AFISA Mdhamini wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Mohamed Nassor Salim
amesema 18,236 kisiwani Pemba, wanatarajiwa kufanya mitihani yao ya taifa ya darasa
la saba, kuanzia asubuhi hii.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi
wa habari hizi, ofisini kwake mjini Chake chake, kuelekea kufanyika kwa mitihano
hiyo leo hii.
Alisema kuwa wanafunzi hao wanatarajiwa kufanya mitihani yao ya darasa la saba,
wakiwa wameandaliwa mazingira mazuri, yatakayowawezesha kufanya vizuri na
kujiamini.
Alieleza kuwa, kuwa wanafunzi hao wanatarajiwa
kufanya mitihani hayo, wakiwemo wanawake 9,235 na wanaume 9001, kwa muda wa
siku nne za mitihani hiyo.
"Sisi wizara tumejipanga vyema katika maandalizi mazuri kwa wanafunzi wetu
wa darasa la saba, kukabiliana na mitihano yao ya taifa,’’alifafanua.
Aliongeza kuwa, mitihani hayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia leo Septemba, 15,
mwaka huu katika vituo vyote vinavyohusika vya skuli za serikali na vile
vya binafsi.
Alielezea kuwa kwa Pemba maandalizi ya mitihani yamekamilika na wanatarajia
kuwa na vituo 139 kwa darasa la saba, kwa skuli ambazo zimesajiliwa.
Afisa Mdhamini huyo, aliongezea kuwa wapo wasimamizi wakuu 139, ambapo ni
wastani wa kila kituo mmoja, huku kukiwepo waalimu watakaosimamia mitihani 601.
katika hatua nyingine, alifafanuwa kuwa wizara imejipanga katika suala la
ulinzi, kwa askari wasiopungua 278, ili kuhakikisha mitihani inafanyika
kwa amani na utulivu.
Afisa Mdhamini huyo, alisema kuwa, badaa ya kumalizika kwa mitihani hiyo, kutakuwa
na mitihani ya upimaji kwa darasa la tatu, ikiwahusisha wanafunzi 18,427.
Alisema kisha, itafuatiwa na upimaji wa wanafunzi wa darasa la nne, ambao wao 1,949
kwa wilaya zote nne za Pemba.
MWISHO.
Comments
Post a Comment