NA ZUHURA JUMA SAID, PEMBA
MAKAMU wa Pili wa rais Zanzibar Hemed
Suleiman Abdulla, amewataka wakandarasi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya
Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, kuwa wazalendo na nchi yao, kwa kujenga
jengo hilo la kisasa na lenye viwango vinavyokubalika kimataifa.
Alisema,
moja ya jitihada za serikali ya awamu ya nane inakusudia kuimarisha kwa vitendo,
huduma za afya na ndio maana imeamua kujenga hospitali za kisasa, hivyo ni
wajibu kwa wakandarasi hao, kuheshimu hilo.
Makamu huyo
wa Pili, aliyasema hato wakati akiwa katika ziara yake ya siku mbili kisiwani
Pemba, alipofika wilaya ya Micheweni kuangalia maendeleo ya ujenzi wa hospitali
ya kisasa wilayani humo.
Alisema, ni
lazima kwa wakandarasi kuweka uzalendo wao mbele, na hasa baada ya serikali kwa
maksudi kuamua kuwatumia wakandarasi wazalendo.
“Kazi kwanza,
iwe imara na muhakikishe mnajenga hospitali hii kwa kiwango kinachokubalika, na
hilo litafanyika ikiwa mtaweka uzalendo wa nchi yenu mbele,’’alieleza.
Aidha Makamu
huyo wa Pili, alifafanua kuwa hata rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la
Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, mara zote amekuwa akisisitiza haja ya
kuwatumia wakandarasi wa ndani.
Aliwakumbusha
wakandarasi hao, kumaliza kazi kwa wakati kama walivyoahidi na kusaini mikataba
ya ujenzi, ili wananchi wapate kuyatumia kwa wakati.
“Nataka
nione kwanza jengo hili la hospitali ya Micheweni na Maziwani kwa wilaya ya
Wete na skuli za wilaya zilizopo
Makangale na Kinyasini nazo zinamalizika kwa wakati
uliopangwa,’’alieleza.
Mapema akizungumza
na wananchi wa Makangale, Makamu huyo wa Pili wa rais wa Zanzibar Hemed
Suleiman Abdulla, aliwataka, kulinda miundombinu ya majengo ya skuli, ili
kutimiza azma ya kuondoa msongamano madarasani.
Alisema,
moja ya wajibu wa wananchi ni kushirikiana na serikali yao, pale inapoanzisha
miradi ya maendeleo, ikiwemo barabara, hospitali au ujenzi wa madarasa.
“Serikali ya
awamu ya nane, sasa imo katika harakati za kutekeleza ahadi zake, sasa ni wajibu
wa wananchi ni kuonesha ushirikiano wa karibu, ili kazi zifanyike kwa
ufanisi,’’alisema.
Hata hivyo,
amewakumbusha wakandarasi wanaobahatika kazi za ujenzi, kuwatumia wananchi na
vijana waliokaribu na miradi hiyo, ili kujipatia ajira za muda.
Katika hatua
nyengine, Makamu huyo wa Pili aliwasisitiza wajenzi wa vyumba saba vya madarasa
eneo la Makangale wilaya ya Micheweni na Kiyasini kuharakisha ujenzi huo, ili
mvua zitakapoanza wawe wameshakabidhi serikali.
Akiwasalimia
wananchi wa shehia ya Kiyasini wakati akigagua ujenzi wa hospital ya wilaya,
Makamu huyo wa Pili aliwataka kuhakikisha wanailinda miundombinu hiyo, ili
endelevu.
“Hospitali
hii ikimalizika itakuwa na vifaa vya kisasa, na kila aina ya mashine za
uchuunguzi zinatarajiwa kuingizwa, lengo ni kuona wananchi wanapata huduma za
uhakikia za afya,’’alieleza.
Nae Mkuu wa
mkoa wa kusini Pemba na kaimu wa Mkoa wa kaskazini Pemba Mattar Zahor Massoud,
alisema fedha zinazotumika kwenye miradi hiyo ni za ahuweni ya COVID 19.
Alisema
matumaini yake, miradi hiyo itakapomalizika iwasaidie wananchi kwa asilimia
100, ili waondokane na usumbufu walionao sasa.
Kwa upande
wake waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar Nassor
Ahmed Mazrui, alimshukuru Makamu huyo wa Pili, kwa juhudi za kipekee, katika
miradi hiyo.
Alisema
utamaduni wake wa kuyakagua miradi hiyo kuanzia hatua za awali, inaonesha
dhahiri umakini wake katika kusimamia ujenzi wa miradi hiyo, ikiwemo hospitali
ya Micheweni na Kinyasini.
“Sisi wizara
tunafarajika kuona tokea ujenzi wa hatua za awali za hospitali za Micheweni na
Kinyasini unautembelea, ili kuona uimarika wake,’’alieleza Mazrui.
Nae
Mkadiriaji majengo kutoka Kampuni ya Group six ya China, Omar Asumani Mzirai,
wanaojenga hospitali y wilaya ya Wete iliyopo Kinyasini, alisema sasa wana wiki
ya saba tokea waanze ujenzi na umeshafikia asilimi 12 ya kazi yote.
“Mheshimiwa
Makamu wa Pili, awali tulikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji,
lakini kwa sasa hilo limeshaandoka na tunaendelea na kazi,’’alisema.
Makamu huyo
wa Pili na ujumbe wake ulitembelea ujenzi wa hospitali za wilaya za Micheweni
na Kinyasni kwa Wete, ujenzi wa skuli za wilaya zilizopo Makangale na Maziwani
mkoa wa kaskazini Pemba.
Mwisho
Comments
Post a Comment