NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
WANANCHI wa kijiji cha Ole Kianga wilaya ya Chake chake, wamesema ajali nyingi
za barabarani zinasababishwa na waendeshaji wa bodaboda kutokana na
utumiaji mbaya wa barabara wanapokuwa kwenye shughuli zao.
Wameyasema hayo leo Septemba 19, 2025 walipokuwa wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, juu ya
uwepo wa ajali nyingi zikisababishwa na waendeshaji wa bodaboda.
Wakieleza kuwa ajali hizo kwa sasa zimekuwa tishio na
kuwaweka roho juu, wanaotumia usafiri wa bodaboda kupitia vyombo hivyo.
Mpanda bodaboda Aisha Ali Abdullah alisema ni usafiri unaorahisha kwa sasa,
ingawa wamekuwa hawana amani, kutokana na waendeshaji kukosa umakini.
Alisema kuwa ndani ya barabara kumekuwa na vyombo vya usafiri kila aina, ingawa
kwa upande wa pikipiki aina ya bodaboda, zimekuwa zikihatarisha usalama wao.
Alifafanua kuwa waendeshaji bodaboda hao, weingi wao wamekuwa ndio chanzo
kikubwa cha kusababisha ajali barabarani, kwani wamekuwa wakitumia barabara.
"Niseme dhahiri hawa waendeshaji bodaboda, ndio chanzo kikubwa
wanaosababisha ajali kw akule kuwa matumizi ya kizembe barabarani,’’aliafafanua.
Kwa upande wake muendesha bodaboda katika kituo cha Ole Kianga
Wahid Khamis Mohamed, alisema, sio sahihi kuwa, wao ndio chanzo cha ajali, kama
wingine wanavyodai.
Alisema kuwa sio waendesha bodaboda wote wanaosababisha ajali, kwani inategemea
na uendeshaji wa mtu na utumiaji wa chombo chake.
"Ijapokuwa, na sisi ni wadau wakubwa wa watumiaji barabara tunao na
wenzetu, lakini chakushangaaza, pakitokea ajali tunaelekezewa kidole sisi,’’alilamika.
Mtumiaji wa usafiri wa bodaboda Maryam Mabrouk Khamis
alisema wapo wale waendesha bodaboda wanaojita, majina sio mazuri, na wakiingia
barabarani huendesha vyombo watakavyo wao.
Kwa mujibu takwimu, kutoka Ofisi ya Taifa ya Mtakwimu na
jeshi la polisi ya matukio ya usalama barabarani kwa Zanzibar ni 49
zilizosabishwa na waendesha piki piki.
Ikafahamika kuwa, hizo ni zile zilizoripotiwa kwa mwaka jana
pekee, ambapo ni punguzo la ajali12 ikilinganishwa na ajali 61 za mwaka 2023.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, kwa ajali hizo zimesababisha vifo
37, ikilinanishwa na vifo 53 vilivyotokea kwa mwaka 2023, ambapo sawa na kupungua
kwa vifo 16.
Aidha kwa mwaka jana, kuliripotiwa majeruhiwa 43,
waliotokana na ajali hizo, ambapo kwa mwaka 2023, taarifa zinaonesha kupungua
kwa majeruhi 12, baada ya kubainika kuwa ni 55.
Upande mwingine,
taarifa ikafafanua kuwa, kwa Tanzania nzima, kwa mwaka jana pekee, kuliripotiwa
vifo 378 vilivyosababishwa na ajali 432 za pikipiki.
Aidha kati ya ajali
hizo pekee kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, ofisi
hiyo ikaeleza kuwa, kulikuwa na majeruhi 395.
Mwisho



Comments
Post a Comment