurani,” Sheikh Khamis
Abdulhamid.
Nae Mkufunzi wa
magonjwa ya Uzazi na wanawake kutoka hospitali ya Rufaa Mnazi mmoja Dk
Ummulkulthum O.Hamad amesema waandishi wahabari kutekeleza wajibu wao ipasavyo
kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu masuala ya haki ya afya ya uzazi,
“Katika jamii kuna
shida bado Elimu ni ndogo kabisa kuhusu afya ya uzazi, ukizungumzia suala hili
jamii yetu inadhani ni suala la wanawake pekee bali ni la linamgusa kila
binadamu kwa sababu mtoto akizaliwa jambo la kwanza unaulizwa umepata mtoto
gani? Badala ya kuuliza hali ya mama mtoto inaendeleaje, hapa ujuwe tayari
jinsia imeanza, Dk Ummulkulthum O.Hamad,
Daktari wa magonjwa ya uzazi na wanawake kutoka hospitali ya Rufaa Mnazi
Mmoja.
Nao waandishi wahabari
wamesema watayatumia mafunzo waliyoyapata kwa kuandika habari na kutayarisha
vipindi vinavyohusiana na haki ya afya ya uzazi kwa lengo la kutoa Elimu kwa
jamii ili kuondokana na dhana potofu kwamba masuala haya yanamuhusu mwanamke
pekee.
Washiriki wa mafunzo
hayo wakieleza changamoto ziliyopo katika afya ya uzazi walisema ni pamoja na
madaktari wanaotowa huduma hiyo kutokuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa sambamba
na kutokuwa na uelewa juu ya baadhi ya huduma wanazizitoa
Mafunzo hayo ya siku
tatu yameandaliwa na tamwa zanzibar kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa
habari ili kuielimisha jamii kuhusiana na afya ya uzazi.
MWISHO |
|
Comments
Post a Comment