UZINDUZI KAMPENI ZA CCM PEMBA, RANGI NJANO, KIJANI ZAANZA KUWACHANGANYA WAPINZANI, NDEGE YANOGESHA UTAMU
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
SHANGWE, nderemo na
vifijo vimetawala katika kiwanja cha Gombani ya Kale, wilaya ya Chake Chake
Pemba, baada ya maelfu ya wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi ‘CCM’
wakiwa na kijano na njano kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi wa kampeni
za chama chao.
Umati huo
uliofurika leo Septemba 15, 2025 unaashiria mshikamano na imani kubwa ya wananchi walioionesha kwa
CCM kupitia mgombea wake Dk. Hussein Ali Mwinyi kuelekea uchaguzi mkuu mwaka
huu.
Kiwanja hicho
kilipambwa na rangi za kijani na njano huku vijana, wanawake, wazee wenye
mahitaji maalu, waliovalia rangi hizo walionekana barabarani wakitembea kwa
furaha.
Mbali na dufu
uwanjani, kulipambwa na vikundi vya ngoma, muziki wa hamasa huku bendera za chama
hicho, zilizokuwa zikipepea kila kona.
Kwenye uwanja huo,
usipokuwa makini kutokana na kushimari na kuenea kwa burudani, huwezi kujua
ucheze na uitikie kikundi kipi cha ngoma uwanja hapo.
Lakini wingine,
waliovalia vazi maalum, ambalo liliunga na sare za CCM, walionekana wakiimba na
kucheza nyimbo za kampeni zinazomsifu mgombea urais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali
Mwinyi.
Shangwe la wana CCM
lilionekana kama kutaka kuzima kidogo, ingawa bila ya kujali kijua kikali
uwanjani, yalipoingia majira ya saa 7:30 mchana, nderemo zilidia, baada ya
kupita ndege ya mgombea urais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi.
Ndege hiyo, ilipita
kwa madaha, ikiwa imepambwa na picha za mgombea huyo, huku ikipeperusha bendera
maalum, na kuzungumka eneo la uwanja wa kampeni na mitaa ya kisiwani Pemba.
Wakizungumza jana
na Zanzibar Leo, uwanja hapo walisema, wanananchi kisiwani Pemba sasa wameamka,
na kamwe hawatakubali kupelekeshwa tena kutokana na maendeleo yanayofanywa.
Walisema Pemba ya
leo si ile ya miaka iliyopita, kwani chini ya uongozi wa Rais Dk. Hussein Ali
Mwinyi, kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo, katika kila sekta.
Mkaazi wa Chake Chake Mohamed Salim, alisema miradi ya
barabara, afya, elimu na upatikanaji wa maji safi na salama, ni ishara nyingine
ya ushahidi tosha kwa CCM na wagombea wake wote.
Nae Maryam Haji Makame wa Wawi, alisema barabara
zilizojengwa na kufanyiwa ukarabati, zimeongeza urahisi wa usafirishaji wa
bidhaa na abiria kati ya vijiji na miji mikuu ya Pemba.
"Hawa
wapinzani kila siku wanatupelekesha tu, wao wanachojali ni matumbo yao wala
hawatufikirii sisi wananchi, lakini ndani ya miaka mitano ya Dk.Mwinyi, maendeleo tunayaona,’’alisema.
Alisema,
wanachokijua Chama cha ‘ACT-Wazalendo’ ni kuhamasisha vurugu na sio kuwaletea
maendeleo, kwa sababu kiongozi mkuu anaposimama jukwaani ni lawama na kukebehi
yaliofanywa.
Naye Asha Abdalla wa Mkoani alisema, sekta ya afya
imeimarika kupitia ujenzi wa vituo vipya na upatikanaji wa dawa kwa urahisi
huku wagonjwa wanaolazwa wakipatiwa huduma za matibabu na chakula bila ya
malipo.
Naye Ali Khamis mkaazi wa Wete, alisema sekta ya
elimu, imepiga hatua kubwa kutokana na ujenzi wa skuli mpya za ghorfa na kuimarika
kwa mazingira ya kujifunzia.
Aidha, Fatma Omar wa Micheweni alisema, kuwa huduma
za maji safi, zimefikia maeneo mengi, hivyo kupunguza adha ya kutembea umbali
mrefu kutafuta huduma hiyo.
Alisema wana kila sababu ya kumuunga mkono Dk. Mwinyi,
kutokana na jitihada zake za kuiletea Pemba maendeleo endelevu, na fursa za
kiuchumi kwa wananchi.
Alawi Makame Alawi alisema yeye siyo mwanachama wa CCM,
lakini ifikapo Oktoba 29, atampigia kura Dk. Mwinyi, ili aendelee kuwaletea
maendeleo wananchi kwa ujumla.
Naye Faki Hamad
Ahmada alisema, Pemba inajivunia mema mengi, yaliyoletwa na Dk. Mwinyi na kubwa
zaidi ni amefanikiwa kuwaunganisha wananchi na kuwa wamoja, na kuondoa
misuguano ya kisiasa.
Kisha mgombea huyo
wa urais aliwasilia uwanjani hapo, na kupokelewa kwa shangwe kubwa, huku
wajumbe halmshauri kuu ya CCM taifa, wenye viti wa mikoa, wilaya, watia nia ya
nafasi kadhaa wakiungana pamoja.
MWISHO
Comments
Post a Comment