NA HAJI NASSOR, PEMBA
MSHTAKIWA Khamis Abdalla Khamis ‘kirere’ wa Kangani wilaya ya Mkoani, aliyetiwa
hatiani kwa kosa la utawiti, kabla ya kusomewa hukumu ya miaka 19 ya chuo cha
mafunzo, ameiomba mahakama ya mkoa Chake chake, kwanza imchunguze akili zake.
Hayo
aliyadai wakati alipopewa nafasi ya kujitetea kabla ya mahakama hiyo ya maalum
ya makosa ya udhalilishaji ya mkoa wa kusini Pemba, chini ya Hakimu Muumini Ali
Juma, kumsomea hukumu yake.
Mshitakiwa
huyo alidai kuwa, anaomba kuchunguuzwa afya yake ya akili, sambamba na kuomba
kupunguziwa adhabu, kutokana na umri wake kuwa mdogo.
Aidha alidai
kutokana na kuhitajika kwake kwenye nguvu kazi ya taifa, aliomba ahuweni
mahakamani hapo, kufungwa kifungo cha nje, na adhabu yake iwe ni kufanya usafi.
‘’Mheshimiwa
Hakimu naiomba mahakama yako tukufu, kwanza inichunguuze akili, lakini pia
inipunguzie adhabu na kunipa kifungo cha nje, maana umri wangu bado
mdogo,’’alidai mshitakiwa huyo.
Hata hivyo
Hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma, alizingatia maombi ya mtuhumiwa huyo,
na kuamua kumpeleka chuo cha mafunzo kwa miaka mitano ‘5’ kwa kosa la kutorosha
na miaka 14 kwa kosa la kulawiti.
Alisema
kuwa, adhabu hizo zitumike tofauti, lakini pia pamoja na adhabu hiyo
mshitakiwa, ametakiwa kumlipa muathirika fidia ya shilingi milioni 2.
Hakimu huyo
alisema, adhabu aliyompa mshitakiwa hiyo ni ya kiwango cha chini, kutokana na
aina ya makosa yake, na hasa kwa mujibu wa sheria nambari 7 ya mwaka 2018,
sheria ya Mwendo wa makossa ya Jinai ya Zanzibar.
Kabla ya
kutolewa hukumu hiyo, Hakimu Muumini alisema ushahidi uliotolewa na mashahidi
mahakamani hapo, haukuacha chembe cha shaka, na ulikidhi vigezo vyote.
Alisema
upande wa mastaka, ulithibitisha mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri wa mtoto,
utoroshaji wake pamoja na tendo la kuingiliwa.
‘’Mtu pekee
anayeweza kuthibitisha ama kukataa kuingiliwa kwake, ni muhanga, na kwa mujibu
mtoto huyo wa miaka 10, alivyotoa ushahidi wakati akiongozwa na wakili wa
serikali, alithibitisha,’’alisema Hakimu Muumini.
Kabla
ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa serikali Ali Amour Makame, alisema
matendo hayo yamekua yakiathiri ndani ya jamii, hivyo ni vyema ikatolewa kwa
adhabu kali.
Alisema,
tayari jamii ilishafanya wajibu wake wa kuripoti kwenye vyombo vya sheria na
kisha navyo kuchukua hatau za kuifikisha kesi hiyo, mahakamani hapo.
‘’Kazi iliyobakia
sasa ni mahakama kutoa hukumu, maana kila pande imeshatekeleza wajibu wake,
kama taratibu na sheria zinavyoelekeza,’’alisema Wakili huyo.
Ilifahamika mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa
Khamis Abdalla Khamis ‘kirere’ miaka
20 wa Kangani wilaya ya Mkoani Pemba, alimtorosha na kisha kumlawiti mtoto wa
miaka 10.
Ambapo
alimtorosha kutoka sokoni Kangani na kumpeleka kwenye banda analolala, ambaapo
hilo ni kosa kinyume na kifungu cha 113 (1) (b) cha sheria ya Adhabu sheria
namba 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Huku kosa la
pili alilotiwa hatiani ni la utawiti, wa mtoto huyo ambalo ni kinyume na
kifungu cha 115 (1) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya
Zanzibar.
MWISHO.
Comments
Post a Comment