TAMWA - ZANZIBAR YAWAPA SOMO WAANDISHI WA HABARI HABARI ZA UDHALILISHAJI MAENEO YASIOPEWA KIPAOMBELE
NA
MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@
MRATIBU
wa Program ya Mradi wa kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa "Tunaweza
kwa pamoja kutokomeza vitendo vya
udhalilishaji wa kijinsia" kwa wanawake na wasichana unaotekelezwa na chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA -ZANZIBAR kwa kushirikiana na UN - WOMEN, Asia Hakim
Makame amewataka waandishi wa habari kutumia taaluma zao kuielimisha jamii juu
ya masuali mbali mbali ya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na wasichana.
Alisema
waandishi wa habari wanamchango mkubwa katika kutoa elumu ya kupinga vitendo
vya udalilishaji wa kijinsia kwa wanawake
na watoto hususan katika sekta zisizo rasmini ikiwemo ya uchumi,elimu, afya na
usafirishaji.
Aliyasema
hayo wakati akifungua mafunzo ya
uandishi wa habari hizo yaliojumuisha waandishi kutoka vyombo mbali mbali vya
habari watakao tekeleza mradi huo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
TAMWA Mkanjuni Chake chake Pemba.
Alisema
kuna maeneo yenye vikwazo mbali mbali vya
udhalilishaji kwa wanawake na wasichana hivyo ni vyema kwa waandishi
wa habari kuiambia jamii juu ya vitendo na viashiria vitakavyopeleka udhalilishaji huo.
Aidha
aliwataka waandishi hao kuyafikia maeneo ya umma yanayotolewa huduma mbalimbali ikiwa pamoja
na masoko, vituo vya afya, skuli na madrasa na katika maeneo ya usafiri wa
umma, kutokana na maeneo hayo kua na
matukio mbali mbali ya udhalilishaji,
ambayo hayajapewa kipaumbele.
"Nguvu
za kukemea jambo hili zielekezeni zaidi kwenye maeneo yasiopewa kipaumbele
ikiwa ni pamoja na yenye mikusanyiko ya watu, huko kuna viashiria na matukio
mengi ya vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na wasichana ingawa wengi
hawafahamu hilo,"alifafanua.
Alieleza
kuwa mradi huo unalenga kupunguza athari
zitokanazo na vitendo vya udhalilishaji
wa kijinsia hususan katika Mikoa miwili ambayo
ni KaskaziniPembana Kaskazini Unguja ambako kunaonekana kuwepo kwa tatizo hilo
kwa kiwango kikubwa.
Akiwasilisha
mada kuhusu hali ya udhalilishaji kwa
wanawake na wasichana katika mafunzo hayo Mkurugenzi Haji Nassor Mohammed alisema
takwimu zilizotolewa na Ofisi ya
mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaonyesha kua wanawake na
watoto ndio waathirika wakuu wa matendo ya udhalilishaji.
Alisema
kuwa udhalilishaji hutokea katika namna tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na
matumizi ya lugha chafu, kupewa majina mabaya na hata matusi mambo ambayo
huonekana ni ya kawaida katika jamii.
"Tukizungumzia
udhalilishaji takwimu zinazoonyesha waathirika wengi ni wanawake watoto na
wasichana, ambao hupatwa na
udhalilishaji wa namna mbali mbali ikijumuisha matumizi ya lugha chafu, majina mabaya na hata matusi, ingawa jamii
huyachukulia haya kama mambo ya kawaida,
alieleza.
Nao
washiriki wa mafunzo hayo Mwamize Khadija Ali Yussuf na Salim Hamad Faki walisema
mafunzo hayo yatawawezesha kuibua ,
kufuatilia na kuielimisha jamii juu athari na namna ya kuchukua tahadhari na
kujikinga na vitendo hivyo kwa wanawake na wasichana.
Aidha
waliahidi kuyafanyia kazi mafunzo waliopewa ili kuikinga jamii yao na matendo
hayo maovu, ambayo kwa kiasi kikubwa
huathiri uchumi na ustawi wa wanawake na wasichana.
MWISHO


Comments
Post a Comment