NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
MGOMBEA urais wa Zanziba kwa tiketi ya Chama ADA-TEDEA Juma Ali Khatib, amesema
pindi wazanzibari wakimpa ridhaa ya kuwa Rais, atahakikisha anaanzisha mfuko
maalumu utakaowsaadia, kuwawezesha vijana kusoma bila ya malipo.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,
kwa chama hicho, uliofanyika Kangagani wilaya ya Wete Pemba.
Alisema kuwa makundi hayo watayazingatia sana kwa sababu ni watu muhimu kutokana
na uhitaji wao wa kimaisha, huku akiamini elimu ndio mwarubaini wa changamoto
zao.
Alisema, mfuko huo hautokuwa
na ubaguzi, na kubwa zaidi ni kuwapatia vijana gharama za masomo, ili kuhakikisha
wanafinikisha ndoto zao.
Mgombea huyo
alisema, inaonekana vijana waliowengi wanahamu wa kujiendeleza kielimu, ingawa
changamoto ni kukosa mfuko wao maalum.
‘’Niwahakikishie
vijana, pindi nikipata ridhaa ya kuwa rais wan chi hii, moja ya kipaumbele ni
kuanzisha mfuko ambao utawasaidia vijana kielimu,’’alifafanua.
Ahadi nyingine
ambayo mgombea huyo alisema, ni kuyashughulikia makundi ya mama na watoto,
akisema ataandaa mazingira ambayo wananufaika na huduma mbali mbali.
‘’Ni kweli wanawake
na watoto nao ni sehemu ya familia, hivyo kama nikipata ridhaa nao, watakuwa
ndio wa kwanza kutatuliwa changamto zao,’’alisema.
Kundi jingine
ambalo ameahidi kulitupia jicho na kulipatia haki zao stahiki ni wajane, ambao
kwa sasa wanalalamikia upatikanaji wa haki zao.
‘’Kuna familia baba
ametangulia mbele ya haki na mama anabaki peke yake, hana msaidizi maisha
yanakuwa magumu, hivyo ADA-TADEA ndio mkombozi wao,’’alifafanua.
Mapema mgombea wa urais
wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, George Gabriel Bussung alisema, ni ya
chama hicho ni kujenga taifa jipya na tajiri lenye kujitolea.
"Tunataka taifa
Tajiri, lenye viwanda vya kutosha pamoja na kudumisha amani na utulivu katika nchi
yetu,"alieleza.
Mgombea mwenza wake, Ali Makame Issa alisema haina haja ya wafuasi hao
kuzuia kura ya mapema, juu ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba
mwaka huu.
Alisema kuwa Tume, imafanya maamuzi hayo kwa utaratibu maalumu ya kuwaandalia
wapiga kura ambao watakuwa na shughuli maalum, siku ya kupiga kura kwa watu
wote.
"Kura hailindwi
tuachie Tume, wafanye kazi yao na unapomaliza kupiga kupiga kuram turudi
nyumbani, na tuziache mamlaka ziendelee na taratibu nyingine,’’alifafanua.
Katibu mkuu Taifa wa chama hicho, Saleh Mohamed Msumari, alisema wanawajali wakinamama kwa kuwapatia haki sawa zinazostahiki.
Hata hivyo, alisema wanampango wa kujenga daraja maalum la kwendea Kisiwa cha
kojani, pamoja na wavuvi kupatiwa maboti makubwa ya uvuvi
MWISHO.
Comments
Post a Comment