NA
MOZA SHAABAN, PEMBA
MADIWANI
wakuchaguliwa na waratibu wanawake na watoto kutoka wilaya nne za Pemba wametakiwa kuwajibika ipasavyo katika
utekelezaji majukumu yao ya msingi ya kiuongozi, ili kujenga imani kwa jamii
juu ya uwezo alionao mwanamke katika kuongoza na kuleta maendeleo.
Wito
huo umetolewa na Afisa Progamu wa mradi wa kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika
masuala ya uongozi (SWIL) unaotekelezwa na TAMWA-Zanzibar Sabrina Ali Mwatanga
wakati wa mafunzo kwa madiwani na
waratibu wanawake na watoto kutoka wilaya nne za Pemba, yaliolenga kuwajengea
uwezo juu ya namna ya kuwajibika ipasavyo katika uongozi wao, yaliofanyika
katika ukumbi wa mikutano TAMWA Mkanjuni Chake chake Pemba.
Alieleza
mafunzo hayo ni mwendelezo wa hamasa na kuwajengea uwezo madiwani na waratibu
hao juu namna bora ya kutekeleza majukumu yao ya kiongozi, ili jamii ione
ufanyaji kazi wao kivitendo.
Afisa
huyo alisema TAMWA imekua ikifanya
juhudi kubwa katika kuwajengea uwezo wanawake mbali mbali katika kushiriki
kwenye vyombo vya maamuzi kupitia uongozi na demokrasia, ila bado jamii haina
imani kubwa na viongozi hao hivyo kuwajibika kwao kutaionyesha jamii nguvu
walionayo wanawake katika kuleta maendeleo.
"TAMWA imekua ikifanya juhudi kubwa katika kuwajengea uwezo wanawake katika kushiriki kwenye vyombo vya maamuzi kupitia uongozi na demokrasia, ila bado jamii haina imani kubwa na viongozi wanawake, basi kuwajibika kwenu kutaionyesha jamii nguvu ya wanawake katika kuleta maendeleo", alisema.
Aliongeza kua uwajibikaji mzuri ni msingi wa uaminifu kwa wanawake katika kugombea nafasi mbali mbali za uongozi, ambapo kitakua kipimo muhimu kwa jamii katika kufanya maamuzi ifikapo uchaguzi mkuu 2030, hivyo TAMWA-ZANZIBAR ikaamua kuwapatia mafunzo hayo ili kuwandaa kwa uchaguzi mkuu ujao.
"
Jamii pia huangalia uwajibikaji wa mtu anapopata nafasi, ambapo huchukua hilo
kama ni kigezo cha kufanya maamuzi katika uchaguzi, ndio TAMWA tukaamua kuwapa
mafunzo haya mukayatumie kama ni maandalizi ya uchaguzi wa 2030", alisema.
Nae
Kaimu Mratibu wa TAMWA Ofisi ya Pemba Amina Ahmed Mohammed alisema, mafunzo
hayo yanalenga kutoa hamasa kwa madiwani na waratibu wanawake na watoto ili
kuongeza ushiriki wao katika ngazi za maamuzi, ili sauti za wanawake ziweze
kusikika na kua tumaini kwa wanawake na watoto, ambapo zinaweza kusaidia
kuleta mabadiliko ya upatikanaji wa haki mbali mbali kwa jamii.
Alisema
wanawake wanamchango mkubwa katika maendeleo, siasa utawala na utamaduni iwapo
watawajibika ipasavyo katika kuzitumikia jamii zao kwa kuzipatia maendeleo.
Akiwasilisha
mada kuhusu ushiriki wa wanawake katika
kugombea nafasi mbali mbali za uongozi mkufunzi wa mafunzo hayo Fat-hia Mussa
Said, aliwataka wanawake kua na uthubutu katika kugombea nafasi hizo.
Alisema
katika miongo ya hivi karibuni dunia imepiga hatua kubwa kuongeza ushiriki wa
wanawake katika uongozi na siasa, ambapo nchi nyingi zimeanzisha sera, sheria
na mikakati ya kuhakikisha wanawake wanapata fursa sawa na wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi.
Alisisitiza
pamoja na mafanikio hayo wanawake bado wapo chini ya uwakilishi wa wanaume
katika mabunge, serikali za mitaa vyama vya siasa na taasisi mbali mbali za
maamuzi ikilinganishwa na wanaume, hivyo alisisitiza wanawake kuchukua juhudi
za makusudi kuongeza ushiriki wao.
Nao
washiriki wa mafunzo hayo waliipongeza TAMWA-Zanzibar kwa kuwapatia mafunzo hayo na kuona umuhimu wa
kuwaongezea maarifa ya uwajibikaji wanawake viongozi jambo litakalo saidia kutimiza majukumu yao
ipasavyo pamoja na kwashajihisha wanawake wengine katika kujitokeza kugombea
nafasi mbali mbali za uongozi katika uchaguzi wa 2030.
Hata
hivyo walieleza bado wanawake viongozi wanakabiliwa na changamoto mbali mbali
ikiwemo mfumo dume, kutojiamini na kutokukubalika kwa jamii, hivyo wameomba
wadau mbali mbali kuendeleza mapambano dhidi ya changamoto hizo, ili kuinua
ushiriki wao katika kugombea nafasi za uongozi.
TAMWA-
ZNZ kupitia mradi wa SWIL imekua ikishajihisha wanawake kushiriki
katika kugombea nafasi mbali mbali za uongozi, ili kupata uwakilishi wao katika
ngazi za maamuzi kwa lengo la kupaza sauti zao juu ya uvunjaji wa haki zao za
msingi na kukuza usawa wa kijinsia,
ambapo huonekana kuvunjwa mara kwa mara.
MWISHO.



Comments
Post a Comment