NA MOZA SHABAN, PEMBA@@@@ SERIKALI ya awamu ya nane, imekuwa ikigeuza sekta ya elimu kwa vitendo, ikiwemo ujenzi wa dahalia. Maana lengo hasa ni kuwapunguzia umbali wa kutembea masafa marefu wanafunzi, pale wanapokwenda na kurudi skuli. Dahalia hizo, zimekuwa zikiwasaidia wanafunzi hao, katika kuongeza ufaulu na maarifa ya kujifunza, masomo yao na kupata utulivu, wa kujiepusha na vitisho vya udhalilishaji. Maana alishasema mara kadhaa, Ofisa Mdhamini wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Mohamed Nassor Salum kuwa, wamekuwa wakipokea kesi za vitisho vya ubakaji kwa wanafunzi. Anasema, wapo wanafunzi hasa kuanzia kidato cha nne, wamekuwa wakiviziwa vichakani, iwe wanapokwenda ama wanaporudi masomoni. ‘’Mazingira haya ya ujenzi wa dakhalia, ni kuwahakikishia ulinzi wao, maana mingi yapo karibu mno na skuli, wanazosoma,’’anasema. Anakiri kuwa, wahalifu wa ubakaji, walishazoea kutumia vichaka, ili kuwadhalilisha wanafunzi. ‘’Sasa wanafunzi wetu hasa wa...