NA MARYAM SALUM,
PEMBA @@@@
MGOMBEA urais wa Zanzibar
kwa tiketi ya Chama cha Wakulima, ‘AAFP’ Said Soud Said amewataka wananchi,
kutokubali kushawishiwa na mtu au chama, kuchafua amani, na badala yake kuilinda
na kuitunza kwa maslahi ya umma.
Alitoa wito huo
wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara, wa kampeni kwa chama hicho,
uliofanyika Kiuyu wilaya ya Wete Pemba.
Alisema kuwa, suala
la uwepo wa uchaguzi wa vyama vingi, hakuna uhusiano wowote na uvunjifu wa
amani, hivyo ni vyema kila mmoja kuliheshimu hilo.
Alieleza kuwa, siasa,
mikutano ya kampeni na hatimae uchaguzi wa kuwachagua viongozi mbali mbali, ni
jambo la kupita, ingawa kuichafua amani na kuirejesha ni jambio zito.
Mgombea huyo wa
urais, aliwaasa wananchi hao na hasa vijana, kujitenga mbali na chama ama kundi
la watu, lenye dhamira ya kutaka kuchafua amani ya nchi.
‘’Mimi nikiwa
mgombea urais wa Zanzibar, niwaeleze kuwa, kwanza tuichaguweni amani na kisha
ndio tuwapigie kura wagombea wetu,’’alifafanua.
Katika hatua
nyingine, Mgombe huyo aliwaahidi wananchi wa Zanzibar, kama endapo atapata
ridhaa, atahakikisha wale ambao walipata ajali ya kuzama kwa meli ya Mv.spice
Island kutafuta familia zao na kuzilipa fidia.
Alisema, familia
hizo ni sehemu ya wazanzibari, hivyo bado tokea zilipokumbwa na kadhia hiyo,
hazipewa fidia, jambo ambalio analikusudia kulifanya.
‘’Naelewa kuwa,
zipo familia ambazo zilipoteza wapendwa wao, lakini hadi leo hakuna fidia
ambayo walipewa na serikali, lakini kama nitapata ridhaa, nitawasaidia,’’alifafanua.
Aidha sera yake nyingine
ambayo aliinai Mgombea huyo, ni kuhakikisha anapandisha bei zao la karafuu na
kunua kwa shilingi 40,000, ili kuwabufaisha wakulima.
Alieleza kuwa,
ameona wakulima waliowengi wa zao la karafuu, wamekuwa hawanufaiki vilivyo na
jasho, hivyo anaamini kama akiingia Ikulu, suala la kupandisha bei ni lazima.
Wakati huo huo Mgombea
huyo wa urais wa kwa tiketi ya AAFP Said Soud Said, aliwahakikisha wananchi hao
na wanachama wake kuwa, ataweka taa kwenye maeneo makubwa ya kuzikia.
Hata hivyo, aliwataka
wananchi siku ya kupiga kura itakapofika kwenda kwenye vituo kupiga kura na
kurudi nyumbani, na kuiacha Tume za uchaguzi kufanya kazi zake.
Kwa upande wake
Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Omar Juma Said alieleza kuwa chama, kina
dhamira ya kuwakomboa wananchi wote kiuchumi.
"Mgombea wetu
kwanza ni mkulima, na kilimo ndio kila kitu, sasa tunahitaji ridhaa yenu ili
aingie ikulu na kuhakikisha tunastawisha wananchi kiuchumi,’’alieleza.
Aidha aliwataka wananchi wa Kiuyu kufikiria
kwanza kabla ya kufanya maamuzi, ili waweze kuchagua kiongozi atakae waletea
maendeleo na siyo kuangalia chama au mtu.
Nao viongozi wa
Chama hicho kutoka katika Mkoa wa kaskazini na wilaya ya Chake pamoja na mgombea
ubunge wa jimbo la Wawi, Khamis Mohamed Haji, walieleza kuwa si vyema, wananchi
kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.
Viongozi hao waliwataka
wananchi wa Kiuyu na maeneo mingine, kuunga mkono chama cha AAFP, kwa kumchagua
mgombea huyo, ili waweze kupata maendeleo zaidi.
MWISHO.
Comments
Post a Comment