NA HAJI NASSOR, DODOMA
WAZAZI na walezi, wametakiwa kuzungumza
na watoto wao wachanga kwa lugha rasmi, zinazozungumzwa na jamii yao, kwani
kufaya hivyo, ni sehemu ya kuongeza makuzi, ufahamu na utanuzi wa ubongo wao.
Kwani,
tafiti zimegundua kuwa, watoto hata wanapokuwa tumboni, wanauwezo mkubwa wa
kusikia mazungumzo ya lugha yoyote, hivyo mara wanapozaliwa wazazi wawe nao
karibu.
Muwezeshaji
kwenye mafunzo ya Kitaifa ya Sayansi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya
Mtoto ‘SECD’ kutoka Mombasa Kenya Everlyne Okeyo, aliyaeleza hayo mjini Dodoma.
Alisema,
watoto wanakosa ukuaji mzuri wa kutengeneza ubongo wao, kwa kule wazazi
kutowashughulika kuzungumza nao, wakidhani hawana uwezo wa kufahama lugha zao.
Alieleza
kuwa, makuzi mazuri ya awali ya mtoto, ni baina ya siku moja baada ya kuzaliwa hadi
miaka minane, ambapo hapo huwa rahisi kwa wazazi na walezi, kuweke mwelekeo wa
maisha ya mtoto.
‘’Wazazi
waliowengi wamekua wanaanza kuweka nguvu zaidi za watoto wao, mara wanapokuwa
na umri wa kuanza elimu ya awali, jambo ambalo sio sahihi,’’alifafanua.
Mwezeshaji
huyo na mtaalamu wa malezi ya sayansi ya awali ya watoto ‘SECD’ alisema, tafiti
zinaonesha kuwa, mtoto anauwezo wa kuzungumza zaidi ya lugha 600 mara
anapozaliwa, ambapo hapo ni jukumu la jamii yake, kumuelekeza wanapotaka.
Katika hatua
nyingine, Everlyne alisema, ubongo wa binadamu una nyuroni bilioni 100, na ndio
maana mtoto mara anapozaliwa, huwa na asilimi 25 ya ubongo wake ni mtu mzima.
‘’Mtoto
anapofikia mwaka mmoja, hufikia asilimia 60, wakati miaka miwili huwa na
asilimia 75 na kuanzia miaka minne hadi sita, hubeba asilimia 90 ya
uwelewa,’’alieleza.
Kuhusu
mazingira, kama ya mtoto kucheza, kujumuika na wenzake na kujifunza, huchangia
kwa haraka ukuwaji wa ubongo wake.
Akizungumza
kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake
na Makundi Maalum Dk. Dorothy Gwajima, aliwataka waandishi wa habari,
kuifikisha kwa jamii, dhana ya malezi ya kisayansi ‘SECD.
Alisema
nguvu ya vyombo vya habari, vinaweza kuwa chachu kwa wazazi na walezi kufikiria
sasa, namna ya kuwalea na kuwaandaa watoto kukabiliana na changamoto mapema.
Aidha waziri
Gwajima, alisema bado ukatili wa watoto umekuwa mkubwa Tanzania, na ndio maana
mwaka 2021 pekee walipokea matukio 11,499.
Kwa upande
wake, mchechemuzi kinara wa ‘ECD’ kutoka Umoja wa vilabu vya waandishi wa
Habari Tanzania ‘UTPC’ Victor Maleko, alisema tokea kuzinduliwa kwa mradi huo,
habari 1,000 zimeshaandikwa.
Alieleza
kuwa, kwa awamu ya pili baada ya kuwepo kwa mafanikio, umehusisha waandishi wa
habari wa nchi nzima kupitia vilabu vyao 28 ikiwemo, kutoka Zanzibar.
Mkurugenzi
Mkaazi wa Shirika la Children in Crossfire, Craig Ferla, alisema mradi wa mtoto
kwanza, umeleta mafanikio makubwa kwa wanafunzi wa elimu ya awali.
Alisema
ushirikiano uliopo baina ya shirika lake na serikali, umepelekea kuwa na hamu
ya kuendelea kuutekeleza, katika skuli mbali mbali nchini mradi huo.
Hata hivyo
Mkurugenzi huyo mkaazi, amempongeza waziri Gwajima, kwa kuendelea kushirikiana
kwa karibu, juu ya kuwapatia malezi ya kisayansi watoto nchini Tanzania.
Meneja Mradi
wa ‘ECD’ kutoka tasisi ya maendeleo ya binadamu kupitia Chuo cha Aga Khan, Joyce
Marangu, amesema wameona sasa kuupanua mradi huo wa malezi ya kisayansi ‘SECD’
baada ya awamu ya kwanza, kufanikiwa.
Alisema
ingawa bado baadhi ya mikoa haijafikiwa kikamilifu, lakini kutokana na
ushirikiano uliopo, hana hofu na jambo hilo.
‘’Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa karibu mno na Chuo cha Aga Khan, na
hili linatupa hamasa kuona mradi huu wa sayansi ya malezi na makuzi
utafanikiwa,’’anasema.
Mafunzo hayo
ya siku sita, yanayojumuisha washiriki 79 wakitoka mikoa kadhaa, yamehusisha
waandishi wa habari, maafisa uastawi, maafisa maendeleo na watendaji wa asasi
za kiraia.
Mwisho
Comments
Post a Comment