NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
DAKTARI dhamana hospital ya Abdullah Mzee Mkoani Pemba,
Khamis Suleiman Khamis, amesema kupatikana kwa makaazi ya ya madaktari,
wanaofanyakazi hospitalini hapo, kumewapa uhakika wa matibabu wagonjwa wale wa dharurua na wa nyakati za usiku.
Alisema, kazi iliyofanywa na Rais wa sasa wa Zanzibar Dk.
Hussein Ali Mwinyi ya kuwajengea nyumba hizo, imeongeza bidii ya kazi kwa madaktari
na kuwahakikisha huduma saa 24 wagonjwa.
Daktari huyo dhamana aliyasema hayo leo Septemba 1, 2025, alipokuwa
akizungumza na waandishi mbali mbali wa habari kutoka Zanzibar na Tanzania bara, katika ziara maalum ya
kuangalia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025.
Alisema nyumba hizo 74 zimenodoa shida ya madaktari hao, kuishi
mbali na kituo chao cha kazi, jambo ambalo lilikuwa likiwawiya vigumu wananchi, wanaohitaji huduma hasa wakati wa usiku.
Alieleza kuwa, baada ya kumalizika ujenzi huo wa nyumba za
kisasa, sasa, madaktari wameondokana na changamoto ya makaazi, ambayo ilikuwa ikiwaathiri pia wapewa huduma.
‘’Kuwepo kwa nyumba hizi 74 za kisasa zenye kila kitu mpaka mashine za kufulia nguo, kwanza lazima sisi
madaktari tumshukuru Dk. Mwinyi, maana sasa kwanza huduma zimeimarika na
madaktari wamepata utulivu wa kazi yao,’’alisema.
Katika hatua nyingine, alisema kwa sasa kumepunguza uwezekano
wa utoro kwa madaktari hao, kwa kupata nyumba hizo za uhakika, karibu na kituo cha kazi.
Akizungumzia huduma katika hospitali hiyo alisema, ni kuwepo kwa kipimo cha kisayansi cha magonjwa ya ndani ya mwili na mishipa midogo midogo ‘MRI’, ambapo hapo awali, hakikiwepo.
Kwa upande wao wananchi wa wilaya ya Mkoani, walisema uwepo wa nyumba hizo kwa sasa, wanauhakika wa huduma za matibabu saa 24, jambo ambalo hapo kabla, walikuwa na dhiki nalo, hasa wakati wa usiku.
Mmoja kati ya wananchi hao Khadija Omar Mohamed, alisema hana
budi kumshukuru Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa uamuzi wake wa
kuzijenga nyumba hizo.
Nae Nassir Abdullkadir, alisema kwa sasa hawana wasi wasi,
kwanza kuwepo kwa madaktari kuishi karibu na hospitali, pamoja na kuimrika kwa
huduma za matibabu.
Rahima Mohamed Haji, alisema anachosubiri kwa sasa ni kufika
siku ya uchaguzi mkuu, kwa ajili ya kumshukuru Dk. Mwinyi kwa kumpigia kura ya ndio.
Wakati huo huo wananchi wa shehia za Kiwani na Kendwa wilaya ya Mkoani, wamesema kukamilika
kwa mradi wa ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji safi lenye ujazo wa lita milioni 1, kumesaidia kupatikana kwa huduma hiyo, kwa uhakika
Asha Iddi Suwedi, alisema kwa sasa wanauhakika wa kuendesha
maisha yake, baada ya ujenzi wa tenki hilo, kumalizika na kupatikana hata umeme unapozimika.
Kwa upande wake Afisa Mdhamini wizara ya Maji, Nishati na
Madini Suleiman Hamad Omar, alisema tenki hilo ni moja kati ya yale matano,
yaliojengwa kisiwani Pemba na Dk. Mwinyi.
Alisema, mradi wa ujenzi huo ambao ulishakamilika tokea mwaka 2022, ulikusudiwa kwa wananchi wa shehia za Kiwani na Kendwa, ingawa kwa sasa, umeongeza shehia nyingine.
Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali
Mwinyi aliweka jiwe la msingi wa nyumba za madaktari Disemba 3, mwaka 2024, na
sasa tayari zimeshamiwa kwa zaidi ya miaka miwili.
Aambapo kwenye Ilani ya CCM iliyomalizika ya mwaka 2020, ibara yake 183 (k) na ibara ndogo ya (ii) ilitamka kuijenga upya hospitali ya Abdulla Mzee Mkoani na uwekazaji wa vifaa vya kisasa vya tiba vya uchunguzi.
Ziara hiyo ya waandishi wa habari, ilitembelea bandari kavu ya Mkoani, nyumba za madaktari Mkoani, uwanja wa michezo Gombani, kiwanda cha mwani, bandari ya Wete na eneo huru la uwekezaji Micheweni. Mwisho
Comments
Post a Comment