Skip to main content

WANAWAKE NGUZO TEGEMEO KULINDA AMANI, MARIDHIANO ZANZIBAR

 



NA ALI SULEIMAN, PEMBA

SIKU zote kundi la wanawake na watoto, huwa ndio linaloathirika mno, hasa kwa ukanda wa bara la Afrika, pale nchi inapoingia kwenye migororo.
Kwa mfano, sasa angalia nchi kama Ethiopia, Sudan kusini, DR Congo, Yemen kwa wakati ule, Misri na hata Zanzibar kwenye mwaka 2001.
Kumbe kundi hili, inaonekana huwa ndio wahanga na waathirika wakubwa wa machafuko, migogoro na vita vya ndani ya nchi, kwa kule kuwa na uwezo mdogo wa kukimbia machafuko hayo.
Mwanaharakati maarufu wa haki za wanawake na watoto Mpalestina, Malala Yousafzai ambae mwaka huu anatimiza miaka 24, daima anasema wanawake duniani kote ndio wanaofanywa jaa.
Mwanaharakati huyu, ambae ameshaikwaa tunzo ya ‘Nobel’ akaenda mbali zaidi, akisema vita, migogoro, machafuko huanzishwa na wanaume, ingawa waathirika kisha huwa ni wao.
Kwengineko ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, anasema mchango wa wanawake ni mkubwa katika kulinda amani na kuendeleza maridhiano, kwani wao ndio waathirika wa machafuko.
Anasema, kutokana na kukumbwa na kushambuliwa na machafuko ya nchi, ndio maana amesema pia ndio wanakuwa na mbinu bora na wenye hamasa za kuhakikisha amani haichafuki.
Lakini hata mwanaharakati wa kitanzania Dk. Avemaria Semakafu, anasema hapendelei nchi kuingia kwenye migogoro na machafuko, kwani wanaobakia ndani ya nchi hiyo ni wanawake.
Anakerwa mno na vikosi vya ulinzi na usalama ambavyo, kwa kwaida huwatafuta vijana na wanaume, ili kuwaadhibu lakini mwishowe huishia kwa wanawake na watoto.
Kwa upande wa Zanzibar mwanaharakati Siti Abass kama alivyo Mzuri Issa kutoka TAMWA, wanakerwa kuona machafuko yanawagusa wanawake na watoto.
Ndio maana, sasa Zanzibar katika kudhibiti hilo, Disemba 6 mwaka huu wa 2020, baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alimtuea kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT- Wazalendo Maalim Seif Sharif, kuwa Makamu wa Kwanza.
Kisha Disemba 8, alimuapisha rasmi, kushika nafasi hiyo ambayo ipo kikatiba, hasa baada ya marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, yaliofanywa mwaka 2010.
KWANINI ZANZIBAR IWE NA MFUMO WA SERIKALI YA PAMOJA?
Moja ya sababu kubwa, ilitokana na siuntafahamu zilizokuwa zikiibuka kila baada ya miaka mitano, mara tu unapomalizika uchaguzi mkuu wa vyama vingi.
Kila mmoja ni shahidi kuwa, umoja, mshikamano na upendo kwa wazanzibari, upo tokea asili, ingawa kuanzia mwaka 1995 uliingia doa, kwa sababu ya harakati za uchaguzi mkuu.
Ndio maana safari tata za maisha kwa wazanzibar, ilidumu kwa chaguzi takriban nne, hadi pale mwaka 2010, aliyewahi kuwa Mwanasheria mkuu wa Zanzibar, marehemu Abubar Khamis Bakari, alipopeleka hoja binafsi baraza la Wawakilishi.
Hoja yake kwa mwaka huo 2010, pamoja na mambo mengine alitaka kuwepo kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa ‘SUK’ ili iwe sababu ya kuwepo kwa maridhiano na kufuta makovu ya kisiasa, yanayojitokeza kila baada ya kumalizika kwa uchgauzi mkuu.
