Na Nihifadhi Issa, Zanzibar@@@@
Mkurugenzi mkuu wa chuo
cha Indian Institute of Technology Madras (IIT) Prof.Preeti Aghlayam amesema
wataendelea kuiunga mkono serikali kuhakikisha
somo la hesabati linapewa kipau mbele maskuli.
Akizungumza baada ya
kumaliza kwa mtihani wa majaribio uliofanyika katika chuo hicho huko bweleo
mkoa wa mjini magharibi alisema kufanya hivyo kutapelekea kuwa na wataalamu wa
wazuri ambao watajikita katika teknolojia mbali mbali.
Alieleza kuwa lengo ni
kufanya majaribio ya mitihani hasa katika somo la hesabati kuona wanafunzi hao wanakuwa na uwelewa mpana hasa
katika masomo ya sayansi ikiwemo hesabati pia ni kuunga mkono maadhimisho miaka 60 ya muungano wa tanganyika na
zanzibar.
Mrajis wa IIT madrasa
mshauri Abdallah Khamis amesema kuwepo kwa siku hiyo ya kuwatahini mabingwa wa
hesabati kutasaidia wanafunzi kujenga kujiamini na kujitahidi kufanya vizuri
katika somo hilo ambalo limekuwa naa kinyan'ganyiro kikubwa cha ajira.
Akizungumza kwa niaba ya
walimu wa skuli zilizoshiri katika mashindano hayo mwalimu Ame Haji Vuai kutoka
skuli ya Lumumba amesema mashindano hayo yanajenga hamasa kwa wanafunzi katika
kulipenda soma la hesabati amesmea lumumba imekuwa ikifanya vizuri kutokana na
jitihada za walimu kuwasimamia vyema
wanafunzi katika masomo yao.
Nao wanafunzi washiriki
wamesema wamepata mwanga wa kutambua ushindani uliopo katika kufanya hesabati
bila ya kutumia vifaa visaidizi vya kieletroniki katika kupitia somo hilo
sambamba na kutoa wito kwa wanafunzi
wenzao kuzidisha bidii ili kufanya vizuri.
Shindano hilo lilipewa
jina la IITM mathematics chmpionship ambapo mshindi wa kwanza ni Abdulhalim
Rajab Ameir kutoka skuli ya sekondari Fedha
na wapili ni mwana arab saidi kutoka skuli ya Lumumba.
Comments
Post a Comment