HAJI
NASSOR, PEMBA:
JUMUIYA
kwa ajili ya watu wenye ulamavu wa akili Zanzibar ‘ZAPPD’ tawi la Pemba,
imeziomba mamlaka husika zinazotoa taaluma ya kujikinga na ugonjwa wa kifua
kikuu ‘TB’ kuhamia vijijini, ili kundi la watu wa aina hiyo, watambue njia za
kujikinga na ugonjwa huo.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Jumuiya hiyo, Khalfan Amour
Mohamed, wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, juu ya kundi
la watu wa aina hiyo wanavyoweza kufikiwa na taaluma.
Alisema vijana kama hao, ambao wapo mjini wamekuwa wakifaidika kwa
kiasi kikubwa na taaluma ya kujikinga na TB, ingawa ukosefu wa taaluma kwa
upana, hukosekana kwa wale waliyoko nje ya mji.
Mratibu huyo alieleza kuwa, kwa waliopo maeneo ya mjini, wamekuwa
wakipata mabango, vipeperushi, matangaazo mbali mbali na hata ukaribu wa vyombo
vya habari, ingawa kwa waliyoko vijijini kuna ufinyu wa taalamu hiyo.
Alieleza kuwa, ni vyema kikosi kazi kinachopambana na kusambaa kwa bekteria
wa TB, sasa kupeleka kwa nguvu elimu hiyo vijijini, ambapo watu wenye ulemavu
watafikiwa.
“Ni kweli Serikali kupitia wizara ya Afya, imekuwa mstari wa mbele
kuhakisha wanatoa elimu ya kujikinga na TB, lakini nguvu sasa ielekezwe
vijijini,’’alieleza.
Katika hatua nyingine Mratibu huyo wa Jumuiya kwa ajili ya watu wenye
ulemavu wa akili kisiwani Pemba, Khalfan Amour Mohamed, aliwataka wazazi na
walezi wa watoto hao, kuwa karibu mno na vyombo vya habari, ili kusikiliza njia
za kujikinga na ugonjwa huo.
Kwa upande wake, Mtaribu wa Idara ya watu wenye ulemavu kisiwani Pemba,
Mashavu Juma Mabrouk, alisema kwa vile ni vigumu kuwakusanya makundi ya watu
kuwapa elimu, njia pekee ni kusikiliza vyombo vya habari.
Alisema, tayari Idara hiyo, imeshandaa vipindi vya redio na tv kwa
ajili ya makundi mbali mbali ya watu wenye ulemavu, ili kujipatia elimu ya
kujikinga na TB.
Alifahamisha kuwa, kimsingi kila mazazi na mlezi anawajibu wa kutumia
dakika walau 20 kwa siku kumuelimisha mtoto wake, juu ya mambo mbali yakiwemo
haya yaliyoikumba dunia kwa sasa.
Katika hatua nyingine Mratibu huyo, aliwataka wale viongozi wa matawi
ya taasisi za watu wenye ulemavu wasisite kuwapa taaluma hiyo, pale
wanapokutana hata Ofisini mwao.
Nae Mratibu wa Jumuiya ya watu wasioona ‘ZANAB’ Pemba, Suleiman
Mansour, alisema bado haja ya wao kukusanywa japo wachache kupewa taaluma hiyo
ipo.
Afisa Mdhamini wizara ya Afya
Pemba, Khamis Bilali Ali, aliwataka viongozi wa matawi, kuwakusanya wanachama
wao, na kisha wizara itawapelekea wataalamu wa ugonjwa wa TB.
Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, amesema kundi la
watu wenye ulemavu lina, lina haki zote kama ilivyo kundi la watu wengine.
‘’Kama ni kweli kundi la watu wenye ulemavu wa akili linaomba kupewa
elimu, hili sio jambo la kucheleweshwa, ni vyema wizara na wataalamu wake
wajipange,’’alieleza.
Mkataba wa kimataifa wa haki za watu wenye ulamavu, Ibara ya 27
imezitaka nchi zilizoridhia mkataba huu, Tanzania ikiwemo zitambue haki za
kundi hilo kufanya kazi kwa misingi ya usawa kama wengine wasio na ulemavu, ili
waweze kumudu maisha yao.
Sheria ya
watu wenye ulemavu nambri 9 ya mwaka 2006 kifungu cha 11 (i) kimesiistiza kuwa
‘mtu
mwenye ulemavu ana haki ya kupatiwa huduma za afya na kuchukuliwa hatua za
kumkinga na jaambo linaloweza kumdhuru’.
Mkataba wa
kimataifa wa haki za watu wemue ulemavu Ibara ya 25, umezitaka nchi
zilizoridhia mkataba huo, kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapewa huduma bora
za matibabu bila ya ubaguzi.
MWISHO.
Comments
Post a Comment