NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
PINGINE wapo wanaodhani kuwa, mwanamke ku kiongozi, kuanzia
shehia hadi taifa, ni kama hidaya.
Hidaya ni zawadi ambayo inawezekana mtu asipewe au apewe kwa mtoaji,
akiona ipo haja hiyo.
Na wale wenye mamlaka na uwezo wa kushawishi mwanamke kupata
nafasi ya uongozi, hudhani kuwa hili ni zawadi kwao.
Maana utasikia kauli kutoka kwa viongozi wanaume wakisema kuwa,
kamati ya shehia fulani kama ina wajumbe 12, basi angalau wanawake wawe watatu.
HALI HALISI
Wanawake wanasema wamekuwa wakishuhudia kauli za kukatisha tamaa
kuwa, hutumika maneno kama vile angalau wanawake wawili, lazima wanawake
waepo.
Fatma Haji Dau wa mtandao wa wanawake Mkoani anasema, imekuwa kama
zawadi kutokana kwa wanaume wanapotaka kupewa nafasi.
Anasema kwa karne hii, tayari wameshapa uwelewa wa jinsi ya
kuongoza, sasa hakuna majaribio tena kuwapa uongozi wanawake bali kama ni haki,
itekelezwe.
Anabainisha kuwa, sheria mama ambayo ni katiba, inavyo vifungu
vinaeleza kuwa, kila mmoja yuko sawa mbele ya sheria, hivyo hakuna zawadi
katika hilo.
“Mwanamke na mwanamme wote wako sawa mbele ya sheria, sasa iweje
sisi wanawake tuonekane kwenye masuala ya uongozi, kama ni hidaya na wala sio
haki,’’anasema.
Mwanaisha Khasmi Mzale wa Msingi Chake chake anasema, sasa
wapewa haki zao uongozi, maana wameshakaa nje kwa karne kadhaa, jambo ambalo
liliwaacha nyuma.
Anasema zipo taasisi binafsi kama vike Chama cha waandishi wa
habari Wanawake Tanzania -TAMWA Zanzibar, imeshawawezesha kiuongozi, hivyo
mamlaka husika zihakikishe kuna kuwa na usawa kwenye uongozi.
Hata mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto wa mjini Wete
Sahaba Mussa Said, katika moja ya mikutano yake, aliwahi kusema kuwa, suala la
uongozi kwa wanawake sio hidaya.
“Kama kundi la wanaume wanapewa nafasi za uongozi bila ya mwenye
mamlaka kuhoji uwezo wake, hivyo na sisi kikatiba tuko sawa,’’anafafanua.
Katika eneo jingine mwanaharakati huyo, anasema kama kwenye
suala la uchaguzi kwa maana ya kupiga kura wanawake huweko mbele, kampeni ni
uwingi wa kwenye vyama na uongozi isiwe ajenda.
WANAWAKE WAHAKI YA KUWA VIONGOZI?
Kaimu Mwanasheria wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba,
Mohamed Hassan Ali anasema jawabu ni kweli kuwa mwana haki sawa na wanaume
kwenye uongozi.
Anasema sasa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa vyama
vingi ndani ya taifa la Tanzania bara na visiwani, ni wakati kwa wenye mamlaka
kuona waliona kundi hilo.
“Wapo wanawake wa mfano mzuri hapa Zanzibar akina Amina Salum
Ali, Salama Mbarouk Khatib ambae kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba na
hata mawiziri wa sasa akina Riziki Pemba wamefanya vizuri,’’anasema.
Kazija Haji Mohamed wa Wambaa, anasema sasa wapewe nafasi nao
waongoze ndani ya Zanzibar na hata kule Tanzania bara, maana muda wa majaribio
kwoa umekwisha.
‘’Kama mamlaka zilikuwa zikitujaribu kwa miaka 60 tokea
tujitawale weyewe, sasa wameshatujua uwezo wetu, kilichobakia watupe nafasi
hizo ili tuongoze,’’anabainisha.
Riziki Hamad Faki wa Mkoani anasema bado zipo nafasi kama za
wakurugenzi, makatibu tawala mkoa, manaibu mawaziri, manaibu makatibu wakuu na
hata masheha wanaweza kuongoza.
Anasemakwa usikivu na ahadi ya rais wa awamu ya nane ya Zanzibar
Dk. Hussein Ali Mwinyi ya kuwapa kipaumbele, wanawake bado tamaa ya kushika
maeneo kadhaa kiungozi tunayao,’’anasema.
