Skip to main content

NASSRA SALUM MOHAMED, MJASIRIAMALI ALIYEANZA NA FUNGU LA NAZI SASA ANG'AA

 


 IMEANDIKWA NA HAJI NASSOR, PEMBA

“ZAMANI ilikuwa mikoba ile ya asili yakitumia ukindu, rangi tu na kisha unaitia mikono kazi kwisha,’’alianza hivyo mjasiriamali mbunifu, Nassra Salum Maohmed wa Wete.
NINI UKINDU
Ukindu ni aina ya jani refu mithili ya nyasi au lile la mnazi, ambapo mti wake kwa maana kigogo, kinafafana kwa karibu na mti unaoitwa Mchikichi.
Ukindu ambapo kisayansi huitwa, Phoenix reclinate, na mara nyingi mti huo, hustawi sehemu zenye kivuli, mbolea au kwenye jua mfano wa kwenye ardhi ya changarawe.
Lakini, kwa nchi za ukanda wa pwani kama vile Tanga, Pemba na Unguja, mti wa mkindu, hupendelea kumea kwenye maeneo yanayopitwa pitwa na maji maji au mtiririko wa mito na maziwa.
Ukindu mmoja ‘chane’ au ‘nyiza’ urefu wake ni kati ya sentimita 12 hadi 15 huku upana wake, ukiwa ni wastani kati ya nusu na robo sentimita.
NAMNA YA KUTAYARISHA MIKOBA YA ASILI
Baada ya kukaushwa kwa jua, jani hilo la ukindu, hupasuwaliwa katikati na kuzikusanya pamoja kuanza kupakasa kwa kuzizongomesha zongemesha pamoja kitaalamu kindu hizo.
Huwa mithili ya jamvi, busati na kupatikana kitu kirefu kinachoitwa ukili, ambao huwa na upana usiozidi nchi moja, ingawa urefu hutegemea na matumizi.
Mjasiriamali huyo mbunifu Nassra Salum Mohamed wa Kiuyu Kigorofani wilaya ya Wete Pemba, anasema baada ya hapo, ambapo kwa mkoba wa kawaida huhitaji ukili, wenye urefu wa pima tano hadi saba.
Pima moja aliyoitafsiri, ni kule kunyoosha mikono yako kwa upana, na hapo kipimo chake huitwa pima moja.
Ambapo ukili huo unakuwa na urefu wa wastani wa mita 5.5 hadi mita 11 kwa mkoba wa saizi ya kati, kwani pima moja ni mita 1.5, ambapo pamoja hilo suala kuweka rangi ni sehemu ya pambo.
“Unaweza kununua rangi kama vile kijani, zambarau, manjano na ukipika kili zako moja moja kwa rangi tofauti kwenye masufuria tofauti, kulingana na rangi wanazozipenda wateja wako,’’alieleza.
Baada ya hapo, unakuwa na kitu chenye ncha kali, mithili ya spoki ya baiskeli kinachoitwa shazia, ambayo huitoboa ncha na kuingiza kamba, mfano wa utembo au nyuzi za kipolo.
“Pembeni mwa kili zako, kunakuwa na tomo tomo nyemba mba ambazo ndizo zinazotumika kupitishia shazia, ikiwa na kamba, ambapo kisha hutengeneza jambo mithili ya jamvi au busati,’’anasema.
Mbunifu huyo anasema, kinachofuata hapo ni kupatikana mthili ya sanduku la mabo, ambalo inategemea na ukubwa wa mkoba unaouhitaji, na kuuvisha ukili wako, ambao tayari umeshaweka rangi uzitakazo.
Baada ya hapo, unaziba sehemu moja kwa kutumia shazia na kamba, na kutia kamba refu ambayo ndio mikono, ya mkoba na hapo unaweza hata kuandika jina upendalo.
“Ipo mikoba yenye majina kama ‘komamanga la kizimbani usimgaie jirani’ ukipata cheo usimsahau mkeo, au ‘umekuja kutembea hukujia umbea’ na mpenzi wangu I love you waliobakia how are you,’’anasema.
Bei ya mikoba hiyo ni kati ya shilingi 8,000 hadi shilingi 12,000 ingawa wakati mwengine, hutegemeana na ukubwa wa mkoba husika.


