NA AMINA AHMED, PEMBA @@@@
UNAPOZUNGUMZIA nafasi ya mkuu wa mkoa mwanamke kwa Pemba, kamwe huwezi kuliacha jina la Salama Mbarouk Khatibu.
Salama hakumbukwi tu kwa nafasi hiyo, kwa wale wanaofuatilia historia yake, kwanza alianzia nafasi ya kuhudumu ukuu wa wilaya za Chake chake na Micheweni kwa nyakati tofauti.
Wapo wanaokumbuka ngarambe zake na jitihada zake za uongozi, wakati ule wa awamu wa saba, alipokuwa mkuu wa wilaya ya Chake chake kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Micheweni.
Kiongozi huyu mwanamke anachukuwa mfano wa mwanamke Hajar na Ibrahim, ambae nae bila ya kujali changamoto na maneno ya kukatishwa tamaa, aliutumika umma.
Hajar, ambae alikuwa mwanamke jasiri, mwenye nia nzuri, aliyeihama nchi yake, ili aende akaishi kando ya nyumba ya Mungu katika ardhi, kame isiyo na maji wala manyasi ili amwabudu Muumba.
HUYU HAPA MKUU WA MKOA KASKAZINI PEMBA
Salama Mbaroku Khatib, nae ni kama mfano huo, ndivyopale anapoamuwa kutekeleza majukumu yake ya uongozi ndani ya mkoa wa Kaskazini Pemba kwa vile hajali muda, juwa wala mvua.
Kwake salama anasema, anachotamani jua linapozama ni kukamilisha majukumu yake, na hasa ya kuwahudumia wananchi kama dhamira baada ya kula kiapo kushika nafasi hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa Makala hii, anasema ndoto zake ni kuona Mkoa huo wananchi wake wanaishi bila ya shida za dhahiri, mfano huduma za kijamii.
‘’Mimi nimekula kiapo kuhakikisha wannachi wa wilaya za Micheweni na Wete wanaishi kwa utulivu na huduma za kijamii za lazima ninawafuata wao,’’anasema Salama.
Salama Mbarouk Khatib ni mwanamke pekee aliteuliwa kuongoza mkoa wa kaskazini kwa mara ya kwa za kati ya wakuu wa mikoa 14 waliopita kabla yake.
Ndio pekee ambae rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, aliyekambidhi kijiti cha uongozi kwa nafasi hiy, kati ya wakuu wa mikoa watano waliopo Unguja na Pemba.
Anasema alichokifanya Dk. Mwinyi ni utekelezaji kwa vitendo vile vifungu vya kila mmoja ana haki sawa na mwenzake, vilivyomo kwenye Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania yam waka 1977 na ile ya Zanzibar yam waka 1984.
Ambapo katiba hizo, kama ukizichungulia kwa kina, zimeweka haki sawa kati ya mwanamke na mwanamme, (50 kwa 50) iwe kwenye uongozi au haki nyingine za kikatiba.
"Kwanza nimshukuru sana Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuniamini na kunikabidhi wananchi wa mkoa wa kaskazini Pemba, 272, 091, wakiwa wanaume 131, 484 na wanawake 140, 607 (sensa 2022),’’anasema Salama.
Kwake nafasi hiyo, anaona umempandisha ndege ya kufungua ukurasa mwengine katika kitabu chake cha historia, ambapo anaona kila anapokutana na changamoto, huzigeuza kuwa fursa.
Kumbe RC Salama ni mkuu wa mkoa wa 15 kwa mujibu wa uteuzi, ingawa kati ya hao, wote walikuwa ni wanaume, jambo ambalo linaonesha mabadiliko na wanawake kupanda chati.
WAPI ALIANZIA SALAMA?
Kwake anasema, hakuwa mjuzi wala mtaalamu wa kuongoza nafasi yoyote, lakini alichofundishwa wakati wa kusimamia majukumu yake, ni kujiamini.
‘’Siri kubwa niwaambie wanawake wenzangu kikubwa ni kujiamini na tunapopata nafasi inatubidi tuitendee haki ipasavyo, ndivyo wanavyofanya hata hao wanaume”, anasema.
Baada ya kutoka wizara ya wanawake na watoto, na kupata uteuzi wake wa kwanza kuwa mkuu wa wilaya ya Chake chake, anasema aliiingia na hofu ya kawaida kama mwanadamu, ingawa alipaya ushirikiano wa kutosha.
