NA HAJI NASSOR, PEMBA
“MAJI ya chumvi yakitoka baharini, huwa na ujoto sifuri au kisaynasi inaitwa ‘zero Bobay’, hapo sasa lazima kuyaingiza kwenye bwawa ‘reserve’ ili kuyavumbika,’’
Ndivyo alivyoanza
mtaalamu na mkulima wa bidhaa ya chumvi ya mawe, Bakari Shaaban Bakari aliyeko
bahari ya mjini Kiungoni Wete Pemba, wakati akizungumza na mwandishi wa makala
haya.
Chumvi kwa maana ya kemia ni kampaundi inayofanywa
na ‘ion’ yaani anioni yenye chaji hasi na ‘Calcium
yenye chaji chanya baada
ya bezi kuunganika na aside au metali
yoyote.
Lakini, kuna aina nyingi za chumvi kutokana
na elementi mbalimbali
na hizi kwa jumla haziwezi kuliwa, na bindamu, kwa mfano chumvi ya aside, chumvi ya muungano.
Kwa
bahati mbaya, chumvi inayotumiwa na watu wengi haina madini ya kutosha ya sodium
na chloride
kutokana na kutengenezwa upya viwandani kwa kusafishwa (refined).
Utumiaji
wa chumvi sahihi na kwa kiwango kinachotakiwa, una faida nyingi mwilini,
ikiwemo kuimarisha na kudhibiti shinikizo la damu, kuboresha ufanisi wa misuli
ya mwili, kuboresha ufanisi wa ubongo.
Kwani, ubongo wa binadamu pamoja na uti wa
mgongo, vimo katika mfumo wa maji chumvi uitwao ‘cerebrospinal fluid).
BOBAY NI NINI?
Ni namba za kawaida
zinazotumika kuangalii ujoto wa maji ya chumvi, yanapotolewa baharini hasa kwa
ajili ya kuyatayarisha kwa uzalishaji wa chumvi ya mawe.
Namba hizo, zimo kwenye
kifaa kirefu cha kigae kinchoitwa hydrogen.
Kwenye kifaa hicho, zimo
nambari zilizo anzaia zero hadi 30, ambapo unapokiweka kwenye maji ya bahari
yaliotengwa bila ya kuingilia na mengine, hupanda kulingana na ujoto wa maji
husika.
KWANINI KITUMIKE KWENYE UZALISHAJI WA CHUMVI?
Kisayansi mtaalamu huyo
mzaliwa wa Kenya, anasema maji ya bahari yote duniani, huwa na ujoto ‘0’
ambapo hilo huwezi kulijua kwa kuangalia kwa macho pekee, wala kuingiza mkono,
bali lazima utumie Hydrogen na
kuangalia Bobay zilivyopanda
ama kushuka.
“Ukiingiza tu kifaa cha hydrogen, basi utaona namba
zinapanda, kuanzia sifri hadi 30, itategemea na ujoto wa maji yalivyo,’’anasema.
HATUA ZA
UZALISHAJI WA CHUMVI YA MAWE KISAYANSI
Hatua ya kwanza, anasema
ni kujenga bwawa ‘Reserve’
lililokaribu na bahari, na kisha ni kuingiza maji ya bahari, ambapo hapo,
kisayansi huwa na ujoto wa wa sifuri.
Kwake yeye bwawa lake
lina upanda wa mita 12, wastani wa pima 6 za za mkono na urefu wa mita 24 sawa
na pima 12 za mtu mzima.
Ambapo bawawa hilo moja hubeba
lita 600 ya maji kutoka baharini, na kisha kwenye uvunaji hujipatia kati vipolo
80 vyenye ujazo wa kilo 50, sawa na 4,000.
Anazidi kufafanuwa kuwa,
maji ya chumvi asili yake yana chumvi aina zaidi ya 200, ikiwa ni pamoja na Magnesium, sodium corbinate, ambayo
inayotumika na binaadamu ni chumvi aina ya sodium chloride.
Kisha hapo maji yatakaa
kwa muda wa siku tatu hadi nne na lazima uwe na bwawa jengine, ambalo kisayansi
linaitwa ‘condenser’.