UBUNIFU WA MIKOBA YA KISASA
Nassra Salum Mohamed ambae ni mjasiriamali mbunifu, anasema baada ya kuona anatumia gharama kubwa na kupoteza muda kwenye mikoba ya zamani, alifikiria jinsi ya kuiongezea thamani.
Hapo alianza kubuni na kuiongezea kitambaa ndani, zipu na mchanganyo wa rangi kwa kutumia ukili na ukindu ambao ndio, anaoutumia kwa kutengenezea ile mikoba ya asili.
UTENGENEZAJI MIKOBA YA KISASA
Kwanza sasa ameachana na kutumia sanduku au bao kama vile mikoba ya zamani, na badala yake unatumia kuishona kwa cherahani ya kawaida, kwa kuunganisha kili zake.
Anasema kamba za utembo au vipolo, shazia sasa ameachana nazo, na kufanya kila kitu kwa cherehani, isipokuwa ile hatua ya kwanza ya upakasaji kili zako kwa kutumia mikono.
Wakati wa kuunganisha kili zako, kwa kutumia mashine ya cherehani, unaunganisha na vitambaa vyembamba ‘lining’ wastani wa mita moja, kulingana na ukubwa wa mkoba husika.
“Ukubwa wa kitambaa hutokana na ukubwa wa mkoba wenyewe, ingawa mengi hasa ninayoshona mimi kitambaa ni mita moja, na hukitia ndani kwa wingi na nje kidogo kama pambo tu,’’anasema.
Jengine ambalo ameiongozea thamani mikoba hiyo, katikati baina ya kitambaa huweka mfano wa kipande cha kipolo cha saruji na boksi, ili uwe mgumu mgumu mithili ya mikoba ya ngozi.
Mbunifu huyo anasema, mikoba hiyo bunifu hutumia dawa maalum nje ya mikoba inayoitwa ‘vanish’ kwa lengo la kukimbiza maji inapotokezea bahati mbaya ya kuroa.
“Jengine ambalo ndani ya mikoba hii bunifu inayo, ni kuweka zipu mithili ya begi au pochi la dukani, lakini huwa na mfuniko kama ile mikoba ya kike pamoja na vanishi ili maji yasikae,’’anaeleza.
Muundo wa mkoba huo, baada ya kutengenezwa, huwa mithili ya mkoba wa dukani au pochi la ulaya, kwa kule kuukuta kama vile umeshaingizwa nguo.
TOFAUTI KATI YA MIKOBA YA ASILI NA YA KISASA
Kwanza, mikoba ya zamani ilikuwa ni rashisi mno kuona kilichotiwa ndani yake, kwa kule kukosa zipu, ambayo kwa hii ya sasa ndio jambo la lazima.
Aidha mikoba ya kisasa, imewekwa na dawa ya vanishi nje yake, ambayo huruhusu maji kutoganda na kuzuia kilichowekwa ndani kuchelewa kuroa, kwa kule pia kuwepo kitambaa na maboksi pembezoni mwake.
Mbunifu huyo anasema, mikoba hii ya kisasa hata gharama yake ni ndogo wakati wa kuitengeneza, lakini imekuwa na wateja na hasa watalii au wafanyakazi serikalini na wafanyabiashara.
Kwenye utayarishaji kuanzia mwanzo hadi mwisho kupatikana kwa mkoba kwa ile ya zamani, ni kati ya siku tano hadi sita, ingawa hii ya kisasa sio zaidi siku nne hadi tano.
SOKO NA BEI YA MIKOBA YA KISASA
Mkoba mmoja anabainisha kuwa, anauuza kati ya shilingi 20,000 hadi shilingi 25,000 ingawa mara zote hutegemeana na ukubwa na wingi wa mapambo ya mkoba husika.
Anasema, mkoba huo kwa siku anaweza kutengeneza kati ya miwili hadi mitatu, na hasa ikiwa ameshakamilisha zana zake kwa maana kili, zipu, kitambaa na cherhani.
Anasema alipoanza alichelewa kupata wateja, kwa vile walikua wakishangaa na kuona sasa amebuni mikoba hiyo, ingawa baadae soko lake lilikua.
Ambapo kwa sasa anaowateja, kwanza kisiwa chote cha Pemba, Unguja baadhi ya mikoa ya Tanzania bara na tayari mikoba yake ipo ndani ya ardhi ya Kenya na Uganda kwa sasa.
“Wateja nashukuru sana wapo, na tunaposikia kuna maonyesho, sherehe na mikutano ya kitaifa tunakwenda na tunapata kuuza mno, maana sasa tunatengeneza hata kwa ajili ya wanaume,’’anasema.
Mikoba hiyo ya kisasa, pia imefungua soko kwa wateja wanaume kwa kule hata kutengenezewa mikoba maalum ya kutiliwa kompyuta mpakato ‘lap top’ na mengine kwa ajili ya safari.
WATEJA WA MIKOBA YA KISASA
Khadija Hassan Mwandini wa Mkoani, anasema ameanza kutumia na kuipenda mikoba hiyo, tokea aliponunua kwa mara ya kwanza, mwaka 2017, alipoikuta kwenye maonyesho ya biashara.
“Mimi tokea nianzi kutumia mikoba hii bunifu, sasa nna miaka minne sijaingia dukani kununua mkoba wala pochi la ulaya, bali natumia hii ya wajasiriamali wetu na hasa ya Bi Nassra,’’anasema.
Omar Haji Makame wa Chake chake, anasema aliwahi kutengenezewa mkoba maalum wa kutilia lapo top yake, na sasa anaendelea nao.
“Mikoba hii mwanzo nilijua kwa ajili ya wanawake tu, lakini nilipokutana na mbunifu huyo, akanitaka nichague rangi na sampuli niitakayo kisha baada ya siku nne, nilikwenda kuchukua,’’anasema.
Shajaki Mjaja Hassan wa Kojani Wete, anasema aliwahi kupata tenda ya mikoba hiyo, wakati alipokwenda Kenya, na aliwahi kuinunua 50, na kwenda kuiuza.



