IMEANDIKWA NA HAJI NASSOR, PEMBA
KWA miaka mingi, suala la haki za
watu wenye ulemavu halikuwa likoenekana na umuhimu wake, kuanzia hapa Zanzibar
na duniani kote.
Dunia
wakati inasonga mbele, hadi kufikia miaka ya 80, ambapo Umoja wa Mataifa UN, jumuiya
za watu wenye ulemavu zilianza kutetea upatikanaji wa haki za binadamu kwa watu
wenye ulemavu.
Suala ka
kutetea haki za watu wenye ulemavu, lilijotokeza hata kwenye vita vya kwanza
vya duniani vya mwaka 1914 na vile vya pili vya mwaka 1918, baada ya kujitokeza
kwa majeruhi kadhaa.
Mitandao
ya kijamii inahabarisha kuwa, kwa wakati huo waliotetea na kupata haki zao za
matibabu na huduma nyingine ni wale, waliopkumbwa na madhila kwenye vita hivyo
pekee.
Katika
eneo jengine mwaka 2006, Umoja wa Mataifa ulianzisha mkataba wa kimataifa
kuhusu haki za watu wenye ulemavu (UN -Convention on the Rights of Persons
with Disabilities- UNCRPD).
Shabaha
kubwa ya mkataba huo ilikuwa ni kulinda na kuboresha hali ya watu wenye walemavu
duniani kote, wapatao 650.
Na
tayari hadi mwaka 2015, mataifa 159 yashautia saini mkataba huo na mataifa 154
kati ya hayo, yaliidhinisha hatua hiyo.
Mataifa
yaliyokubali mkataba huo yamepokea wajibu wa kuhakikisha haki sawa za elimu, ajira,
kumiliki mali na kuoa, kama walivyo watu wengine.
Mikataba
hiyo pamoja na mambo kadhaa, ipo mikataba ukiwemo wa Umoja wa Mataifa ya Haki
za Watu Wenye Ulemavu, ulioasisiwa mwaka 1945, mkataba wa Kimataifa wa Haki za
Binaadamu.
Lakini
kulikuwepo kwa viwango vya kanuni na sheria juu ya nafasi sawa kwa watu wenye
ulemavu wa mwaka 1973, samba mba na Mkataba wa kimataifa juu ya Haki za Watu
Wenye Ulemavu (UNCRPD) wa mwaka 2009.
ZANZIBAR
Kwa
upande wa Zanzibar, masuala ya watu wenye ulemavu yalianzia katika ustawi wa jamii
chini ya wizara ya Afya kwa wakati huo.
Kisha mwaka
2004, yakahamishiwa chini ya Ofisi ya Waziri Kiongozi ambapo Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iliunda Idara ya Watu Wenye Ulemavu.
Pamoja hatua
hiyo, pia serikali ilianzisha Baraza la taifa la watu wenye ulemavu mwaka 2008,
ambapo sasa masuala ya watu wenye ulemavu yanashughulikiwa kupitia Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais.
SERA, SHERIA
NA MIONGOZO YA ZANZIBAR
Kuanzia hapo Zanzibar, ilianza kutambua na
kusimamia haki za watu wenye ulemavu, kutokana na hamasa ya kimataifa na
kikanda pia.
Ndio maana hivi karibuni, Makamu wa Kwanza wa
rais Zanzibar Othman Massoud Othman, ambapo Idara ya watu wenye ulemavu iko
chini yake, amesema lazima kila mmoja asimamie haki za watu hawa.
Anasema, suala la kusimamia haki za watu wenye
ulemavu, uwepo wa mikataba, sheria na kanuni ni hatua moja, lakini pili ni
ngazi ya jamii kuona wanapatiwa haki zao.
“Kila mmoja katika familia yake, wapo watu
wenye ulemavu wa aina yoyote ile, sasa ni wajibu kabla hata ya uwepo wa sheria,
kuona kundi hili ni sehemu ya jamii na wanastahiki haki zote,’’anasema.
Rais wa sasa wa Zanzibar Dk. Hussein Ali
Mwinyi, amekuwa akirejea mara kwa mara, kuitaka jamii kuwalinda kwa nguvu zote
watu wenye ulemavu.
Anasema, watu wenye ulemavu wana haki sawa
kama walivyo wengine, hivyo suala la kuwafanyia ukatili na udhalilishaji
lisipewe nafasi.
KATIBA YA ZANZIBAR
Kwa
upande wa Zanzibar, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo inayokatiba yake
ya mwaka 1984, pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2010, imetambua kuwa watu
wote wako sawa mbele ya sheria.
Kwa mfano
katika kuona kundi la watu wenye ulemavu halibaguliwi, kifungu cha 11 cha
katiba hiyo kimetaja usawa wa binadamu, kifungu cha 14 cha haki na uhuru wa mtu
binfsi.
SHERIA no 9/2006 HAKI NA FURSA
Sheria
hii yenye vifungu 47 na sehemu sita, imetungwa mwaka 2006, ili kukidhi haja na
kuonesha haki za watu wenye ulemavu Zanzibar.
Kwa mfano
kifungu cha 15 cha sheria hiyo, kimeanisha taarifa ya mawasiliano, (1) kimetamka
kuwa vituo vyote vya televisheni, vilivyosajiliwa Zanzibar vinatumia lugha ya
alama.
