Skip to main content

KUELEKEA KUMALIZA UDHALILISHAJI, DHAMANA HAKI YA MTUHUMIWA INAYOWAGAWA WAJAJI ZANZIBAR

 


IMEANDIKWA NA HAJI NASSOR, PEMBA

DHAMANA ni kitu au ahadi inayotolewa kumdhamini mtu anayetaka kukopa mali au anayekabiliwa na mashtaka mahakamani.
Wengine hueleza kuwa, dhamana ni ruhusa ya kuwa huru anayoweza kupewa mtuhumiwa wakati wa uchunguuzi wa kosa lake unaendelea au shauri lake linaendelea kusikilizwa mahakamani, au akisubiri uamuzi wa rufaa yake.
Suala la dhamana ni la kisheria nani la kikatiba zaidi, hivyo wanasheria huita, dhamana ni haki ya kikatiba kwa mtuhumiwa.
Dhamana ni haki inayopata msingi wake katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo ina dhana inayomtaka kwamba mtu hatochukuliwa kuwa mwenye hatia, mapaka tuhuma zithibitishwe dhidi yake, Ibara ya 13 (6) (b).
Kwa kuzingatia dhana hii ya haki ya kisheria, utaona ni muhimu kwa kumpa mtu dhamana apate kuwa nje ya kizuizi mpaka hapo tuhuma zake, zitakapothibitishwa na mahakama au upande wa mashtaka.
Kumbe nagundua sasa, dhamana ni haki halali kwa mtuhumiwa na sio zawadi wala upendeleo na kwa kosa lolote.
NANI MWENYE HAKI YA KUTOA DHAMANA?
Zanzibar nayo inazo sheria, kanuni na miongozo yake kadhaa inayochapusha kuendesha muhimili wa mahakama, kuanzia ya mwanzo hadi mahakama kuu.
Kabla ya mwaka 2018, makosa yasio na dhamana yalitajwa kwenye kifungu cha 150 (1) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai namba 7 ya mwaka 2004.
Ambapo sheria hiyo, ilitaja makosa yasio na dhamana kwa mtuhumiwa (mshitakiwa), kama vile kuua kwa maksudi, uhaini, ujambazi, kukamatwa na silaha ya moto pamoja na upatikana na dawa za kulevya.
Kwenye makosa hayo ambayo sheria hiyo kabla ya kufutwa kwake, pia kifungu hicho hicho cha 150 (4), kikasema mtuhumiwa aliyepatikana na moja kati ya makosa hayo anaweza kupewa dhamana.
Na hapo kifungu hicho kikasema ni Mahakama kuu pekee, ndio itakayokuwa na uwezo kisheria kutoa dhamana kwa mtuhumiwa na yeye baada ya kuomba dhamana ‘bail’ na kuingiza sababu za kuomba huko.
Kwa tafsiri ya kifungu hicho cha 150 (4), kinapotaja Mahakama kuu, moja kwa moja kinawalenga Jaji Mkuu na majaji wengine, maana imeshatajwa kuwa Mahakama hiyo itaundwa na Jaji mkuu na majaji wengine wasiopungua wawili.
Hapa tunajifunza kuwa, kwa sheria ile kongwe ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai namba 7 ya mwaka 2004, ilikuwa imetoa mamlaka na uwezo kwa Jaji yeyote wa mahakama kuu anaefikiwa na ombi au maombi ya dhamana, kuweza kutoa au kuzuia.
Hivyo ndivyo hali ya utoaji au uuzuiaji wa dhamana ‘bail’ kwa makosa yasio na dhamana ‘non boilable offences’ ndio ilivyo kuwa.
NINI KILIFUATA?
Wapo wanaharakati na hata waathiriwa wa matendo hayo, walianza kulalamikia kitendo cha kila Jaji, kuwa na uwezo wa kutoa dhamana kwa makosa yaliotajwa kuwa hayana dhamana.
Wapo waliohoji, iweje kila Jaji atoe dhamana wakati makosa hayo ni makubwa, na walidhani suala la kutoa dhamana liwe kwa Jaji Mkuu pekee.
Baada ya kelele za muda mrefu za waathiriwa wa matendo hayo pamoja na wadau wa haki jiani, wapo waliojitokeza kuziparamia ngazi za Mahakama kuu, kutaka kifutwe kifungu cha 150 (4).
Na mahakama iridhie kuwa awe Jaji Mkuu pekee ndio mwenye uwezo wa kutoa au kuzia dhamana kwa mshitakiwa kwenye makosa yaliotajwa kuw ahayana dhamana.
Sheria hiyo ya mwaka 2004, baada ya kupelekwa baraza la Wawakilishi, hatimae ikazaliwa sheria mpya ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai namba 7 ya 2018, kumbe kilichobadilika ni mwaka pekee.
