Skip to main content

WAANDISHI WA HABARI: 'CHINA ITOWE MISAADA MIKUBWA KWA AFRIKA IJITEGEMEE'

 

 NA HAJI NASSOR, ALIPOKUWA BEIJING

WAANDISHI wa habari wa mataifa ya Afrika, wameiomba serikali ya China, kuyapa mataifa yao miradi endelevu mikubwa ya maendeleo, ili baadae yaweze kujiendesha, badala ya kutegemea misaada kila baada ya muda.

Wakizungumza kwenye ziara ya kuvitembelea vituo vya Tehema, star times vilivyopo Beijing nchini China, walisema urafiki na uhusiano wa China na mataifa ya Afrika, unaweza kuchapuzwa na miradi mikubwa.

Mwandishi wa habari kutoka Gambia Arret Jatta, alisema kwa muda mrefu mataifa hayo, yamekuwa yakipokea misaada kutoka kwa serikali ya China, ingawa baada ya miradi kumazilika, hurejea kwenye utegemezi.

Alieleza kuwa, China imekuwa ikitumia mamiliobi ya dola, kuyaunga mkono mataifa ya Afrika, ingawa huwa ni kwa kiasai kidogo, kwa mujibu wa mahitaji ya wakati uliopo.

‘’Wakati umefika sasa kwa taifa la China, kulielekea taifa moja moja la Afrika, na kulipa msaada mkubwa wa maendeleo, katika nyanja ama ya elimu, afya, miundombinu ili changamoto hiyo imalizike,’’alipendekeza.

Nae mwandishi Agren Mutambo kutoka Kenya, alisema ipo miradi mikubwa kama ya ujenzi wa miundombini, afya, maji safi na salama, kama China ikiyafanya kwa ukubwa wake katika mataifa yanayoendelea, inaweza kusaidia.

‘’Ijapokuwa China imekuwa ikitoa misaada mikubwa kwa mataifa ya Afrika, lakini napendekeza iongeze nguvu, maana bado baadhi ya mataifa shida ipo,’’alisema.

Kwa upande wake mwandishi Yakali Tariku kutoka Ethiopia, alisema changamoto kubwa ndani ya baadhi ya mataifa ya Afrika, ni kukosekana miradi mikubwa na endelevu, hivyo ni wakati umefika kwa China, kuongeza juhudi.

‘’Tunajua Rais wa sasa wa China Xi Jinping , amekuwa na uhusiano na urafiki kwa dhati kwa mataifa ya Afrika, likiwemo la Ethiopia, lakini sio vibaya kuongeza nguvu katika eneo la miradi mikubwa,’’alifafanua.



Waandishi wa habari Josphine Mabere wa Kenya na mwenzake Zuhura Juma wa Zanzibar, waliipongeza serikali ya China kwa misaada yao ya kibinaadamu, wakati wa janga la Covid19.

Mtaalamu wa sayansi ya jamii kutoka taasisi ya Magharibi mwa bara la Asia na Afrika, anayefania kazi zake nchini China Professa: He Wenping, alisema China imekuwa ikihakikisha kila muda, kupeleka misaada mikubwa kwa Afrika.

Akiwasilisha mada ya sera na utendaji kazi kwa China, juu ya maendeleo ya Afrika Dk. Yao Shuai, alisema misaada yenye thamani ya dola bilion 615.8 imeshapeleka mataifa ya Afrika, kati ya mwaka 1950 na mwaka 2018.



Aidha alisema, wapo madaktari zaidi ya 1,069 wamesambaazwa katika mataifa, na maeneo 76, barani Afrika wakitoa huduma za matibabu ya kibinaadamu.

‘’Na kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2020, China imeshajenga vituo vya michezo 45 na skuli 170 katika maeneo mbali mbali ya mataifa ya Afrika, ikiwa ni sehemu ya kuongeza uhusiano wake,’’alifafanua Dk. Yao.

Awali akifungua mafunzo ya siku 20 kwa waandishi wa habari wa mataifa ya Afrika, yanayozungumza lugha ya kiengereza, Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (CICG) Han Likiang, alisema mafunzo hayo, ni sehemu ya kuziwezesha nchi ukuaji uchumi wao.

Waandishi wa habari wa redio, tv, mitandao ya kijamii na magazeti wapo nchini China, wakiendelea na mafunzo na ziara, ni kutoka nchi za Gambia, Zambia, Kenya, Ethiopia, Tanzania Zanzibar na wenyeji China.

Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...

HABARI ZA HIVI PUNDE

 TAARIFA za hivi punde, zilizofikia ofisi ya Pemba Today, zinaeleza kuwa, Jeshi la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, linamshikilia askari mwenzao, kwa tuhuma za ubakaji ndani ya moja ya kituo cha Polisi kisiwani Pemba Muume wa mwanamke aliyedai kubakwa na Mwanamke mwenyewe, wamedai kutokea kwa tendo hilo, na huku Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, akithibitisha kupokea kwa lalamiko hilo.... Kwa taarifa zaidi ya tukio hili endelea kufuatilia mtandao huu, ambao kukuhabarisha ni fahari yetu...