NA AMINA AHMED,
PEMBA:::
UNAPOZUNGUMZIA nafasi ya mkuu wa mkoa
mwanamke kwa Pemba, kamwe huwezi kuliacha jina la Salama Mbarouk Khatibu.
Salama hakumbukwi tu kwa nafasi hiyo, kwa wale wanaofuatilia
historia yake, kwanza alianzia nafasi ya kuhudumu ukuu wa wilaya za Chake chake
na Micheweni kwa nyakati tofauti.
Wapo wanaokumbuka ngarambe zake na jitihada zake za uongozi,
wakati ule wa awamu wa saba, alipokuwa mkuu wa wilaya ya Chake chake kabla ya
kuhamishiwa wilaya ya Micheweni.
Kiongozi huyu mwanamke anachukuwa mfano wa mwanamke
Hajar na Ibrahim, ambae nae bila ya kujali changamoto na maneno ya kukatishwa
tamaa, aliutumika umma.
Hajar, ambae alikuwa mwanamke jasiri,
mwenye nia nzuri, aliyeihama nchi yake, ili aende akaishi kando ya nyumba ya
Mungu katika ardhi, kame isiyo na maji wala manyasi ili amwabudu Muumba.
HUYU
HAPA MKUU WA MKOA KASKAZINI PEMBA
Salama Mbaroku Khatib, nae ni kama mfano huo,
ndivyopale anapoamuwa kutekeleza majukumu yake ya uongozi ndani ya mkoa wa Kaskazini
Pemba kwa vile hajali muda, juwa wala mvua.
Kwake salama anasema, anachotamani jua linapozama ni
kukamilisha majukumu yake, na hasa ya kuwahudumia wananchi kama dhamira baada
ya kula kiapo kushika nafasi hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa Makala hii, anasema ndoto zake ni
kuona Mkoa huo wananchi wake wanaishi bila ya shida za dhahiri, mfano huduma za
kijamii.
‘’Mimi nimekula kiapo kuhakikisha wannachi wa wilaya za
Micheweni na Wete wanaishi kwa utulivu na huduma za kijamii za lazima
ninawafuata wao,’’anasema Salama.
Salama Mbarouk Khatib ni mwanamke pekee aliteuliwa kuongoza mkoa
wa kaskazini kwa mara ya kwa za kati ya wakuu wa mikoa 14 waliopita kabla
yake.
Ndio pekee ambae rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, aliyekambidhi kijiti cha uongozi
kwa nafasi hiy, kati ya wakuu wa mikoa watano waliopo Unguja na Pemba.
Anasema alichokifanya Dk. Mwinyi ni utekelezaji kwa vitendo
vile vifungu vya kila mmoja ana haki sawa na mwenzake, vilivyomo kwenye Katiba ya
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania yam waka 1977 na ile ya Zanzibar yam waka 1984.
Ambapo katiba hizo, kama ukizichungulia kwa kina, zimeweka
haki sawa kati ya mwanamke na mwanamme, (50 kwa 50) iwe kwenye uongozi au haki
nyingine za kikatiba.
"Kwanza nimshukuru sana Dk. Hussein Ali
Mwinyi kwa kuniamini na kunikabidhi wananchi wa mkoa wa kaskazini Pemba, 272,
091, wakiwa wanaume 131, 484 na wanawake 140, 607 (sensa 2022),’’anasema
Salama.
Kwake nafasi hiyo, anaona umempandisha ndege ya kufungua
ukurasa mwengine katika kitabu chake cha historia, ambapo anaona kila
anapokutana na changamoto, huzigeuza kuwa fursa.
Kumbe RC Salama ni mkuu wa mkoa wa 15 kwa mujibu wa uteuzi, ingawa
kati ya hao, wote walikuwa ni wanaume, jambo ambalo linaonesha mabadiliko na
wanawake kupanda chati.
WAPI ALIANZIA SALAMA?
Kwake anasema, hakuwa mjuzi wala mtaalamu wa
kuongoza nafasi yoyote, lakini alichofundishwa wakati wa kusimamia majukumu yake,
ni kujiamini.
‘’Siri kubwa niwaambie wanawake wenzangu kikubwa ni kujiamini
na tunapopata nafasi inatubidi tuitendee haki ipasavyo, ndivyo wanavyofanya
hata hao wanaume”, anasema.
Baada ya kutoka wizara ya wanawake na watoto, na
kupata uteuzi wake wa kwanza kuwa mkuu wa wilaya ya Chake chake, anasema
aliiingia na hofu ya kawaida kama mwanadamu, ingawa alipaya ushirikiano wa
kutosha.
