NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ WANAWAKE wanaofanya biashara katika masoko ya Mjini Wete na Kifumbikai Wilaya ya Wete Kaskazini Pemba, wameshauriwa kuripoti vitendo vya ukatili na udhalilishaji kwa viongozi wao wa masoko, ili kuchukua hatua zaidi katika kukabiliana navyo. Ushauri huo umetolewa na Msimamizi wa masoko na mazingira Wilaya ya Wete Sadri Mussa Said, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Wete Kaskazini Pemba. Alise katika masoko yote kuna viongozi waliochaguliwa kwa ajili ya kusimamia wafanyabiashara na kuwatatulia changamoto zao mbali mbali za kimazingira na kinidhamu, hivyo ni vizuri kuwatumia ili kupata msaada wa changamoto hizo wanapokua katika shughuli zao za kibiashara. "Masoko yote kuna viongozi waliochaguliwa kwa ajili ya kusimamia wafanyabiashara na kuwatatulia changamoto zao mbali mbali za kimazingira na kinidhamu, hivyo tunawashauri wanawake kuwatumia kuripoti matukio ya udhalilishaji yanapotokezea, ili kupata m...