SERIKALI ya Mapinduzi
Zanzibar (SMZ) kupitia Wizara ya Maji, Nishati na Madini imeingiza mapato
ya sh. bilioni tatu na milioni hamsini na sita kwa kipindi cha miezi mitatu
ikiwa ni mauzo ya maliasili zisizorejesheka ikiwemo kifusi, mchanga mawe,
kokoto na vumbi.
Hayo yameelezwa na
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizaya hiyo ambaye amehamishiwa katika Wizara ya Ardhi
na Maendeleo ya Makaazi, Dkt Mngereza Mzee Miraji wakati akimkabidhi ofisi
Katibu Mkuu mpya wa wizara hiyo Joseph John Kilangi aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi.
Dkt. Mngereza
amesema kutokana na changamoto za upotevu wa maliasili kwa kushirikiana na
watendaji wake waliamua kuchukua hatua za makusudi kuazisha mfumo wa kuombea
maliasili zisizorejesheka ili kuzuia upotevu mali hizo. Hivyo April hadi Juni
wizara hiyo imeweza kuingiza fedha hizo ambapo mwezi wa Juni pekee
uliingiza shilingi bilioni moja na nusu.
“Mfumo huu ni mzuri
sana kwani unaweza kuona gari inapoingia katika shimo la maliasili, mali
iliyobeba, uwezo wa gari, na wapi inaelekea hali ya kuwa nipo ofisini hata
usiku. Pia mtu akilipa malipo benki kupitia mfumo huu unaonesha
fedha zilizoingia aina zote za malipo kuanzi kibali shilingi 3000, kutokana na
kamera zilizofungwa. Hii ndio ilikuwa kazi ngumu ya kudhibiti upotevu wa
maliasili” alisema Dkt.Mngereza
Aidha Dkt. Mngereza
aliwashukuru watendaji kazi wa wizara hiyo kwa mashikiano makubwa
waliyompa katika kipindi chote alichotumika wizara hiyo kwani walikuwa
wakifanya kazi kwa mashikiano ya karibu hali ambayo imeonesha dhamira ya
Serikali katika kuwaletea wananchi wake maendelo.
Kwa Upande wake
Katibu Mkuu wa Wizara Hiyo Joseph J. Kilangi aliyekabidhiwa amesema anaamini
yote aliyokabidhiwa atayaendeleza kwa dhati ile ile hivyo, amewaomba
watendaji wa wizara hiyo kumpa mashirikina kama walivyompa Dkt Mngereza kwa
sababu wote wanajenga nyumba moja ya kutekeleza ahadi za Serikali ya Awamu ya
Nane inayongoza na Rais Dkt Hussein Mwinyi.
Aidha amewataka
watendaji wa wizara hiyo kutomchoka mapema kutokana na kuwaita mara kwa mara
kwani majukumu hayo ni mapya kwake hivyo anahitaji kujifunza mambo mengi
kupitia kwao. Amesema anaamini akipewa mashirikiano hakuna kitakacho mshinda
kwani kinachohitajika ni uwazi na uwajibikaji.
Mapema Waziri wa
Wizara hiyo, Shaibu Hassan Kaduara amemshukuru Dkt Mngereza kwa
mashirikiano makubwa aliyompa pamoja na juhudi za kuanzisha mfumo huo. Amesema
mashirikinao ya Dkt. Mngereza yameweza kufanikisha bajeti ya wizara
hiyo kupita kwa urahisi hivyo amewataka watendaji wa wizara hiyo, kuendeleza
ili ufanisi upatikane.
Makabidhiano hayo
yamekuja kufuatia uteuzi aliyoufanya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapiduzi Zanzibar Dkt Hussein siku ya Juni 30,2022 wa kuwateua manaibu
katibu mkuu pamoja kuwabadilisha makatibu wakuu wa wizara mbali mbali za SMZ.
Comments
Post a Comment