UJIO WA SHERIA NO 7 MWAKA 2018
Kama tulivyoitaja kuwa jina lake ni sheria ya Mwenendo wa Makoasa ya Jinai namba 7 ya mwaka 2018, ambapo kwanza ilikuja kuongeza makosa yasio na dhamana.
Yaani kutoka yale makosa matano ‘5’ ya awali kwenye sheria kongwe na sasa kufikia makosa 11 ndani ya sheria hiyo mpya, ambayo sasa inatimiza miaka mitatu.
Na sasa kifungu cha 151 (1) kikayataja makosa hayo, pamoja na yale matano mengine yaliongezeka ni kukutwa na dawa za kulevya kwa kiwango kikubwa, ubakaji ‘rap’, kuingilia kinyume na maumbile.
Makosa mengine yaliotajwa kwenye kifungu hicho ni ulawiti, kubaka kwa kundi ‘rape gang ’pamoja na kuingilia maharimu awe mke au mume ‘insets’.
Sheria hii ambayo kwa sasa inakaribia kutimiza miaka mitatu tokea Machi 21, mwaka 2018 Rais mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipoisaini.
Nayo sasa kwenye kifungu chake cha 151 (4) kikaeleza kuwa, mwenye mamlaka kisheria ya kutoa dhamana sasa ni Jaji mkuu pekee.
Kumbe sasa, kwa sheria hii mpya, imemtaja Jaji mkuu pekee kuwa ndie mwenye uwezo kisheria wa kutoa dhamana kwa yale makosa 11 yaliotajwa kuwa, hayana dhamana.
MKINZANO WA WADAU WA HAKI JINAI
Yupo wakili maarufu Zanzibar akitajwa kwa jina lake la umaarufu ‘kijogoo’ aliziparamia ngazi za mahakama kuu Zanzibar, naye akiiomba mahakama hiyo kutoa ufafanuzi juu ya kifungu cha 151 (4).
Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii, alifika mahakama kuu ya Zanzibar, kwa madai kuwa, kifungu cha 151 (4) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai namba 7 ya mwaka 2018, kinapingana na kifungu cha 93 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Hapa hoja yake ni kwamba, kifungu cha 151 (4), kimemtaja Jaji Mkuu ‘Chief Justice ‘CJ’ pekee kuwa ndie mwenye uwezo wa kukubali au kukataa dhamana kwa makosa yasio na dhamana, likiwemo la ubakaji.
Wakati sasa kifungu 93 (1) cha Katiba ya Zanzibar kimetamka kuwa, kutakuwa na mahakama kuu ya Zanzibar, ambayo itakuwa ndio ya kumbu kumbu na kuwa na mamlaka yote ya kesi za jinai na madai.
Aambapo hata kifungu cha (2) kikasisitiza kuwa, Majaji wa mahkama kuu watakuwa na Jaji Mkuu na Majaji wengine wasiopungua wawili, watakaojulikana kama majaji wa mahkama kuu.
Kwamba, kumbe kumpa uwezo kisheria Jaji mkuu pekee kutoa au kuzuia dhamana, ni kinyume na Katiba, ambayo imeshatamka kuwa, Mahakama kuu inaundwa na Jaji Mkuu na Majaji wengine wasiopungua wawili.
Hivyo kifungu hicho cha sheria cha 151 (4), kilichoelekeza Jaji mkuu pekee, aliomba kifutwe na kwa wakati huo kilifutwa na Mahakama kuu chini ya Jaji Mhe: Abdull-hakim.
NANI ANAWEZA KUOMBA DHAMANA?
Kisheria, pamoja na kwamba kuna sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai nambari 7 ya mwaka 2018, inayozuia dhamana kwa washitakiwa, lakini bado imetoa haki hiyo.
Mwenye uwezo wa kisheria kuomba dhamana kwanza ni mtuhumiwa mwenyewe, ambapo kwa mfano anaweza kuiomba mahakama kuu.
Tena kizuri zaidi, hata kwa yale makosa yaliotajwa kuwa hayana dhamana, lakini zipo sababu kama za umri, ugonjwa, na yanapotokezea magonjwa ya mripuko.
Ndio maana mwezi Januari mwaka 2020, Mahakama kuu ya Zanzibar, iliamuru kupewa dhamana kwa aliyewa kuwa mtendaji mkuu wa Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC) wilaya ya Mkoani, Seif Suleiman Kassim, ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya ubakaji wa mwanafunzi wa miaka 13.
