Skip to main content

NYENZO UTEKELEZAJI SERA YA MAENDELEO YA WATOTO IMEPATIKANA




Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Abeida Rashid Abdallah amesema Mpango Jumuishi wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto wa Miaka Mitano (5) utakapokamilika utakuwa nyenzo muhimu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Watoto na Malengo ya Kitaifa na Kimataifa.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu 01-3/09/2025 cha kuandaa Mpango huo kilichofanyaka katika Hotel ya Visitors Inn, Jambiani, Mjini Unguja kilicho andaliwa na Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji wa Utendaji Serikalini Zanzibar (ZPDB).

Amesema Mpango Jumuishi wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto wa Miaka Mitano unahimiza huduma za afya, chanjo, lishe bora na ulinzi wa mtoto na malezi yenye mwitikio, hivyo kuchangia moja kwa moja kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs),hususan lengo nambari nne (4) linalohusiana na Kupunguza Vifo vya Watoto chini ya Umri wa miaka mitano.  

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi na mikakati yake ya maendeleo, imeweka kipaumbele kikubwa katika masuala ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (ECD) ili kuhakilisha  kila mtoto wa Kizanzibari anapata malezi bora ili aweze kufikia utimilifu wake (potential).

“Programu hii ni muhimu sana kwa kuwa unajikita katika kuhakikisha kila mtoto wa Kizanzibari anapata malezi bora, afya njema, lishe inayostahiki, ulinzi, na fursa ya kujifunza katika hatua za awali za maisha yake” Amesema Abeida.

Naye Naibu Katibu Mkuu Taaluma,Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Dkt Mwanakhamis Adam Ameir amesema Zanzibar kuna baadhi ya watoto wa darasa la tatu (3) mpaka la saba (7) hawajui kuandika kutokana na kukosa fursa ya kuijifunza katika umri wa awali. 



Hivyo Wizara hiyo pia inafanya jitihada ya kuwafundisha walimu kuhusu Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya mtoto hasa katika ulaji kwani baadhi ya vyakula vinavyouzwa katika mashuleni sio salama  ikiwemo malai na n.k.


Ameeleza kwamba elimu kuhusu Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto  imeanzishwa katika Chuo cha Ualimu Nkutuma, wanafunzi wa kidato cha nne na sita waliopata divisheni ya kwanza na ya pili (one and two) wanafundishwa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ili waweze kuwalea Watoto katika misingi inayohitajika.



Kwa upande wa Wizara ya Afya, Akizungumza Naibu Mkurugenzi kinga Dkt Fatma Kabole amesema changamoto ya Afya ya akili kwa akinamama inaongezeka lakini Jitihada za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi zimesaidia kuboresha huduma za Afya kwa kujenga hosipitali na kuimarisha vituo vya Afya kwa Unguja na Pemba.

Dkt Fatma amesema Wizara ya Afya imejenga hospital nne (4) katika ngazi ya Mkoa, vituo vya Afya 92 vimeimarishwa, vituo 52 ya Afya vituo vinatoa huduma za upasuaji huku vituo 11 vya akinamama vimeimarishwa ili kuwaondolea changamoto inayowakabili.

Akizungumza katika kikao kazi hicho, Mtalaam wa Hifadhi ya Mtoto kutoka UNICEF ndugu Ahmed Rashid Ali amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuekeza katika Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwani faida yake ni sawa na kuwekeza shilingi moja katika biashara na kupata faida ya shilingi saba.

Amesema utafiti umeonesha asilimia 18 watoto wameduma huku asilimia 40 hawakufikia viwango vya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali, hivyo Shirika la UNICEF linafanyakazi ya kushirikina na Serikali ya Mapinzudi Zanzibar kupata kinga na matibabu ya changamoto iliyopo.



Mapema akizungumza, Mratibu wa Programu ya Malezi, Makuzi na maendeleo ya Awali ya Mtoto kutoka ZPDB) Dkt. Maryam Issa amesema lengo la Programu hiyo ni kuhakikisha watoto 276,000 wa Zanzibar wanakua katika mwelekeo unaofaa kwa kuhakikisha wanapata huduma za afya, lishe, ulinzi na usalama wa mtoto ifikapo 2030.

Amesema shughuli mbali mbali zimekuwa zikitekelezwa kupitia program hiyo ikiwemo kufanya utafiti wa hali ya malezi na makuzi ya awali ya mtoto ya Zanzibar (ECD base line survey), ambapo miongoni mwa matokeo ya utafiti huo yameonesha kwamba Takribani asilimia 32 ya watoto wenye umri wa miaka 0–3 Zanzibar wamechelewa kimaendeleo.

Pia Dkt Maryam amesema Programu hiyo imefanya  utafiti mdogo wa kuangalia huduma rafiki za Malezi na makuzi ya mtoto katika masoko, hospitali na skuli za maandaalizi kwa Unguja na Pemba. hali ambayo inaonesha kuwa huduma hizo  hazipo, hivyo programu inakwenda kuweka huduma hizo katika maeneo niliyoyataja.

Aidha amesema Maandalizi ya Mtaala wa Malezi na Makuzi ya Awali ya Mtoto kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii yamekamilika. Na sasa tayari mafunzo kwa wahudumu hao wa afya yameanza katika maeneo ya Unguja na hatua inayofata wanatarajia Kwenda kisiwani Pemba kutekeleza.

Naye Afisa Muandamizi kutoka Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji Maliasili na Mifugo  amesema Wizara hiyo inazalisha asilimia 60 ya vyakula vya mboga mboga, protini, vitamini lakini shida iliyopo ni katika uelewa wa mlaji kwani tatizo lipo kwa wenye watu wenye uwezo na wasiokuwa na uwezo hivyo elimu ya lishe inahitajika kwa jamii.



Programu ya ECD inaratibiwa na Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (ZPDB) na inatekelezwa kwa mashirikiano kati ya Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Wizara ya Kilimo Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo.

MWISHO

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...