Anasema, kama mgagaa na upwa hali ugali mkavu, basi yeye alikuwa
akigagaa na watumishi wenzake na kusikiliza ushauri, na kufanya uamuzi wa
pamoja wakati huo.
Mashaallah, Allah amjaalie mafanikio mema,
wepesi na utayari wake katika utendaji kazi kabla ya kuteuliwa kuongoza
nafasi hiyo kumechangia kufika hapa alipo sasa.
Anasema ingawa alianza
kupikwa na kupikika, wakati akiwa Ofisa
Mipango, wizara ya wanawake na watoto Pemba, hivyo hata alipoteuliw akushika
nafasi hiyo, ilikuwa rahisi kiasi.
" Nilikuwa najiamini na naitendea haki kazi
niliopewa sekta niliyopangiwa sikuwa na hofu wala woga, pakutolewa uamuzi kama kiongozi
nilikuwa natoa, pakushauri nilikuwa nashauri pia,’’anakumbuka.
Anasema miongozo, sera
na sheria ndio zinazomlinda kila mtumishi, ingawa suala la kujiamini na kuacha
hofu katika kazi ndio mwarubaini kwake, unaopmpa uhakika wa kuwatumikia
wananchi.
Jukumu la uongozi alilonalo huku akiwa ni mke,
lakini pia mama wa familia, haliathiri utendaji wake kazi, hivyo ni kusema
maisha ya uongozi hayaathiri familia yake bali yanaongeza
heshima na mashirikiano.
Anasema
kila kitu ni kujipanga na kukipangilia, lakini mimi kwa nafasi zote
nilizowahikushika hadi hii ya Mkuu wa Mkoa, sioni dhiki na kuihudumia familia
yake.
Kwake
haamini kuwa, mwanamke akipewa nafasi inaweza kumshinda kwa sababu ya familia,
bali anachokiona ni ikiwa atakosa kujipanga na kujipangilia inaweza kuwa
changamoto.
" Mimi ni mama ambae nina mume na nina
watoto, serikali inanitegemea lakini niseme kwamba kikubwa ni kujifahamu tu , kuwa
wewe ni kiongozi na nyumbani wewe ni mama ambae unastahiki kufanya majukumu
yako,’’anasema RC Salama.
Anaeleza kuwa wananchi wameamka sasa hivi
hawaangalii jinsia wanaangalia utendaji kazi aliwaasa wanawake wenzake
kutuogopa fursa wasizichezee wafanyekazi kadri ya uwezo wao na suala hilo
linaweza kuwapa fursa kusonga mbele.
Anasema licha ya watu wachache kumtia midomoni, katika
utowaji wa maamuzi ya kiutendaji, katika uongozi wake hakulipokea suala hilo kama ni kikwazo kwa
upande wake.
" Kuna baadhi ya watu wanaotaka wakuendeshe
vile wanavyotaka wao kwa maslahi yao binafsi, jambo ambalo kwangu silipi
kipaumbele naamua kwa kufuata sheria,’’anafafanua.
Kwake anaona ukifanyakazi kwa dhati, hasa ndio
changamoto na kasoro zinapoonekana na ukikosa kasoro wewe sio binaadamu au
ukizikataa.
kwahiyo nakubali
kushauriwa lakini zaidi na angalia ule ushauri ninaopewa je
hautokweda kinyume na sheria za serikali, jee
una maslahi ya taifa, hautoathiri serikali ndipo
naufanyia kazi kikubwa ninachoangalia ni hicho", alisema.
ANAOFANYA NAO KAZI
RC SALAMA
Mgeni Khatib Yahya mkuu wa wilaya ya Micheweni,
anasema kuwa kiongozi huyo ndie ambae alikuwa anajifunza mambo mengi
kutoka kwakwe.
Anasema alipokuwa Mkuu wa wilaya ya Wete kabla ya kuhamishiwa
Micheweni, alivuna mambo mengina na mazuri na hasa suala la kujiamini.
Kwake alikuwa ndio kioo, katika kufanikisha majukumu yake ya kila
siku, na hatomsahau tena maana, alimfundishi wa vitendo aina ya uongozi na
kuongoza.
"Najifunza siku
hadi siku mambo mazuri kutoka kwa mkuu wa Mkoa Salama Mbarouk Khatib, ananishauri
ananipa maelekezo kama msaidizi wake na natekeleza majukumu yangu vyema
kwa kufuata nyao zake zaidi za uthubutu,’’anasema.