Mjumbe wa baraza la vijana Chake chake Mwanakhamis Haja Khamis
anasema wakati umefika sasa kupewa nafasi za uongozi, maana asasi za kiraia
kama TAMWA zimeshawawezeshwa.
Anasema kwa vile suala la uongozi kwa mwanamke sio hidaya kutoka
kwa mtu mwingine, ndio maana lazima iwe 50 kwa 50 kati yao na kundi la wanaume.
“Hadi sasa kwenye vyombo vya maamuzi bado sisi tuko kidogo,
hivyo inakuwa vigumu kutatua changamoto zetu hilo, lakini mwarubaini wa hili ni
kupewa nafasi,’’anasema.
TAMWA WANASEMAJE
Kaimu Mratibu wa TAMWA-Pemba Amina Ahmed Mohamed, anasema wanawake
sasa wako ‘fit’ kushika nafasi yeyote.
Anabainisha kuwa, baada ya kundi la wanawake kuishi kizani kwa
zaidi ya miaka 100, sasa wakati umefika nao kuweka kwenye mwagaza kwa kupewa
nafasi ya uongozi.
Anasema, wanawake kama walivyo wanaume hakuna hata mmoja
aliyetajwa kwenye Katiba wala sheria na mikataba mbali mbali, juu ya suala la
uongozi.
“Kama katiba imetaja sifa za mkuu wa wilaya, mkoa, mbunge,
mkurugenzi na nafasi nyingine bila ya kuhusisha jinsia, hivyo hakuna kutengwa
kwa wanawake,’’anaeleza.
Anasema walishawawezesha wanawake kushika nafasi ya uongozi
tokea miaka ya 2008, kupitia miradi yao kadhaa ukiwemo wa WEZA I, WEZA II na WEZA
IIII, pamoja na ule wa SWIL kuwajengea uwezo kimitaji.
“Sasa wanawake wa Unguja na Pemba, wako tayari kushika nafsi za
uongozi, maana wamewiva kitaaluma, wanajiamini hivyo mamlaka ziwakumbuke
kiuongozi,’’anasema.
Hata Mkurugenzi wa TAMWA Zanzibar Dk. Mzuri Issa Ali akizungumza
kwenye uzinduzi wa muongozo wa mwanamke na uongozi hivi karibuni, alisema bado
kiu ya wanawake kushika nafasi ya uongozoi haijazimwa.
“Lakini hatuna budi kumpongeza rais wa Zanzibar wa awamu ya nane
Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuwaona wanawake kuanzia wakuu wa wilaya, mkoa,
mawaziri, makatibu wakuu na hata Katibu mkuu kiongozi,’’anasema.
WANAWAKE VIONGOZI
Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Pemba Salama Mbarouk, amekuwa akirejea
kauli yake, ya mara kwa mara kuwa, wanawake ni viongozi madhubuti na imara
wanapopewa nafasi.
Anasema ingawa kwa serikali ya awamu ya nane, imejitahidi
kuwakumbuka, ingawa bado jitihada za kweli zinahitajika kumpa nafasi mwanamke
katika uongozi.
Mwakilishi wa Jimbo la Chambani Bahati Khamis Kombo, baada ya
kutangaazwa kushika nafasi hiyo mwaka 2020, alisema anataka kuuoneshwa
ulimwengu kuwa, wanawake wanaaminika.
Alisema, kwa miaka mitano iliyopita aliwafanyia mengi na ndio maana
wananchi wake, ni miaka mengine mitano ya 2025, anatarajia kuitekeleza vyema
Ilani ya chama chake.
“Mimi sioni sababu ya kuibua mijadala na vikao visivyo na
Mwenyekiti kufikiria sana mamlaka zinapotaka kumpa nafasi ya uongozi mwanamke,
kwani kila kundi lipo sawa mbele ya sheria,’’anasema.
Mwakilishi wa Jimbo la Gando Maryam Thani Juma, anasema kama sio
hila na baadhi ya wanaume, kuanzia kwenye vyama hadi siku ya kupiga kura, na
wanawake kupata mwamko tokea zamani, kuingia majimboni, sasa mambo yengekuwa
mazuri.
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja Suzan Peter
Kunambi akizungumza kwenye mikutano ya kusikiliza kero za wananchi, alisema
anataka kuhakikisha hakuna udhalilishaji wilayani mwake.
“Mkombozi wa wanawake na watoto sasa kaja ndani ya wilaya yenu,
ninachohitaji kwenu ni ushirikiano ili kufikia ndoto zangu za uongozi, maana
huwa tunaambiwa mwanamke hawezi,’’anasema.
