NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WAJASIRIAMALI kisiwani Pemba, ambao bado hawajazisajili biashara zao, wamekumbwa kufanya hivyo haraka, ili wawe na sifa wakati wanapoomba misaada ama kuingia, katika mashindani mbali mbali.
Ushauri huo umetolewa leo Septemba 18, 2025 na Mkurugenzi
mtendaji wa Jumuiya ya kitaifa ya wafanyabishara Zanzibar ‘ZNCC’ Hamad Hamad,
alipokuwa akizungumza na wajasiriamali hao, wakati akiyafungua mafunzo, ya
umuhimu wa usajili wa majina ya biashara na bidhaa zao, yaliyofanyika ukumbi
wa Manispaa Chake chake.
Alisema, njia moja kwa wajasiriamali hao kufikia ndoto
zao, suala la kusajili bidhaa zao na majina ya biashara, haliepukiki, ikiwa
wana malengo ya kufika mbali.
Alisema, unapoisajili biashara na jina la biashara, huwa
ni kuilinda na kujihakikishia kuipandisha hadhi, kama zilivyo kwa biashara nyingine
za makampuni.
‘’Niwatake haraka sana, ambao hawajajisajili ‘BPRA’
kufanya hivyo, maana kinyume chake, jina la bidhaa zako ambazo zimeshakuwa
maarufu kama hujazisajili, huna hakika ya kubakia nazo,’’alifafanua.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo mtendaji wa ZNCC,
Hamad Hamad, aliwataka wajasiriamali hao, kujiunga na jumuiya hiyo, ili wawe na
sauti moja, wanapokuwa na changamaoto zao.
Alieleza kuwa, ZNCC ndio mkombozi kwa wajasiriamali wote
wa Zanzibar, na hasa ikiwa wataamua kujiunga, ili kuwa na suati ambayo, itasaidizi
kuzipatia ufumbuzi changamoto zao.
Wakati huo huo, Mkurugenzi huyo Mtendaji, aliwahimiza wajasiriamali
hao, kuendelea kutengenza bidhaa zitokanazo na zao la mwani, kwani bado soko
lake liko juu.
‘’Na bahati nzuri kwa sasa baada ya suati zetu, serikali
imesikia kilio chetu, na wameamua kujenga kiwanda cha kuusarifu mwani, na kuachana
na kuzalisha na kuuza kama ulivyo, jambo ambalo faida ilikuwa ndogo,’’alifafanua.
Mapema mtendaji kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali
Zanziba ‘BPRA’ Pemba Yussuf Juma Ali, alisema suala la kusajili jina la biashara
ni lazima, kwa mujibu wa sheria, ili kuepusha mvutano na wafanyabishara mwingine.
Akiwasilisha mfumo wa kielektroniki unaobeba taarifa za
bidhaa husika ‘barcode’ mtendaji kutoka Jumuiya ya kitaifa ya wafanyabiashara
Zanzibar ‘ZNCC’ Tumai Soud, alisema mfumo huo ni muhimu, katika kuipa thamani
bidhaa husika.
Alisema, mfumo huo ndio chanzo kwa mteja kuinunua bidhaa
husika, kutokana na kumpa taarifa zote, aina ya bidhaa, malighafi iliyotumika
na muda wa mwisho wa matumizi.
‘’Suala la msimbomlia ‘barcode’ ni vyema nyinyi wajasiriamali
mkaweka, ili kuhakikisha bidhaa zenu, zinakuwa zinawavutia wateja,’’alifafanua.
Aidha mtendaji huyo, aliwafahamisha kuwa, namba za
biashara ‘barcode’ kwa Tanzania huanzia nambari 620 na
kufuatiliwa na namba nyingine, wakati kwa Kenya inaanzia nambari 616.
Mjasriamali Fatma Abdalla Nassor, alisema wakati umefika
kwa BRA, ZBS, ZNCC kuwangalia kwa jicho la huruma, ili kuwapunguzia gharama za
usajili.
Kwa upande wake mjasiriamali kutoka Kifumbikai Wete, Fatma
Nassor, alisema bado ZBS, wamekuwa wazito kuwahudumia, jambo linalowarejesha
nyuma.
Mafunzo hayo ya siku moja, yaliowashirikisha wajasiriamali
53 kutoka wilaya nne za Pemba, yameandaliwa na ZNCC ikiwa ni sehemu ya utekelezaji
wa mpango kazi wa 2020/2025.
Mwisho
Comments
Post a Comment