Hapo, ilibidi suala hilo liwe la kikatiba zaidi, ndipo yalipojitokeza marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, na sasa kuanzia vifungu vya 39, vikatakamka kuwepo kwa nafasi ya Makamu wawili.
Ambapo, moja ni kuwepo kwa Makamu wa Kwanza, ambae anatoka kwenye chama kilichoshika nafasi ya pili kwenye uchaguzi mkuu, huku Makamu wa Pili akitoka kwenye chama kilichopata kura nyingi.
Sasa tayari, Zanzibar imesharudi tena kwenye mfumo wa serikali ya Umoja wa Kitaifa tokea Disemba 6, mwaka 2020 alipomaliza kula kiapo kwa Makamu wa Kwanza wa rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
WANAWAKE WANASEMAJE KWA MARIDHIANO HAYO Ifahamike kuwa, kama wanawake ndio waathirika wakubwa wa machafuko, hapa sasa pia inageuka ndio washika dau wakuu kuhakikisha maradhiano hayo yanaendelea.
Kwa mfano mwanaharakati wa haki za wanawake wilaya ya Chake chake, Sifuni Ali Haji, anasema wameunga mkono kwa kiasi kikubwa, kufikiwa maridhiano hayo.
Anasema, lazima wahamasishane baina yao kuona maridhiano yaliofikiwa Zanzibar yanakuwa endelevu, kwa maslahi mapana ya Zanzibar.
“Mimi nimeridhishwa kuona viongozi wetu wanafanyakazi pamoja, na sasa yale tuliokuwa tukiambiwa na Rais wetu wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwninyi kuwa yajayo ni neema tupu yameshaanza,’’anasema.
Kubwa Sifuni, anawataka wanawake wenzake kisiwani Pemba, kuhakikisha kila mmoja, na kwa nafasi yake, anatumia muda wa japo dakika 10, kuwaelezea umuhimu wa maridhiano hayo.
Kwa upande mmoja hata Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Pemba, Salama Mbarouk Khatib, anasema atatumia nafasi yake, kukutana na makundi mbali mbali vya wanawake, ili kuwaeleza umuhimu wa umoja.
“Umoja unazaa amani, upendo, mashikamano ambao umetokana na kusameheana na kuvumiliana miongoni mwa wazanzibari, jambo litakalowapa umahiri viongozi wetu,’’amasema.
Anasema chuki, kubaguana, kutengana, kukebehiana havina nafasi Zanzibar na kilichopo mbele yetu, ni kuungana ili neema ya Zanzibar mpya ifike.
Hata Mwenyekiti wa Tumaini Jipay Pemba ‘TUJIPE’ Tatu Abdalla Msellem anasema, yaliofikiwa na viongozi wakuu, baada ya kumalizika uchaguzi, lazima yaheshimiwe na kila mmoja.
“Sisi wanawake ndio ambao huingizwa kwenye migogoro, machafuko na hata vita, sasa panapofanyika jambo ambalo linamaslahi kwa umma, lazima tulidumishe,’’alieleza.
Anafafanua, huu sio wakati wa kufanya kebehi, dharau, tashititi bali kila mmoja kwa nafasi yake, ahakikishe anathamini na kutoa mchango wake.
Anabainisha kuwa, serikali ya Umoja wa Kitaifa ‘SUK’ ndio suluhisho la kufkia maendeleo ya kweli, kwa kule viongozi hao kukubali kufanya kazi pamoja.
“Kama viongozi wetu wa kisiasa, wameshakubaliana kufanya kazi pamoja, na mimi kama mwanamke, lazima niwashawishi wenzangu na hata kupitia asasi yangu kuunga mkono jambo hilo,’’anaeleza.
Mtetezi wa haki za wanawake wilaya ya Micheweni, Raya Said Rashid, anasema maridhiano yaliofikiwa yamefungua ukurasa mpya, kwa kule sasa watu kusahau vyama vyao.
