NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
KIPYENGA cha kampeni za uchaguzi mkuu, kwa upande wa Zanzibar,
kilipulizwa Septemba 12.
Hapo,
ilikuwa ni nfasi kwa wagombea, kujitupa viwanjani na kwenye kumbi mbali mbali,
kutangaaza sera na ilani zao.
Kwa
Tanzania, kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Siasa, uchaguzi hufanyika kila
baada ya miaka mitano.
Maana
uchaguzi wa kwanza, wa vyama vingi nchini ulifanyika pale mwaka 1992, na sasa
taifa hili linaelekea kufanya uchaguzi wake wa saba, Oktoba 29, mwaka huu,
yaani kesho.
IIishazoeleka,
kila unaposikia neno uchaguzi, huihusisha jinsia ya wanaume pekee, jambo ambalo
ni kukiuka mikataba, sheria na katiba.
Ijapokua, kwa sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022, Tanzania ilionesha wanawake ni wengi zaidi kwa asilimia 51.6 na wanaume 48.4, lakini takwimi hizi hazinauhusiano na uwingi wao, kwenye safu ya uongozi.
Kwa upande wa Zanzibar,
sensa ikamulika kuwa, wananchi wote ni milioni 1.8, kati yao wanawake wakiwa laki
974,281 na wanaume ni 915,492.
Eneo jingine, Zanzibar
inayo mikoa mitano, ingawa wakuu wake wa mikoa wanawake ni wawili tu, huku
takwimu zikiumiza tena kichwa kwenye wilaya 11, wanawake wakiwa wawili.
Hayo yanaendelea
kuwaumizwa vichwa wanaharakati kuona nini kinakwamisha wanawake kutokuwa wingi
kwenye uchaguzi, kwengineko ni majimbo 18 wawakilishi wakiwa wanne pekee wanawake
ksiwani Pemba.
Lakini,
chenyewe chama cha UDP, kimemuamini mwanake, kupeperusha bendera ya chama chao,
katika nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ushupavu
wa mgombea huyo Saumu Hussein Rashid, amesema lengo la chama hicho ni kufungua
fursa za kiuchumi kwa kila mtanzania, ili aweze kujitosheleza kupitia biashara yake.
Ameyasema
hayo alipokuwa akizungumza na wajasiriamali wa soko la Tibirinzi Chake chake
Pemba, wakati akitoa sera ya chama hicho na kuomba kura kwa wafanyabiashara
hao.
Anasema kuwa
atahakikisha anakuza kipato cha watanzania, ili kuifungua kiuchumi kwa
kila mjasiriamali, aweze kujitosheleza katika mahitaji yake.
Alifafafanua
kuwa atahakikisha anaweka miundombinu mizuri, itakayowawezesha
wajasiriamali wadogo, ili waweze kuwa wafanyabiashara wakubwa, kwa
kuongeza pato lao.
‘’Niwambie
wajasiriamali nina nia njema na ilani ya chama change, ni kuwanyanyua kiuchumi,
ili muwe wafanyabiashara wakubwa, muweze kujitosheleza katika mahitaji yenu,’’ alifafanua.
Alieleza
kuwa chama hicho kimejidhatiti, katika suala la upendo daima, pamoja na
kuendeleza kudumisha amani, umoja na utulivu.
KILICHOMSUKUMA KUOMBA NAFASI HIYO
Anasema,
ni kuona wanawake na watu wenye ulemavu, wakilalamikia kudororo kwa uchumi,
jambo linamlokasirisha.
Njia
pekee ni kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na pindi
akipewa ridhaa atalitekeleza hilo kwa vitendo.
‘’Nina
hamu sana kuwataka watanzania, wahakikishe wananipa kura za ndio, ili nije niwatumikie
kwa dhati,’’anasema.
Eneo
jingine, anasema ni kuona wananchi, wananufaika na rasilimali zao, ikiwemo mazao
ya biashara na taifa.
Lakini,
akwaahidi wanawake, kuwa hawatodhalilishwa tena, na kisha kesi zao kubakia
kwenye mafaili ya mahakamani, kama ilivyo sasa.
‘’Niwahakikishie
kuwa, nikiingia madarakani, jambo la mwanzo sheria zitarekebishwa, maana
nimegundua wanawake wanadhalilisha na hawapati haki zao,’’anasisitiza.
HAWAOGOPI WANAUME KWENYE KINYANG’ANYIRO HICHO
Anasema,
hana hofu, wasiwasi na wagombea wanaume, maana anasema hawaendi kwenye jukwa
kwa mapambano ya mwili, bali wanashindana kwa sera.
Mgombea
huyo, anasema ilikuwa kazi rahisi mno, ndani ya chama chake, baada ya
kutangaaza nia kukubaliwa, kutokana na ujasiri wake.
‘’Mara
tu wajumbe waliponikubali kuwa nipeperushe bendera, ndipo nilipoanza, kujiamini
na sikuwa na hofu hata mgombea mwingine,’’anasema.
