Skip to main content

CANADA YAKABIDHI VIFAA VYA SH/= MILION 270 VYA UCHUMI WA BULUU

 

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

SERIKALI ya Canada, imesema itaendelea kushirikiana na serikali za Tanzania, katika maeneo mbalimbali, ikiwemo kwenye uchumi wa buluu, ili walengwa wakuze pato lao na taifa.

Hayo yameleezwa leo Juni 23, 2026 na Balozi wa taifa hilo, nchini Tanzania Emily Burns, kwenye hafla ya ugawaji wa vitendea kazi kwa vikundi vya wajasiriamali, waliokeza kwenye bahari, na ufunguzi wa kituo cha mafunzo eneo la Chamanangwe wilaya ya Wete Pemba.

Alisema, ushirikiano huo, anaamini utawasaidia wajasriamali waliokeza kwenye eneo hilo, hasa wanawake na vijana, ambao kwa muda mrefu walikuwa hawakuhusishwa moja kwa moja.

Alieleza kuwa, kwa eneo la Zanzibar na baadhi ya mikoa ya Tanzania bara, ilivyozungurukwa na bahari, wakati umefika manufaa yake, yawanufaishe makundi yote.

‘’Serikali ya Canada, inaziahidi serikali zote mbili kwamba, ushirikiano huu kwenye sekta ya uchumi wa buluu, utakuwa endelevu pamoja na maeneo mingine,’’alifafanua.



Katika hatua nyingine, Balozi huyo wa Canada nchini Tanzania, aliwataka wajasiriamali hao, kuhakikisha vifaa hivyo ikiwemo boti maalum, wanavitumia, kwa lengo la kukuza pato lao.

Alisisitiza kuwa, serikali ya Canada imetumia gharama kubwa, ili kununa vifaa hivyo, kama sehemu ya kuziunga mkono seriali za Tanzania, hivyo lazima waelekeze nguvu zao huko.





‘’Vifaa hivi tulivyovikabidhi kwenu, ni heshima kubwa kwa viongozi wa Tanzania, ambao wamekuja na sera ya uchumi wa buluu, sasa mwelekeo uwenu uwe wa maana sana,’’alisisitiza.

Hata hivyo, alipongeza hatua za marais wa Tanzania, kwa kuzingatia kwa vitendo sera ya uchumi wa buluu, kwa wananchi wake.

Mapema Mkurugenzi wa Mradi wa Resea Andreanne Martel- Mi, alisema ni jambo la faraja, kuona serikali ya Canada imetekeleza kwa vitendo ahadi yake.









Alisema, amefarajika sana kuona kuwa, wameingia kwenye siku nyingine, yenye mwalekeo wa kuwasaidia vifaa vya kutendea kazi, wajasiriamali hao wingi, wakiwa wanawake.

‘’Kama inavyoeleweka kuwa, wanawake ndio kundi ambalo liliachwa nyuma kwenye sekta kadhaa, ikiwemo ya bahari, lakini kwa hili lililofanywa na wenzetu wa Canada, matunda yanakuja kwa haraka,’’alifafanua.

Aliongeza kuwa, mradi huo ambao unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya IUCN, WFTT na Ocean hub, ni kuona taasisi hizo zinatia nguvu, ili mradi utekelezeke.

Alieleza kuwa, mfano wa utoaji wa vifaa hivyo, wala sio shughuli ndogo, bali pia ni kutambua uwepo wa kundi hilo na umuhimu wake, katika kukuza pato lao na taifa.

‘’Kushirikiana kwetu na taasisi hizo, sio tu kwamba tuwe pamoja, bali ni kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuimarisha mnyororo kwa wanawake na vijana, kwenye eneo la uchumi wa buluu,’’alifafanua.

Katika hatua nyingine, alisema vikundi hivyo kwa sasa vimekuwa kiuchumi, na kama vile kukabidhiwa kwa vifaa hivyo, vinakwenda kujitegemea.







 Mkuu wa wilaya ya Wete Abdalla Rashid Ali kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba, amewataka wajasiriamali waliokabidhiwa vifaa hivyo, kwanza kuvithamini na kisha kuhakikisha vinazaa matunda.

Alieleza kuwa, fedha nyingi zimetumika kununulia vifaa, hivyo sasa ni wajibu wao, kuona vitawasaidia wao na wingine hapo baadae.

‘’Kwa hakika wenzetu wa jumuiya ya Inclusion wamefanya jambo jema, kuwapata wafadhili wa serikali ya Canada na sasa kuwagawia vifaa hivi,’’alifafanua.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania ‘WFTT’ Rose Marandu, aliiongeza serikali ya Canada, kwa kukubali ununuzi wa vifaa hivyo.





Alieleza kuwa, serikali ya Canada, imekuwa mdau mkuu wa maendeleo katika sekta mbalimbali, ikiwemo ya uchumi wa buluu.  

Nae Ofisa Mdhamini wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Pemba Dk. Salim Hamza, alisema kwa miaka 10 iliyopita, Zanzibar hakukua na sera na uchumi wa buluu, jambo lililowatenganisha wanawake.

Alisema, sasa serikali imeshatekeleza kwa vitendo hilo na ndio maana, rasimali za bahari zinawanufaisha wanawake na wanaume.

‘’Niwapongeze sana Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania na yule wa Zanzibar, kwa kuzitafsiri kwa vitendo ahadi zao, kwa walioekeza kwenye sekta ya baharini,’’alisema.

Wakisoma risala yao, iliyosomwa na Saada Juma Haji kutoka kikundi cha Tusijisahau cha Madenjani, alisema, sasa wanakwenda kuuwaga umaskini.

Alieleza kuwa, hilo linakuja baada ya vifaa ambavyo waliviomba, vimekujana kama walivyotaka, na kupata ari na mori ya kuendelea na kazi zao.



Alisema, wamekuwa wakijishughulisha na ukulima wa majongoo bahari, mwani, usarifu wa dagaa na uhifadhi wa mazingira ya bahari.   

Vifaa vilivyokabidhiwa kwa vikundi hivyo 12 ni boti maalum na mashine zake, viatu, meza za ofisi, mabero, viatu maalum, lapo top, mezani.

Vyingine ni makoti maalum ya kuokolea maisha, waya za kuanikia dagaa na mwani, vioo vya kuzamia, majembe pamoja na uzinduzi wa kituo cha mafunzo cha wajasiriamali, kwa mujibu wa kazi zao hizo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 270.

Vikundi vilivyokabidhiwa vifaa hivyo ni pamoja na Jiongezee, Jitihada, Mtu ni yupi, Tusijisahau, Mwendaji si mkaaji, Tushikamane, Hapa kazi tu kwa upande wa Pemba na Mafanikio group, Tageti group, Magarawani na Marikacha kwa upande wa mkoa wa Tanga.











Mradi wa Resea ambao ulikuwani wa miaka mitatu, kutoka mwaka 2023 hadi 2025, ingawa umeongewa muda hadi mwishoni mwa mwaka huu, unafadhiliwa na serikali ya Canada.

Mradi huo unatekelezwa na mashirika matatu, likiwemo la Mission inclusion, IUCN na WFTT, unafanyika mataifa ya Kenya, Moazambique, Madascar, Comoros na Tanzania, ambapo mradi huo unao maeneo kadhaa, ikiwemo la uchumi wa buluu.

  Mwisho  

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...