“Sasa hapa nilipo Micheweni hata wanachama wanavaliana sare za vyama, hakuna CCM wala ACT, wote sasa letu moja, kilichobakia tuendeleze kazi mbele,’’anafafanua.
Hapa anataka kuona, sasa suala la vyama vya siasa lisiwe chanzo cha kuharibu udugu, umoja, mshikamano wao ambao upo tokea asili.
“Wazanzibari sote tuwamoja tokea asili, lakini hapo katikati tulishabikia vyama hadi kila mmoja kumpoteza mwenzake, hili jambo lisipewe nafasi, maana linadhoofisha maendeleo yetu,’’anabainisha.
Mwalimu wa Madrassa wa Mbuzini wilaya ya Chae Chake Fatma Khamis Mbarouk, anasema suala la kuridhiana lipo kisheria hata kwenye masuala la dini ya kiislamu.
“…….Aaussi na Khazrajii…ni makundi yaliohasimiana na kisha kufanya mapatano, sasa na sisi hili lazima tuliunge mkono na kuliridhia jambo lililofanywa na viongozi wetu,’’anaeleza.
Mwanakhamis Juma Msabaha wa Jumuiya ya wanawake Wete, anasema kama viongozi wakuu wameshakaa pamoja, hakuna budi na wengine wakiwemo makundi ya wanawake kufuata hilo.
“Tunajifunza kuwa, viongozi wanapokosana siis tuwashawishi wapatane na wanapopatana wao, sisi tufuate,’’anashauri.
MAKUNDI MENGINE YA JAMII YANASEMAJE
Kamanda wa Polisi mkoa wa kusini, Pemba Ahmed Khamis Makarani, hivi karibuni akizungumza na waandishi wa habari, alisema jambo kubwa, wanalolifanya kila siku ni kuhakikisha umoja wa wazanzibari hauchezewi.
Mufti Mkuu wa Zanzibar sheikh Saleh Omar Kaabi, amekuwa akirejea kauli yake ya mara kwa mara, kuwa kama uchaguzi mkuu umeshamalizika, watu waungane kufanya shughuli zao za maendeleo.
Hata Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi wakati akizungumza kwenye siku ya maadili, alisema maridhiano yaliofikiwa Zanzibar hayapaswi kubezwa.
Mwenyekiti wa Jumuiya sauti ya Vijana Pemba Said Mussa Rashid, anasema vijana wako wazi kuona maridhiano hayo yanafanyiwa kazi.
Anasema watahamasishana kama vijana, kuona kwanza umoja, mshikamano, amani na maridhiano hayo yanakuwa endelevu kwa maslahi ya taifa.
Klabu ya waandishi wa habari Pemba PPC nayo hivi karibuni ilishirikiana kwa Shirika la Internews, iliwajengea uwezo waandishi wa habari kuripoti habari za amani na maridhiano.
Mkutano huo wa siku moja uliofanyika mjini Chake Chake, ulilenga kuona waandishi hao wanawaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa maridhiano na utunzaji wa amani kwa maslahi mapana ya Zanzibar.
Ndio maana Mwenyekiti wa ‘PPC’ Bakar Mussa Juma, wakati akizungumza kwenye mkutano, alisema PPC imeona ni vyema kuwajengea uwezo waandishi hao, ili wasiwe chanzo cha kuharibu amani na maridhiano.
Hata wakati akiwasilisha mada ya namna ya kuandika habari za amani ‘peace journalism’ Mwenyekiti mstafu wa PPC Khatib Juma Mjaja, aliwataka waandishi hao kuhakikisha wanazitumia vyema kalamu zao.
Anasema maridhiano yaliofikiwa Zanzibar si vyema yakatiwa doa kupitia vyombo vya habari, na ndio maana PPC kwa kushirikiana na Interenews likaendesha mkutano.
Mwisho
Khadija Yussuf and Makame Khamis
1 Share
Like
Comment
Share

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...