NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha NRA, Khamis Faki Mgau amesema,
pindi akipata ridhaa ya kuongoza nchi, atahakikisha kila mwalimu wa skuli ngazi
ya cheti, atamlipa mshahara wa shilingi 1.5.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara,
akifungua kampeni kwa chama hicho, uliofanyika Kangagani wilaya ya Wete Pemba.
Alisema kuwa kila mwalimu wa skuli kwa ngazi ya cheti, atamlipa kima hicho,
ingawa wale wenye elimu ya juu watavuuka kima hicho.
"Walimu wa
skuli wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuwafundisha watoto wetu, ingawa wamekuwa
wakipokea mishahara midogo, nikiiingia madarakani, nitarekebisha fedha za
wafanyakazi hao,"alifafanua.
Ahadi nyingine Mgombea huyo aliotoa ni kuweka mazingira laini, ili kila mmoja
aliyefikia uamuzi wa kufunga ndoa, iwe rahisi.
Alisema kuwa
ifikapo mwisho wa mwezi kila kijana anahakikisha kumlipa shilingi laki 900,000,
ili kumuwezesha kumudu mke zaidi ya mmoja.
"Nikosa la jinai kumuona kijana ana mke mmoja na atakaekiuka sheria hiyo,
kifungo cha miaka sita, kitamuhusu,’’alifafanua.
Kwa upande wake, Mgombea wa Urais wa Jamuhuri
wa Muungano wa Tanzania kwa tekiti ya chama hichi, Khamis Ali Hassan, alisema
ingawa Dk. Mwinyi kupitia Mbunge wa Kojani amefanya mingi, amewahakikisha wananchi
kuyaendeleza,’’alifafanua.
Alisema kuwa
atahakikisha analeta maendeleo makubwa kwa kueka mbiundo mbinu maji safi na
salama, ili kuhakikisha huduma hiyo inakuwa rafiki kwa wananchi.
"Chama cha NRA,
kipo kwa kuendeleza mazuri kama yanavyotekelezwa na Rais wetu wa Zanzibar na
Rais na mwenzake wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alieleza.
Nae Katibu Mkuu ambae pia ni mgombea kwa nafasi ya uwakilishi wa Jimbo la
Kojani Khalid Makame Issa, aliwataka wananchi kuwa watulivu siku ya
upigaji wa kura, kama ilivyotangazwa na Tume za Uchaguzi,
Alisema kuwa amani
ni kitu muhimu ndani ya nchi, endapo ikitoweka wahenga wakubwa watakua ni watoto,
wazee watu wenye ulemavu na wanawake.
"Niwatake wananchi wote kwenda kupiga kura tarehe 29 kwa amani, na
tuyaache maamuzi yaliyotolewa na Tume kwa upigaji wa kura ya mapema, kwa ajili
ya watu maalum,’’alifafanua.
Kwa upande wako
Makamu Mwenyekiti wa NRA Bimkubwa Abdalla Said, aliwataka wananchi kukipigia
kuwa za ndio chama hicho, ili kiwaletea maendeleo yenye jija.
Alisema kuwa kupitia mamlaka husika ameviomba vyombo vya sheria
kuchukua hatua kwa mitandao inayomfachua, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania.
"Tupo nae bega kwa bega viongozi wetu wote wawili ili kulinda amani na
kuleta mabadiliko, katika nchi yetu," alieleza.
MWISHO.

Comments
Post a Comment