NA HAJI NASSOR, PEMBA::
WANANCHI kisiwani Pemba, wameshauriwa
kuvitumia vituo vya afya vilivyo karibu yao, kwa ajili ya kuwapeleka ndugu na
jamaa zao, kufanyiwa uchunguuzi wa afya ya akili, ili wagundulike mapema ikiwa
ni watu wenye ulemavu wa akili ama laa.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Chake Chake, Mratibu wa Huduma za Afya ya Akili
Pemba Salim Khamis Ali, alisema wapo baadhi ya wananchi, huwapeleka ndugu na
jamaa zao kwa waganga wa kienyeji.
Alisema wapo
wagonjwa huwapokea wakiwa wameshacheleweshwa mno, kwa kule ndugu na jamaa zao,
wanapowagundua kuwa wanaumwa, hukimbilia kwa waganga wa kienyeji, badala ya
hospitali na vituo vya afya.
Mratibu huyo
alisema, Wizara ya Afya Zanzibar katika kulijali kundi la watu wenye ugonjwa wa
akili na wale walemavu wa akili, imeweka huduma zao kwenye vituo vyote vya afya
hadi vya vijijini.
Alisema hilo
limewekwa, ili sasa kuwapunguzia masafa wananchi, wanaotaka huduma za afya ya
akili, ambapo hapo zamani, walilazimika kwenda hospitali za wilaya pekee.
“Ilikuwa
huduma hizi za afya ya akili, zinapatikana hospitali za wilaya za Wete, Mkoani
na Chake Chake lakini sasa hata kwenye hospitai za coteji na vituo vyote vya
afya, huduma hizi zinapatikana,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine, Mratibu huyo wa Huduma za Afya ya Akili Pemba Salim Khamis Ali,
alisema wagonjwa hao wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku kisiwani Pemba.
Alisema,
hilo husababishwa na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na masongo wa mawazo, au
wakati mwengine mtu kukumbwa na magonjwa mengine kama vile Ukimwi.
“Hata
magonjwa kama vile Ukimwi au mtu kuondokewa na mpendwa wake ghafla, haya yote
yanaweza kusababisha kukumbwa na ugonjwa wa akili,’’alifafanua.
Baadhi ya
wananchi kisiwani Pemba, wamesema bado jitihada za makusudi, zinahitajika ili
kulilinda kundi la watu wenye ugonjwa wa akili na hata wale wenye ulemavu wa
akili.
Mratibu wa
Jumuia kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa akili Zanzibar ZAPPD, tawi la Pemba,
Khalfan Amour Mohamed, alisema bado jamii imekuwa ikiwadharau watu wenye ulemvu
wa akili.
Alisema,
pamoja na mchango mkubwa walionao wananchi wenye ulemavu wa akili, lakini bado
jamii haijaona umuhimu wa kuwashirikisha katika shughuli za kila siku.
‘’Wakati
mwengine watu wenye ulemavu wa akili huwekwa kundi moja na wale wagonja wa
akili, ingawa kitaalamu hao ni makundi mawili tofauti,’’alisema.
Mfanyabiashara
wa nguo katika mji wa Chake chake ambae anaulemvu wa akili Maulid Ali Kassim,
alisema changamoto kubwa anayoiona kwa jamii ni kutowakubali wao.
‘’Bado jamii
haijatuamini kuwa sisi ni sehemu yao, na ndio maana kila tunachokifanya sisi
tunabezwa na kuonekana hatuna mchango kwa taifa,’’alisema.
Asha Said
Idd ‘dada a’ mwenye ulemavu wa akili mkaazi wa Mkoani Pemba, amesema kama
sheria hazijatekelezwa ilivyo, kundi hilo linaweza kuendelea kudai haki zao
kila siku.
Waziri
katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza Zanzibar Harusi Said Suleiman, alisema wamo
kwenye mchakato wa kuifanyia marekebisho sheria ya watu wenye ulemavu nambari 9
ya mwaka 2006.
Mwisho
Comments
Post a Comment