WENGINE WANASEMAJE MWANAMKE KUPEWA UONGOZI
Mwanidishi wa ITV/Redio One Pemba Suleiman Rashid Omar anasema,
wana haki kikatiba, na wapo waliofanya vizuri kwenye nafasi zao akiwemo Makamu
wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Hussein Ali Mwinyi, alisema anawaamini sana wanawake katika uongozi, kutokana
na ukweli, subra, uvumilivu na uweledi wanapopewa nafasi.
Mwanaharakati wa haki wanawake na watoto Tatu Abdalla Msellem
anasema uongozi kwao sio hidaya ni haki yao kikatiba, hivyo hakuna mjadala wa
kupewa nafasi hizo.
Aliyekuwa Msaidizi Katibu ofisi ya Mufti Pemba sheikh Said Ahmad
Mohamed, anasema hakuna kizuio kikubwa katika dini suala la kumpa uongozi
mwanamke wa kiislamu.
“Kinachoshauriwa tu, iwe kupewa kwake huko huo uongozi, hayapi
kisogo majukumu na wajibu wa familia yake akiwemo mume wake kwa aliye kwenye
ndoa,’’anasema.
Taarifa ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC,
inafafanua kuwa, kwa uchaguzi wa 2020, wanaume walioteuliwa na vyama kugombea
kuingia katika Baraza la Wawakilishi walikua 190 na walioshinda ni 42 wakati
wanawake walikuwa 61 na walioshinda ni wanane (8).
Taarifa za Shirika la Wanawake la Umoja wa
Mataifa (UN Women) na Umoja wa Mabunge (IPU) za 2017 zimeonesha kuwepo ongezeko
dogo la viongozi wanawake katika serikali na mabunge.
Maana katika majimbo 50 ua uchaguzi ya
Zanzibar, wanawake katika baraza la kutunga sheria, wanane hii ni saw ana
asilimia16, wabunge ni wannne kwa asilimia 8, mawaziri ni sita sawa na
asilimia 33 na Makatibu Wakuu ni saba sawa na asilimia 39.
Kati ya wakuu wa mikoa watano Zanzibar,
wanawake ni wawili, huku wakuu wa wilaya 11, wanawake wakiwa watatu pekee,
ambapo na masheha wanawake ni 81 kati ya 388.
Katiba ya Zanzibar ya 1984, kwenye
kifungu cha 11 na cha 14, vimeweka wazi kuwa kila mzanzibari anayo haki na
uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo
yanayomuhusu.
Aidha
Dira ya Zanzibar ya 2050 imeelezea jinsi gani masuala ya usawa wa jinsia juu ya
kuondoa unyanyasaji na kuimarisha mifumo ya uwezeshaji wanawake.
Sera ya jinsia inaeleza ushiriki wa wanawake
katika vyombo vya utoaji maamuzi, katika ngazi zote ni mdogo na kwa hivyo
serikali, kwa kushirikiana na wadau wengine, itafanya juhudi kuona makundi yote
na yaliyopembezoni.
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika SADC) ambayo mkataba wake ulitiwa saini mwaka 2008 inaeleza,
kutaka kuondoa utafauti na kuwatenga wanawake katika nyanja mbalimbali za
maendeleo na kusaidia kuwepo usawa wa kijinsia katika nchi wanachama na kufikia
asilimia 50/50 kwenye maamuzi.
Makubaliano yanayojulikana kama ‘Itifaki ya
Maputo’ ambayo yalifanyika Msumbiji mwaka 2003, inacho kipengele kinachoonyesha
haki ya wanawake, kushiriki katika siasa na mchakato wa vyombo vya kutoa
maamuzi.
Mkataba wa kimataifa wa kutokomeza aina zote
za ubaguzi, (CEDAW) wa mwaka 1979 ambao unapinga aina zote za udhalilishaji na
kusisitiza, ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi.
Ibara 12,
inasisitiza ushiriki sawa wanawake na wanaume kufikia asilimia 50/50
kwenye nyanja za maamuzi, serikalini na taasisi binafsi.
Aidha jukwaa la Mpango wa Utekelezaji wa
Beijing mwaka 1995, ibara ya 7 kinataka ushiriki katika vyombo vya maamuzi kwa
kuzingatia uwiano wa kijinsia kwenye ngazi zote za uongozi.
mwisho


Comments
Post a Comment