“Au
televisheni hizo, zinatumia maandishi katika taarifa zao ili, viziwi watumie
maandishi katika taarifa zote za habari, vipindi vya elimu na vile vya matukio
ya kitaifa,’’kinafafanua kifungu hicho.
SERA YA WATU WENYE
ULEMAVU
Sera hii imeweka ajenda za
Kitaifa ili kuhakikisha ujumuishaji wa watu wenye ulemavu kwa kuzingatia
mchakato wa kimaendeleo.
Serikali, imeandaa sera hii ili
kuifanya kuwa ni chombo muhimu cha kutoa maelekezo ya masuala ya watu wenye ulemavu.
Aidha ni kusaidia mchakato wa
fursa sawa, kupunguza umaskini na kukuza ujumuishaji wao katika ngazi ya jamii
na serikali kuu.
Sera imebainisha baadhi ya changamoto na vikwazo vinavyowakabili
watu wenye ulemavu Zanzibar, ikiwemo ufikiaji wa miundombinu, upatikanaji wa
huduma za umma.
Huduma za afya kwa
kundi hilo, ikitajwa kuwa bado hakuna dirisha wala eneo maalum, ambalo linaweza
kutumiwa na watu wenye ulemavu.
Suala la upatikanaji
wa taarifa, haki katika masuala la kisheria, jambo linalotajwa kuwakwaza na
kuwarejesha nyuma watu wenye ulemavu
Khamis Abdalla Sururu
ambae ni Mkurugenzi wa Jumuia kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa akili Zanzibar
‘ZAPDD’ anasema suala la vikwazo kwa watu wenye ulemvu linatengenezwa na jamii.
“Watu hawaoni umuhimu
wa kuweka miundombinu ambayo yatakuwa wezeshaji kwa watu wote, hadi pale
anapopata tatizo na kupelekea ulemavu,’’anasema.
Sururu anasema watu
wenye ulemavu, wameshajielewa nafasi yao, na kazi sasa iko kwa wale ambao
wanaona hawa ulemavu, na sasa ni kuandaa mazingira rafiki sasa.
Anasema kama kuna
ujenzi wa majengo ya umma, kama skuli, hospitali, barabara na hata kufikia
huduma za kibenki ni wakati sasa kuweka mazingira rafiki.
Bimkubwa Mohamed Ali
ambae ni mjumbe kwenye Jumuiya ya wanawake wenye ulemavu JUWAUZA, anasema bado
watu wenye ulemavu wanakabiliwa na chungu ya changamoto.
“Mfano hata
unapokwenda benki kutoa fedha kwenye mashine ‘’ATM’ hakuna nambari za nukta
nundu, jambo linalowatesa watu wasioona,’’anasema.
INETERNEWS
Ni moja ya shirika la
kimataifa linalowajengea uwezo waandishi wa habari katika kuwapa mbinu za
uandishi bora wa habari za watu wenye ulemavu.
Katika mafunzo
yaliofanyika hivi karibuni Zanzibar baina ya Machi 7 hadi 8, na kushiriki kwa
waandishi wa habari wa Unguja na Pemba, walielezwa hata majina sahihi ya
kutumia.
Mkuu wa program
kutoka Internews Tanzania Shaban Maganga, aliwaeleza waandishi hao kuwa moja ya
jina sahihi ni kusema mtu mwenye ulemavu na sio mwenye ulemavu.
“Wapo waandishi
wamekuwa wakieleza ulemavu wa mtu kwanza na kusahau ubinadamu wake, jambo
ambalo ni kinyume na haki za binadamu,’’anasema.
Mhariri mtendaji wa
shirika la Magazeti ya serikali Zanzibar
Ali Haji Mwadini, alisema waandishi wa habari wasipokuwa makini wanaweza
kuwaumiza watu wenye ulemavu.
“Unapoandika neno ‘kiwete’
badala ya mtu mwenye ulemavu’ au
mfano neno jengine lisilokubalika ni kusema ‘kipofu’ badala ya mtu asieoona na kumwita ‘asiyesikia’
badala ya kiziwi unaweza
kuwadhalilisha,’’anasema.
WANANCHI
Hilali Omar Mjaka wa
Chake chake, anasema kinachoonekana bado jamii haijakuwa tayari kuzitekeleza
haki za watu wenye ulemavu.
Aisha Hussein Sadala
wa Mchanga mdogo, anasema kama sheria na kanuni hazitumika kuwaabidhi
wanaozipinda haki na fursa za watu wenye ulemavu, kundi hilo litaendelea kupata
shida.
WAANDISHI W AHABARI
Fatma Hamad Faki
mwandishi wa blog ya pembayaleo, anasema kunahitaji uthubutu na ujasiri ili
kuyafikia makundi ya watu wenye ulemavu.
Mwandishi wa mitandao
ya kijamii Zanzibar Yassir Mkubwa, amesema mafunzo ya siku mbili yalioandaliwa
na Internews yamempa mwanga.
“Sasa nimeona maeneo
‘angle’ ambazo naweza kuziandikia habari na kutengeneza vipindi vya kuwasaidia
watu wenye ulemavu,’’anasema.
Mwisho
Comments
Post a Comment