Ambapo uamuazi huo wa dhamana ulitolewa na marehemu Jaji wa Mahakama kuu ya Zanzibar, Mkusa Isack Sepetu, baada mahakama hiyo, kujiridhisha na maombi ya dhamana ya mtuhumiwa huyo ambayo yaliwasilishwa Januari mwaka huo.
Tena miongoni mwa sababu zilizomtoa nje kwa dhamana mtuhumiwa huyo, ambaye alikuwa mahabusu kwa muda miezi miwili, ni pamoja na wadhifa alionao kwenye eneo lake la kazi.
Jaji Sepetu alisema “mahakama imejiridhisha na hoja za mtuhumiwa huyo na ikiwemo kama akiendelea kukaa mahabusu kungeathiri shughuli nyingine za kitaifa, hasa kutokana na msimu huo wa uvunaji wa zao la karafuu ambalo ndilo kinara wa uchumi wa Zanzibar,’’.
Ambapo aliyefanya hayo wala sio Jaji Mkuu, bali ni Jaji ambaye kimsingi anaunda mahakama kuu, ambayo ilishatajwa kuwa, itaundwa na Jaji Mkuu na majaji wengine wasiopungua wawili.
Mfano mwengine wa kupatikana dhamana kwa makosa yasio na dhamana, ni wale washtakiwa wawili Azizi Idrissa Abdalla miaka 22 na Mkubwa Abdalla Mjaka miaka 20 wote wa Wawi, wanaokabiliwa na tuhuma ya kubaka kwa pamoja nao Mahakama kuu, iliwapa dhamana.
Wao walipatiwa dhamana, baada ya kuomba kupunguza idadi ya wathumiwa rumande, hasa ikizingatiwa kuwa, kwa wakati huo Zanzibar, ilikumbwa na ugonjwa corona.
UPI MSIMAMO WA WANAHARAKATI W AKUPINGA UDHALILISHAJI?
Tatu Abdalla Msellem anasema, bado baadhi ya Majaji wamejiona hawana mamlaka kisheria kutoa dhamana, na ndio kesi kadhaa ambazo hazina dhamana mtoaji wa dhamana huwa ni mmoja.
Anasema, hao wamekuwa wakitumia dalili mbali mbali, ikiwa ni pamoja na kwamba kesi zote za jinai ziko chini yao, hivyo suala la kutoa dhamana kwa kesi hizo ni sawa.
“Wengine Majaji wanaamini kuwa, kwa vile sheria imeshampa haki Jaji Mkuu pekee, hivyo wanapopelekewa maombi dhamana kwa makosa yasio na dhamana, hawatoi,’’anasema.
Sifuni Ali Haji anasema, kama kesi zisizo na dhamana mfano za ubakji na ulawiti zikiendela kutolewa dhamana, kuna dalili kubwa ya makosa hayo kunawiri.
“Kama sheria ya Mwenendo wa makosa ya Jinai ya mwaka 2018 imeshazuia makosa haya kutopewa dhaman, basi sasa isiwe kila Jaji anafanya apendavyo,’’anashauri.
WAATHIRIKA WANASEMAJE?
Mama ambae mwanawe alibakwa na aliyekuwa kiongozi wa ZSTC, anasema kupewa kwake dhamana kwa mshitakiwa, ni kudhoofisha mwenendo wa kesi hiyo.
Anasema, kesi hiyo inamashahidi wengi, sasa inakuwa ni rahisi kwa mshitakiwa anapokuwa nje kuwashahiwishi mashahidi wengine kutofika mahakamani.
“Kwa hakika suala la dhamana kupewa kwa watuhumiwa, lisiwepo maana alichokifanya yeye ni kosa la jinai, na nikinyume na haki za binadamu,’’anasema.
NINI KIFANYIKE?
Waathirika wanasema vifungu ambavyo vinamkanganyiko na hasa juu ya dhamana kwa watuhumiwa, viondolewe ili iwe dawa ya kwa wastakiwa.
Mwanaharakati kutoka TAMWA Fat-hy Mussa Said, anasema suala la dhamana liendelee kwa Jaji Mkuu pekee, na kusiwe na kila jaji kuwa na haki hiyo.
Aliyekuwa Mwanasheria Dhamana wa ofisi ya ‘DPP’ Pemba Ali Rajab Ali, anasema lazima sheria iondoe mipindo, ili kama kuna dhama iwe wazi na kama hakuna isiwe kwa watu maalum.
Mtoto Aisha Haji Kassim miaka 17 wa Madungu Chake chake, alisema kama sheria imeshayaorodhesha makosa yasio na dhamana, ibakie hivyo hivyo.
Mzazi Hasina Mjaka Hamad wa Vitongoji anasema kama sheria zikipindwa pindwa, na hata mitaani kesi hizo zitaendelea kunawiri
Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...