“Mimi nilinunua kwa bei ya jumla ya shilingi 22,000 kwa mkoba mmoja na kutumia shilingi milioni 1,100,000 na kisha kuuza mmoja, ambapo kwa pesa ya Tanzania ni shilingi 35,000 na kujipatia shilingi 1,750,000 hivyo kupata faida ya shilingi 650,000,’’anaeleza.
Wateja wengine Halima Juma Kheir wa Wete na Fatma Omar Kassim wanasema mikoba hiyo bunifu, ni mizuri mno kwa vile hata ulichokiweka ndani sio rahisi kuroa.
COSTECH
Mwezi Disemba mwaka jana, Tume ya taifa ya Sayansi na teknologia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ‘COSTECH’ ilikuwa na mafunzo ya siku tatu kisiwani Pemba kwa waandishi wa habari na watafiti.
Lengo la mafunzo hayo, ambayo yaliwakutanisha baina ya waandishi wa habari na watafiti hao, ni kundoa kutoelewana kikazi baina ya pande mbili hizo.
Ambapo COSTECH imebaini kuwa, wapo watafiti na watafiti kadhaa wamekuwa wakifanya tafiti, ingawa haziwafikii walengwa ambao ni wananchi na watunga sera.
Kwenye mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Maarifa kutoka ‘COSTECH’ Dk. Bunini Manyilizu, alisema ubunifu, utafiti na sayansi ndio kila kitu, ikiwa taifa linataka kusonga mbele.
Lakini akasema hayo yanaweza kufikia ikiwa tu waandishi wa habari watakuwa na uwelewa wa kuzifanyia kazi tafiti za watafiti na kazi za wabunifu.
“Ikiwa mtafiti amefanya utafiti na kisha ukabakia kwenye kabati, hautowasaidia watunga sera, watoa uamuzi na wananchi bali waandishi lazima wawasilishe kwa jamii,’’alisema.
Bunini akawataka waandishi hao, baada ya kumaliza mafunzo ya siku tatu, sasa kwenda kwenye maeneo mbali mbali kwa ajili ya kuwaibua watafiti na wabunifu.
Kwa upande mwengine Bunini anasema, hata wabunifu wanapaswa kutambuliwa kwa kazi zao, kwa vile wamekuwa wakitoa mchango wao mkubwa.
“Waandishi nendeni mkawaibue wabunifu wetu, ambao nao wana mchango katika kukuza pato la taifa, hivyo lazima watunga sera na watoa maamuzi waelewa changamoto zao,’’anasema.
TAMWA
Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA, ndio ambao walimuibua mbunifu huyo wa mikoba ya kisasa kuanzia mwaka 2017.
Ambapo awali, walianza na uwekaji wa hisa, kisha utengenezaji wa mikoba ya ukili, na kisha kuanza kufuga kabla ya kuendesha miradi mengine kama ya biashara ndogo ndogo.
TAMWA kupitia Afisa wake uwezeshaji Pemba Asha Mussa Omar, anasema mjasiriamali huyo Nassra Salum Mohamed, ni mmoja aliyekwisha wezeshwa na kupitia TAMWA, lakini wapo wengine zaidi ya 70 kisiwani Pemba.

mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...