Akawataka
wanawake, waendelee kutetea haki zao za kudai uongozi, iwe ngazi ya familia,
taasisi, udiwani, ubunge n ahata urais kama mimi,’’anashauri.
WAFANABIASHARA WANAMATUAMINI GANI?
Mfanyabiashara
wa soko la Chake chake kwa niaba ya wenzake Mohamed Juma, wamemuomba
mgombea huyo, kuwaimarishia soko hilo, ili liwe katika mjumuiko na muanganiko
wa biashara zote.
‘’Sisi
wafanyabiashara tumejitenga kupitia biashara zetu mbali mbali, tunakuomba
utuimarishie soko letu, liwe la kisasa na lenye muonekano mzuri,’’ alifafanua.
Nae
Omar Haji Omar, amesema anayomatumaini ya karibu, pindi mgombea huyo akipata
ridhaa, kwa kuimrisha biashara zao, kutokana na kuwa na sera za kijamii.
Khadija
Yussuf Mgeni, anasema kwa sasa wajasiriamali wadogo, wanaendelea kudidimia,
kutokana na kodi na matozo yasiozingatia mwenendo wa soko.
‘’Mimi
kura yangu utaipta kesho Oktoba 29, maana sera za ahadi zako, kwangu
zinanipeleka kwenye ndoto za kuwa mjasiriamali mkubwa,’’anafafanua.
WANAWAKEW WANASEMAJE
Aisha
Haji Hassan wa Chake chake, anasema mgombea huyo ana dira la kuwainua kiuchumi,
na sio kuwakandamiza.
Khadija
Ali Hija wa Madungu, anasema amekuwa akimfuatilia mgombea huyo, na amekuwa na
sera kama mbobevu wa uchumi.
‘’Wanawake
kama hawa wanafaa mno kuwaunga mkono, maana sera zake hazionekani kama za kubabaisha,’’anasema.
WANAHARAKATI
Amina
Ahmed Mohamed, ambae ni Kaimu Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania TAMWA-Zanzibar ofisi ya Pemba, anasema wanayo haki sawa ya kuongoza,
kama walivyo wanaume.
Anasema,
wakati umefika sasa kwa wapiga kura, kuwaamini wagombea wanawake, kuanzia ngazi
ya udiwani hadi urais.
Mashavu
Juma Mabrouk, ambae ni Mratibu wa Baraza la taifa la watu wenye ulemavu,
anasema kadiri siku zinavyokwenda, na wanawake wanaanza kuonekana.
‘’Lakini
juhudi inahitajika mno, maana wanawake wamekuwa wakiburuzwa kwa uhaba wao,
katika vyombo vya maamuzi,’’anasema.
Mohamed
Hassan Ali, anasema sheria kwa vile zinawaruhusu kuomba nafasi za uongozi,
jamii iendelee kuwaamini.
KATIBA/SERA/MATAMKO
Katiba ya Zanzibar ya 1984, kwenye kifungu
cha 11 na cha 14, vimeweka wazi kuwa kila mzanzibari anayo haki na uhuru wa
kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi, juu ya mambo yanayomuhusu.
Dira ya Zanzibar ya 2050 imeelezea jinsi gani
masuala ya usawa wa jinsia, juu ya kuondoa unyanyasaji na kuimarisha mifumo ya
uwezeshaji wanawake.
Sera ya jinsia inaeleza ushiriki wa wanawake
katika vyombo vya utoaji maamuzi, katika ngazi zote ni mdogo na kwa hivyo
serikali, itafanya juhudi kuona makundi yote na yaliyopembezoni.
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC) ambayo mkataba wake ulitiwa saini mwaka 2008 inaeleza, kutaka
kuondoa utafauti na kuwatenga wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Na kusaidia kuwepo usawa wa kijinsia katika nchi
wanachama na kufikia asilimia 50/50 kwenye ngazi zote za maamuzi.
Makubaliano yanayojulikana kama ‘Itifaki ya
Maputo’ ambayo yalifanyika Msumbiji mwaka 2003, inacho kipengele kinachoonyesha
haki ya wanawake, kushiriki katika siasa na mchakato wa vyombo vya kutoa maamuzi.
Mkataba wa kimataifa wa kutokomeza aina zote
za ubaguzi, (CEDAW) wa mwaka 1979, ambao unapinga aina zote za udhalilishaji na
kusisitiza, ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi.
Ibara12, inasisitiza ushiriki sawa wanawake na
wanaume kufikia asilimia 50 kwa 50, kwenye nyanja za maamuzi, serikalini na
taasisi binafsi.
Aidha jukwaa la Mpango wa Utekelezaji wa
Beijing mwaka 1995, ibara ya 7 kinataka ushiriki katika vyombo vya maamuzi kwa
kuzingatia uwiano wa kijinsia kwenye ngazi zote.
Mwisho





Comments
Post a Comment