NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
MGOMBEA urais wa Zanzibar wa tiketi ya chama cha Alliance for Democtratic
Change ‘ADC’ Hamad Rashid Mohamed, amsesema moja ya kipaumbele chake, kama atapata
ridhaa ya kuwa Rais wa Zanzibar, atahakikisha walimu wa madrsa kuwalipa
mishahara kama, walivyo wafanyakazi wingine.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho,
zilzofanyika uwanja wa Gombani kongwe Chake Chake Pemba.
Alisema kuwa atahakikisha walimu wote wa madrassa, atawalipa mishahara kama wafanyakazi wingine, pamoja kuwapatia vifaa vya TEHAM.
"Mukinipa ridhaa ya kuwa Rais wa Zanzibar, nitahakikisha walimu wote wa madrassa, nitawalipa mishahara kama wafanyakazi wengine wa utumishi wa umm," alisema.
Aidha Mgombea huyo, alisema kama atapata ridhaa hiyo, ataimarisha kilimo cha
mpunga, ili kuhakikisha hakuna mwananchi anayenunua mchele.
Alieleza, kwa ardhi ya Zanzibar ilivyo kubwa, na kwa uzoefu
wake wakati alipokuwa Waziri wa Kilimo, ana hamu kupata ridhaa, jambo hilo
linawezekana mno.
‘’Nikiwa Rais wa Zanzibar, suala la kuimarisha kilimo hasa
cha mpunga, ni jambo ambalo, nitalingalia kwa nguvu, kwani ni aibu kuona
tunaagiza kila kitu kutoka nje ya Zanzibar,’’alifafanua.
Katika hatua nyingine, Mgombea huyo urais wa Zanzibar kwa
tiketi ya ADC Hamad Rashid Mohamed, aliwataka wanachama wake, kutunza amani na
utulivu kuelekea uchaguzi mkuu.
Mapema Mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,
kwa tiketi ya ‘ADC’ Wilson Elias Mulumbe na Mgombea mwenza wake, Shoka Khamis
Juma, walisema kuwa, endapo watapata ridhaa, watahakikisha wanabadilisha
katiba.
Alisema kuwa ndani ya siku100 mchakato huo utaanza kubadilishwa kwa
sheria hizo na kuanza kutumika, ili ziwe na mwalekeo mpya wa taifa.
"Tutabadilisha katiba mpya, ambayo mchakato wake tayari ulishaanza, hivyo
itakuwa ni rahisi kwetu sisi ADC, maana ulishaanza zamani,’’alisema.
Nae Mwenyekiti wa wanawake taifa kutoka ADC Nadhira Ali Haji,
aliwataka wanawake kuhakikisha, hawachokozeki na kuwa sehemu ya uchafuzi wa
amani.
Alisema kuwa Tanzania ni nchi ya amani na utulivu na amewataka kuendeleza amani iliyotawala, na kuiacha Tume ya Uchaguzi kufanyakazi zake kwa uhuru.
"Niwatake wanawake wenzangu kudumisha amani na utulivu uliotawala nchini
mwetu, na tuiache Tume ya Uchaguzi ifanye kazi yake,’’alifafanua.
Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Taifa Mwalimu Hamad Azizi alisema, aliwahakikishia
wazanzibari, kuwa endapo watamchagua mgombea Hamad Rashid Mohamed, atahakikisha
amani na maendeleo ya nchi yatapatikana.
Nae Makamo Mwenyekiti wa ADC Tanzania Bara Hassan Shaaban Mvungi, alisema kuwa kiongozi pekee anaestahiki kushinda nafasi ya uraisi ni Hamad Rashid Mohamed, juu ya utekelezaji wa sera wa michezo, uchumi wa buluu, kuwezesha wavuvi kwa kuzalisha vitoweo kupitia biashara hizo.
MWISHO.
Comments
Post a Comment