“Maji ya chumvi ukiyaweka kwenye bwawa la
kwanza ‘reserve’ kisha
yanaweza kupanda ujoto ‘Bobay’
hadi kufikia kati ya tatu hadi nne,’’anasema.
Kifuatacho hapo sasa,
utayahamisha maji hayo kwa kutumia mpira wa maji, na kiyaingiza kwenye bwawa
jengine.
Wakati unayingiza kwenye
bwawa hilo, tayari joto la maji hayo kutoka baharini, yatakuwa limeshapanda, na
sasa utalazimika kuyagawa wenye mabwa mawili tofauti.
Hivyo sasa maji
yatalazimika kuwekwa kwenye condenser
nambari moja na condenser
nambari mbili, ambapo baada ya siku tano sasa ‘Bobay’ hupanda hadi kufikia kati ya 10 hadi 15.
KWANINI MAJI YAPADE JOTO JUU ‘Bobay’?
Kisayansi, maji ya bahari
unapoyachukua na kuyahifadhi sehemu bila ya kuingiliwa maji mengine kama ya
mvua, huzalisha joto kali mno, ambapo baadae hukauka na kufanyika kitu mithili
ya chumvi.
Wakati wa hayo
yameshafika ndani ya Condenser
nambari 2, yakiwa na ‘Bobay’ 10
hadi 15, huendelea kuvumbikwa hapo kwa siku 4, na yatakuwa yanapimwa kila siku,
na hadi yatakapofikia ‘Bobay’ 20
kisha huhamishwa tena.
Mtaalamu huyo,
anabainisha kuwa, sasa hapo maji hayo yatakuwa mazito mithili yamafuta ya nazi,
na yatahamishwa tena kwenda kwenye bwawa nambari 3, condenser number three.
Wakati yakifika ndani ya
bwawa hili nambari tatu, yakiwa na ujoto wa uniti 20, yataachwa hapo, hadi
lipande tena na kufikia‘Bobay’ au
uniti 25 huhamishwa na kusafirishwa hadi kwenye bwawa nambari nne, kitaalamu
linaloitwa Evaporator or crostalyser.
Anasema dalili za
kuelekea kuzaliwa kwa chumvi, ni kuona kwenye bwawa, kuwepo kwa ukungu ukungu
au utandu utandu ambao huo ndio chanzo cha chumvi husika.
“Juu ya maji ukiona kama
kuna vumbi vumbi au ukungu fulani, basi hiyo na chumvi inaanza kushikana na
kisha kadiri unavyokuwa mzito, huanguka chini,’’anaeleza.
Kwa kwaida chumvi huanza
kuzaliwa juu ya maji, ambapo kisha huanguka chini ndani ya ‘bwawa’ na kisha
kadiri ‘Bobay’ zinavyopanda,
na chenga chenga huongezeka,’’anafafanua.
Ndani ya bwawa hilo
namabri nne, mtaalamu na mkulima huyo anafafanua kuwa, ukiona sasa kipimo chako
cha hydrogen kinaonesha Bobay’ zimeshafikia 26 hadi 27, hapo
chumvi sasa imeanza kuzaliwa.
“Hapo sasa hata kwa macho
ya kwaida, unaweza kuanza kuona chenga chenga za chumvi, ambapo sasa husubiriwa
kupevuka kwa siku 10 tu, kabla ya kuanza kuvunwa,’’anaeleza.
Tokea siku ya kwanza ya
kuyahifadhi haji hadi kufikia siku ya kuvunwa chumvi, kwa kilimo cha siku ya
kwanza, huwa ni kati ya siku 27 hadi 30.
UVUNAJI WA CHUMVI
Kwanza, iweleweke kuwa,
chumvi ili ipatikane hakuna haja ya bwawa nambari nne, likauke kama wengine
wanavyofikiria.
Bali hatua zilizoelezwa
hapo, ni sawa na uvumbikaji wa maji ya bahari, kwamba chumvi hii ya mawe,
unaweza kuvuna na bwawa likiwa na maji yake.
