NA
MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@
Watu
wenye ulemavu wa Uziwi wameziomba taasisi Serikali na binafsi zinazotoa huduma mbali mbali za kijamii,
kuweka wa kalimani wa alama katika taasisi hizo ili kuhakikisha upatikanaji wa
huduma bora kwa watu wote.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti
watu wenye ulemavu wa uziwi walisema, wamekua wakichelewa kupata huduma bora na stahili katika baadhi
ya taasisi kutokana na kutokuwepo
mawasiliano mazuri kati yao na watoa huduma, hali inayosababishwa na upungufu
wa wakalimani wa lugha za alama katika
taasisi hizo.
Mmoja
kati ya watu wenye ulemavu wa uziwi Zuhura
Kombo Omar kutoka Mjimbini Mkoani Pemba alisema, katika taasisi nyingi
za utoaji huduma za kijamii kumekua na
uhaba wa wakalimani wa lugha ya alama hali inayosababisha kutopata huduma bora
na kwamuda sahihi.
Alisema
kukosekana kwa wataalamu hao unasababisha kutokuwepo kwa mawasiliano mazuri
jambo linalosababisha kukosekana na kwa
huduma bora pamoja na haki zao msingi ambazo ni lazima kuzipata.
"
Tunapokwenda katika taasisi za utoaji huduma zikiwemo za serikali na zisizo za
kiserikali tumekua tukichelewa au kutopata huduma stahili, kutokana na
kukosamawasiliano sahihi hali inayosababishwa na kutokuwepo kwa wakalimani wa lugha ya alama
pamoja na watoa huduma wenye ujuzi wa lugha hio ," alisema.
Nae
Mbarouk Ali Saleh kutoka Mtambile Mkoani Pemba alisema, changamoto za kutokuwepo kwa wakalimani wa lugha za alama
katika sehemu za kutoa huduma za jamii, kunasababisha baadhi ya watu wenye
ulemavu wa uziwi kushindwa kupata huduma
stahili kutokana na kutokuwepo watu
wenyeuwezo wa kufahamu mahitaji yao.
Alieleza
kuwa iwapo kila taasisi itaweka watoa huduma wenye taaluma ya lugha za alama itasaidia kurahisisha mawasiliano
pamoja na upatikanaji wa huduma bora kwa kila mmoja, jambo litakalosaidia
ustawi wa jamii kwa ujumla.
Nae
Fatma Kombo Omar wa Mjimbini Pemba alisema, mazingira rafiki kwa watu wenye
ulemavu katika taasisi za utoaji huduma muhimu,
ni moja kati ya hatua muhimu katika kuhakikisha usawa na upatikanaji wa
haki zao za msingi.
Aidha aliiomba serikali kuhakikisha uwepo wa
wataalamu wa lugha za alama katika taasisi hizo
ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora kwa watu wenyeulemavu wa
uziwi.
"
Mazingira rafiki kwetu ikiwemo wakalimani wa
lugha za alama ni hatua muhimu katika kuhakikisha usawa na upatikanaji
wa haki na huduma bora, hivyo ni vyema kwa serikali kulizingatia hili ili
kuhakikisha tunapata mawasiliano sahihi tunapofuata huduma, " alieleza.
Kwaupande
wake Mratibu Baraza la Taifa la watu
wenyeulemavu Pemba Mashavu Juma Mabrouk alisema, nivyema kwa Serikali na
taasisi zote za binafsi zinazotoa huduma kwa jamii kuweka wataalamu wa lugha za
alama ili kurahisisha mawasiliano wakati wa utoaji huduma kwa kila mtu.
Aliongeza
kua, baraza limekua likichukua jitihada kadhaa ikiwemo kuzishauri baadhi ya
taasisi hizo ikiwemo wizara ya Afya
kuweka wakalimani wa lugha za alama katika taasisi hizo, lengo ni
kujumuisha watu wote katika upatikanaji wa huduma mbali mbali nchi.
Kwa
mujibu wa kifungu cha 32 (1) (d) cha Sheria ya watu wenye ulemavu ya Zanzibar
ya mwaka 2022 kinaeleza kua taasisi yeyote ya Serikali au binafsi itahakikisha
taratibu za utoaji na upatikanaji wa huduma zinazingatia mahitaji maalum ya
watu wenye Ulemavu.
MWISHO
Comments
Post a Comment