NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
AFISA Mdhamini wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Pemba, Mfamau Lali Mfamau amesema, kwa kazi iliyofanywa na
Rais Dk. Mwinyi ya kuimarisha uwanja wa michezo wa gombani, ikiwemo kuezekwa, ni
dhahiri, kwa wanamichezo hana deni.
Alisema, kwa sasa uwanja huo ambao unavutia umezekwa
na kuwafanya watamazaji kutonyeshewa na mvua wala kupigwa na jua, wanapokuwa
uwanjani hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari na wahariri wa vyombo
vya habari vya Tanzania bara na Zanzibar, waliokuwa wakiangalia miradi ya
maendeleo, alisema kwenye michezo amefanikiwa.
Alieleza kuwa, kazi iliyofanywa na Dk. Mwinyi kwa
uwanja huo wa michezo Gombani pekee, imedhihirisha kutekeleza tunu ya wanamichezo.
Alifafanua kuwa, jingine ambalo limeimarishwa ndani
ya uwanja huo, ni uwekaji viti uliozunguruka uwanja wote, jambo ambalo kabla, halikuwepo.
‘’Kwa sas zipo ‘VIP’ ambapo hili linaufanya uwanja
huu kuendelea kua na vigezo vya kimataifa katika anga la michezo,’’alifafanua.
Akizungumzia kuhusu vyumba vya kubadilishia nguo ‘dressing
room’ kwa wachezaji, alisema hapo kabla walilazimika kutoka nje ya vyumba
vyao, kwa ajili ya huduama za kibinaadamu.
Aidha alisema, japo awali kulikuwa na uwanja wa tope,
kama mbadala wa uwanja wa Gombani, ambao kwa sasa umeshawekewa nyasi bandia.
Hata hivyo alieleza kuwa, upo uwanja mwingine wa kisasa
wenye uwezo wa kuchezewa michezo minne (4in one).
‘’Uwanja huu, unaweza kutumika kwa ajili ya mchezo
wa kikapu, mikono, mpira wa meza na mpira wa pete, kwa nyakati tofauti,’’alifafanua.
Baadhi ya wanamichezo, walisema kazi iliyofanywa na
Dk. Mwinyi katika kipindi cha miaka mitano, hasa kwenye eneo la michezo kubwa.
Omar Haji Omar wa Madungu Chake chake, amesema,
uimarisha wa miundombinu ya michezo, imewapa hamu ya kumuungano mkono.
Khamis Hamad Haji wa Wawi, alisem baada ya kazi ya
kuimarisha miundombinu ya michezo, hata kuangalia namna ya kuhamasisha,
inaonekena.
‘’Kwa mfano kuongezeka kwa zawadi kwenye kombe la
Mapinduzi, jambo ambalo linaamsha hisia kwa vilabu na hata watamazaji,’’alifafanua.
Nae Mwajuma Haji Mzaramu, alisema alichokiona kama ni
manufaa, ni kujengewa kwa uzio wa uwanja wa Gombani.
Mwisho
Comments
Post a Comment