Mkuu wa wilaya ya Wete Dk. Hamad Omar Bakar, wanaotaka kuona
kuwa mwanamke anaweza kuongoza katika mazingira yoyote, wafike mkoa wa
kaskazini Pemba.
Kwake mkuu huyo wa Mkoa anamuona mtu wa tofauti, ambae ana
nia thabiti ya kweli katika kuitumikia nafasi hiyo na wananchi, bila ya kujali
mvua, usiku wala jua kali.
‘’Sisi wakati mwengine tunafikiria kwa mvua inavyonyesha
jambo fulani, mkuu wa mkoa atalighairisha, lakini mara unamuona huyo amefika
sehemu,’’anasifia mkuu wa wilaya Wete.
WANANCHI
Aziza Makame Abass Mkaazi wa Limbani
wilaya ya Wete, anasema kuwa jitihada inazofanywa na mku huyo wa mkoa, katika kuleta
maendeleo, zinaonekana.
Anasema maeneo mengi aliyarithi yakiwa na changamoto za ukosefu
wa huduma za kijamii kwa uhakika, ingawa kwa sasa kila eneo hali inridhisha.
"Kwanza binafsi nampenda anavyofanya kazi nikisikiliza
radio jamii nisipomsikia jioni basi asubuhi nitamsikia anazungumzia jambo
lolote tunajuwa hasa wa kama tuna kiongozi sio wengine ambapo hata kuwasikia,
ni shida,’’anasema.
Nassra Salum Mohamed ambae ni diwani wadi wa
Kiuyu, anasema Mkuu wa mkoa wao, ni anakipaji cha uongozi, kuzungumza na hata
kuamua jambo, na ni vyema wanawake wengine wakajifunza kwakwe.
‘’Hata sisi madiwani tukisikia tuna kikao na mkuu wa mkoa,
inabidi kama unachangamoto unataka kuisilishwa kwa, uifanyia uchambuzi wa kina,
vyenginevyo itakurudia mwenyewe,’’anasema.
Salim Ali wa Wete, anasema anazipongeza juhudi
za kupata viogozi wanawake zilizochukuliwa na mashirika na asasi mbali mbali, zilizopigania
nafasi ya uongozi kwa mwanamke.
‘’Nasikia kuna chama Chama Cha waandishi wa Habari
wanawake Tanzania ‘TAMWA’ Zanzibar na wengine wamekuwa wakiwawezesha wanawake,
nawaambia kwa mkoa wa kaskazini Pemba wamefanikiwa,’’anasema.
WANAHARAKATI
Mratibu wa TAMWA Pemba Fat-hya Mussa Said, anasema
wanaijivunia mno, uongozi wa Mkuu huyo wa Mkoa hasa kwa vile alikuwa kwenye
kapu la wanaharakati.
‘’Salama alikuwa anashikia bango kuwa, wanawake wanapopata
nafasi za uongozi wasizibeze, na bahati nzuri imemuangukia yeye, sasa tunaona
macheche yake kwenye uongozi,’’anasema.
Aisha Himid Vuia, anasema alichokifanya Dk. Mwinyi cha kuwapa
nafasi nyingi wanawake, ni matokeo ya kelele za wanaharakati, ambapo hakuna
mwanamke kiongozi aliyezubaa.
Khalfa Amour Mohamed, anasema wamekuwa wakishirikiana na Mkuu
huyo wa mkoa katika shughuli kadhaa na hajawahi kukataa, maana anapenda
kushirikiana na makundi ya kijamii.
HALI HALISI YA WANAWAKE NA UONGOZI
Zanzibar kwa
sasa kasi ya wanawake kuingia katika uongozi imeongezeka
ukilinganisha na miaka iliyopita ambapo TAMWA viongozi wanawake katika
Baraza la wawakilishi ni asilimia 36 ambayo ni sawa na wanawake 28
kati ya wawakilishi 84 waliopata nafasi hiyo.
Ni wanawake 22 pekee ambao ni viongozi
wakuu kati ya nchi na mataifa ya nchi 123 kwa idadi
hiyo bado jitihada zinahitajika katika kuona mwanamke anapata fursa sawa katika
vyombo vya maamuzi.
Mkuu huyo wa mkoa wa kaskazini Pemba, Salama Mbarok Khatib,
aliteuliwa kushika nafasi hiyo Disemba 1, mwaka 2020 na kula kipambo Disemba 3,
mwaka huo huo pamoja na wakuu wa mikoa wenzake.
MWISHO.
Comments
Post a Comment