NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA
KATIKA miaka ya hivi karibuni, wanawake wamekuwa mstari wa
mbele katika nyanja nyingi za uongozi, kuanzia siasa hadi biashara.
Hata hivyo, safari yao haijakosa changamoto,Ingawa dunia
imepiga hatua katika masuala ya usawa wa kijinsia, bado wanawake wengi wanakosa
nafasi sawa za kushiriki katika maamuzi
Dunia ya sasa imekua kiteknolojia hususa ni ushiriki wa
wanawake katika kutoa mamuzi na hata kusimamia uwongozi wa nyanja mbali mbali
nchi.
Tanzanzia ni moja ya nchi ambayo kila ifikapo October hufanya uchaguzi kila baada ya miaka 5 kuwapa
nafasi wananchi ya kuchagua kiongozi wanaye mtaka.
Takwimu za
Zanzibar zinaonyesha kuwa katika
uchaguzi wa mwaka 2020, waombaji wanawake walikuwa 135 kati ya jumla ya 601
waliojitokeza kuchukua fomu sawa na asilimia 22.4% na mwaka 2025 zaidi ya
asilimia 75 ya wagombea wanawake wamejitokeza kugombania.
Hii ni kutokana na elimu iliyotolewa na wadau mbali mbali
wakiwemo wa haki za binadamu ili kuona usawa wa kijinsia umefikiwa.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Pandani Salama Massoud amesema kuwa ,lengo la chama chao ni kumuwezesha mwananchi
kujikwamua kiuchumi na kufikia uchumi wa soko la kati kimataifa ili nchi
kuendana na ukuwaji wa kiteknolojia uliopo.
Salama ni mwenye umri wa miaka 47 mkazi wa mzambarauni mwenye elimu ya kidato cha nne mwenye taluma ya uwalimu ngazi ya cheti ambaye pia amebahatika kua na nafasi ya ofisi ya bunge EALA ambaye anahudumua kama katibu muktasi binafsi wa Mbunge wa CUF
Amesema kilicho msukuma kuamua kugombea nafasi hiyo ni
kuhakikisha analeta mabadiliko jimbo la Pandani katika nyanja mbali mbali.
Alifahamisha kuwa, ataweka miundombinu rafiki
itakayowawezesha wajasirimali na wananchi wa kipato cha nchi kuweza kujikwamua
kimaisha kwa kuanzisha miradi itakayowaletea kipato.
"Malengo yangu ni kuhakikisha nakipatia ushindi chama
cha wananchi CUF na kuijenga Zanzibat inayoendana na mtazamo mpya unaoendana na
dunia ya mahitaji ya dunia ya sasa inayomilikiwa na teknolojia,"alieleza.
Amesema atahakikisha wananchi wanamiliki mlo wa mara 3 kwa
siku ili kukuza ustawi mzuri wa mwili na akili sambamba na kukuza sekta ya
uchumi husasa ni kwa wajasirimali pamoja na kukuza pato la zanzibar katika
mazao yaliyopo ikiwemo karafuu.
Ukosefu wa ruzuku haukusita katika kufanya kampeni zake kwa
kuimarisha uzalengo wa chama chake kwa wananchi wake ili kuhakikisha malengo
yake matimia na hata ya jimbo lake.
Asha Makame Juma mkazi wa Pandani ambaye pia ni mwanachama
wa chama cha CUF asema amefurahishwa na sera za mgombea ubunge huyo na
atashirikiana nae ili kuona wanaleta mabadiliko katika jimbo lao.
Juma Khamis faki amesema kuchagua kiongozi ni haki ya kila
raiya hiyp hawana budi kuona na wao wanapata haki hiyo kwa kujitokeza kwa wingi
na kuona wanatimiza haki yao ya msingi ili kuoa na taifa imara.
Salma khamis Mjasirimali mdogo mdogo alieleza, jinsi
alivofurahishwa na sera ya kuwawezesha wajasirimali kwani bado kuna uhitaji
katika kuhakikisha wajasirimali wanafikia malengo yao hivo ni kuona badailiko
katika hatua hiyo.
"Sisi kama wanawake tunashirikina kwa pamoja ili kuona
wanawake wenzetu wanashika nafasi mbali mbali katika ngazi za mamuzi hususa ni
serekali.
Chama cha wandishi wa habari Tanzanzia TAMWA kwa
kushirikiana na wadau mbali wa haki za binadamu wamesema kuwa wanawake wanayo
haki sawa ya kushiriki na kuongoza kama walivyo wanaume.
Aliyasema hayo Kaimu Mratibu wa Chama cha Wandishi wa Habari
wanawake Tamwa TAMWA Zanzibar ofisi ya Pemba Amina Ahmed Muhammed.
Katiba ya Zanzibar ya 1984, kwenye kifungu cha 11 na cha 14,
vimeweka wazi kuwa kila mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa
ukamilifu katika kufikia uamuzi, juu ya mambo yanayomuhusu..
Serikali ya Zanzibar imejidhatiti kuweka rasilimali maalum
(mfano: bajeti, kamati kitaifa) kama sehemu ya kuhakikisha utekelezaji wa
usalama wa wanawake.
Dira ya Zanzibar 2050
inaweka msingi mzuri wa sera na mwelekeo kwa masuala ya usawa wa jinsia,
kuondoa unyanyasaji wa kijinsia, na uwezeshaji wa wanawake. Hata hivyo, ama
utekelezaji wa vitendo, ushiriki wa wanawake kwa ukamilifu katika ngazi zote,
na ufuatiliaji wa kina ni maeneo ambayo yatahitaji nguvu zaidi ili dhamira hiyo
iwe matokeo.
Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Lipumba amesema wanawake
walio wengine wamepata elimu na uwelewa wa kushiriki katika nafasi mbali mbali
za kugombani uwongozi ili kuona nchi sasa inaenda na uswa wa kijinsia katika
kushiriki na kushirikishwa kwa wanawake.
Mgombea huyo hakusita kuwasisitiza wananchi endapo
watamchagua wataona mabadiliko makubwa husasa katika nyaja muhimu ili kuona
mabadilo ya jimbo la Pandani na kuwa mfano kwa majimbo mengine.
Ushiriki wa wanawake katika nyanja mbali mbali utasaidia
kujenga taifa imara na lenye usawa wa kijinsia.
Mwisho.
Comments
Post a Comment