NA SAID BARAGHASHI, PEMBA
WANANCHI kisiwani Pemba, wametakiwa
kushiriki kikamilifu kwenye shamrashamra za kueleka maadhimisho ya siku 16 za
kupinga ukatili na udhalilishaji, kwa wanawake na mtoto wa kike, zinazotarajiwa
kuanza mwishoni mwa mwezi huu.
Kauli hiyo
imetolewa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya maadhimisho huyo kisiwani humo,
Mchanga Haroub Shehe, wakati
wakiwasilisha mapendekezo ya ratiba ya shamra shamra ya maadhimisho hayo, kwa mkuu wa wilaya ya Mkoani.
Alisema, shughuli hiyo kwa kiasi kikubwa,
wanawategemea wananchi wa wilaya zote nne za Pemba, hivyo ni vyema wakakikisha
wanashirikiano nao katika kufanikisha sherehe hizo.
Alieleza
kuwa, moja ya sababu ya kuwafikia wakuu wa mikoa na wilaya, kwanza ni kupata
baraka, ushauri, maelekezo na namna ya kuwapata wananchi kushirikiana kuwanzia
mwanzo hadi mwisho.
‘’Sisi
tutawahamasisha wananchi kushiriki, lakini na wakuu wa wilaya ambao ndio wenye
masheha na wananchi, mtusaidie ili kufanikisha jambo hilo,’’alisema.
Aidha Kaimu Mwenyekiti
huyo, alimueleza mkuu huyo wa wilaya ya Mkoani kuwa, wanatarajia kuwa na
shughuli mbali mbalii, ikiwa ni pamoja na kongangamo kubwa wilayani humo.
Shughuli
nyingine ni kufanya mikutano ya jamii, katika shehia mbali mbali kwa lengo la
kufikisha ujumbe juu ya kuondoa
ukatili na udhalilishaji, kwa wanawake na mtoto.
Kwa upande
wake Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, alisema amewapokea na
kuwakaribisha kuenelea na shughuli zao hizo, za kuelimisha jamii juu ya athari
ya matendo hayo ya ukatili na udhalilishaji.
Alisema,
kamati hiyo anaiamini, na kwamba atawaskumbusha masheha kwa shehia
zitakazobahatika, ili kuona washiriki wanaotakiwa wanapatikana katika shughuli
mbali mbali.
‘’Mlipogusa
suala la kutokomeza matendo hayo, nami ni mdau mwenzenu, sasa kwanza karibuni
wilaya ya Mkoani, lakini naahidi kushirikiana nanyi katika kila
hatua,’’alifafanua.
Aidha
amesema ofisi yake ni moja ya wafuatiliaji wa
matokeo hayo yanapotokea kwenye jamii na wameona kuengezeka zaidi, katika baadhi ya shehia.
‘’Zipo
shehia zimeakuwa zikiripoti mara kwa matukio haya kama vile Mwambe, Kengeja, Kiwani
na hata shehia ya Mgagadu, ingawa sio takwimu ya kutisha,’’alieleza, Mkuu huyo
wa wilaya.
Mjumbe wa
Kamati hiyo Khalfan Amour Mohmed na mwenzake Hafidh Abdi Said, walipongeza
hatua ya mkuu wa wilaya, kuahidi kushirikiana na kamati yao.
Kamati hiyo
kwa ajili ya kufanikisha shamra shamra na kisha kilele cha maadhimisho ya siku
16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto, inaundwa na tasisi kadhaa
ikiwa ni pamoja na TAMWA, ZLSC, PEGAO, TUJIPE, CHAPO, KUKHAWA, ZAPDD, PAFIC na
tayari wajumbe hao wameshakutana na wakuu wa mikoa, wilaya na baadhi ya mafisa
wadhamini.
mwisho
Comments
Post a Comment