Kwani mkulima huyo na
mtaalamu wa uzalishaji chumvi, anasema, kwanza unatumia majiti maalum
yaliotengenezwa mithili ywa mfano ‘mop’
au ‘rake’.
“Hili huwa inakusanyiwa,
maana haishauriwi kutumia mikono, kwa vile inaweza kuua alama za kiganja, na
kupoteza alama za finger print,
anafafanua.
Anasema, unaikusanya
pamoja vishungu vishungu na kufanya kuoikosha kwa maji hayo hayo ya chumvi, na
baada ya dakika 5 hadi 10, unanza kuingiza kwenye chombo.
KWANINI CHUMVI ITIWE MADINI JOTO ?
Madini joto ni aina ya
unga unga fulani, ambao kazi yake kubwa ndani ya mwili wa mwadamu, ni pamoja na
kukazanisha mifupa.
Vyakula karibu vyote
vinavyotoka baharini, hujengwa na madini joto, iwe samaki au chaza.
Sasa ili wananchi wapate
madini hayo muhimu, ndio maana huwekewa kwenye chumvi, na kwa mfano sayansi
inataka kuwa madini joto yenye ujazo wa kijiko kimoja cha kulia, iyayushwe kwa
maji lita 10.
“Hivyo kwanza uwe na maji
yenye ujazo wa lita 10, unachanganya pamoja na madini joto, ujazo wa kijiko
kimoja cha chai, na kisha unaimiminia chumvi na kichanganya pamoja,’’aneleza.
Madini joto yanafaida
kubwa mwilini wa binadamu, ikiwa ni pamoja na, kwa mama mjamzito kupata kizazi
bora.
Kinga dhidi ya maradhi ya
kuvimba shingi ‘goiter’ kupata
ukuaji mzuri wa watoto, kujenga ubongo, kutozaa watoto weye ulemavu wa akili.
WATEJA WA CHUMVI WANASEMAJE?
Mfanyabiashara Khamis
Muhidi Khamis wa Chake Chake, anasema chumvi hiyo ndio pekee, anayopenda
kutokana na kuzalishwa kitaalamu.
Anasema, kwanza iko
nyeupe, imeingizwa madini joto na ukali wake hausababishi uchungu kama zilivyo
chumvi nyingine.
Hata Omar Haji Makame wa
Wete, anasema kwa miaka minne sasa, ameachana na kuagizishia bidhaa hiyo kutoka
Mkoani Tanga na Mbombasa Kenya, bali ananunua kwa mkulima huyo.
Mwanaishi Hamad Hassan wa
Mchanga mdogo, anasema yeye na wenzake wamekuwa wakitumia chumvi hiyo, kwa kule
kugaiwa wanapokwenda siku za mavuno.
COSTECH
Mwezi Disemba mwaka jana,
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknologia ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ‘COSTECH’ kwa kushirikiana na Tume ya Mipango Zanzibar, iliendesha
mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari na watafiti.
Moja ya malengo ya
mafunzo hayo, ni kuwaleta karibu waandishi na watafiti, ili kufanya kazi kwa
karibu na kuwasaidia wabunifu, ili kupata taarifa za kitafiti.
Ndio maana wakati
akifungua mafunzo hayo ya siku tatu, Mdhamini wa Tume ya Mipango Zanzibar
kisiwani Pemba Dadi Faki Dadi, alisema tafiti zinaumuhimu mkubwa kwa maendeleo
ya nchi.
Alisema tatfiti
zilizofanywa na kisha kuishia kwenye makabati, haziwasaidii wananchi, hivyo ni
wajibu wa watafiti hao, kukutana na waandishi wa habari, ili kuwawasilishia
wananchi na watunga sera.
Kwenye mafunzo hayo, Kaibu
Mkurugenzi wa Utawala na Maarifa kutoka ‘COSTECH’ Dk. Bunini Manyilizu, alisema
utafiti na sayansi ndio kila kitu, ikiwa taifa linataka kusonga mbele.
mwisho
Comments
Post a Comment