Anasema, kama mgagaa na upwa hali ugali mkavu, basi yeye alikuwa akigagaa na watumishi wenzake na kusikiliza ushauri, na kufanya uamuzi wa pamoja wakati huo.
Mashaallah, Allah amjaalie mafanikio mema, wepesi na utayari wake katika utendaji kazi kabla ya kuteuliwa kuongoza nafasi hiyo kumechangia kufika hapa alipo sasa.
Anasema ingawa alianza kupikwa na kupikika, wakati akiwa Ofisa Mipango, wizara ya wanawake na watoto Pemba, hivyo hata alipoteuliw akushika nafasi hiyo, ilikuwa rahisi kiasi.
" Nilikuwa najiamini na naitendea haki kazi niliopewa sekta niliyopangiwa sikuwa na hofu wala woga, pakutolewa uamuzi kama kiongozi nilikuwa natoa, pakushauri nilikuwa nashauri pia,’’anakumbuka.
Anasema miongozo, sera na sheria ndio zinazomlinda kila mtumishi, ingawa suala la kujiamini na kuacha hofu katika kazi ndio mwarubaini kwake, unaopmpa uhakika wa kuwatumikia wananchi.
Jukumu la uongozi alilonalo huku akiwa ni mke, lakini pia mama wa familia, haliathiri utendaji wake kazi, hivyo ni kusema maisha ya uongozi hayaathiri familia yake bali yanaongeza
heshima na mashirikiano.
Anasema kila kitu ni kujipanga na kukipangilia, lakini mimi kwa nafasi zote nilizowahikushika hadi hii ya Mkuu wa Mkoa, sioni dhiki na kuihudumia familia yake.
Kwake haamini kuwa, mwanamke akipewa nafasi inaweza kumshinda kwa sababu ya familia, bali anachokiona ni ikiwa atakosa kujipanga na kujipangilia inaweza kuwa changamoto.
" Mimi ni mama ambae nina mume na nina watoto, serikali inanitegemea lakini niseme kwamba kikubwa ni kujifahamu tu , kuwa wewe ni kiongozi na nyumbani wewe ni mama ambae unastahiki kufanya majukumu yako,’’anasema RC Salama.
Anaeleza kuwa wananchi wameamka sasa hivi hawaangalii jinsia wanaangalia utendaji kazi aliwaasa wanawake wenzake kutuogopa fursa wasizichezee wafanyekazi kadri ya uwezo wao na suala hilo linaweza kuwapa fursa kusonga mbele.
Anasema licha ya watu wachache kumtia midomoni, katika utowaji wa maamuzi ya kiutendaji, katika uongozi wake hakulipokea suala hilo kama ni kikwazo kwa upande wake.
" Kuna baadhi ya watu wanaotaka wakuendeshe vile wanavyotaka wao kwa maslahi yao binafsi, jambo ambalo kwangu silipi kipaumbele naamua kwa kufuata sheria,’’anafafanua.
Kwake anaona ukifanyakazi kwa dhati, hasa ndio changamoto na kasoro zinapoonekana na ukikosa kasoro wewe sio binaadamu au ukizikataa.
kwahiyo nakubali kushauriwa lakini zaidi na angalia ule ushauri ninaopewa je hautokweda kinyume na sheria za serikali, jee
una maslahi ya taifa, hautoathiri serikali ndipo naufanyia kazi kikubwa ninachoangalia ni hicho", alisema.
ANAOFANYA NAO KAZI RC SALAMA
Mgeni Khatib Yahya mkuu wa wilaya ya Micheweni, anasema kuwa kiongozi huyo ndie ambae alikuwa anajifunza mambo mengi kutoka kwakwe.
Anasema alipokuwa Mkuu wa wilaya ya Wete kabla ya kuhamishiwa Micheweni, alivuna mambo mengina na mazuri na hasa suala la kujiamini.
Kwake alikuwa ndio kioo, katika kufanikisha majukumu yake ya kila siku, na hatomsahau tena maana, alimfundishi wa vitendo aina ya uongozi na kuongoza.
"Najifunza siku hadi siku mambo mazuri kutoka kwa mkuu wa Mkoa Salama Mbarouk Khatib, ananishauri ananipa maelekezo kama msaidizi wake na natekeleza majukumu yangu vyema kwa kufuata nyao zake zaidi za uthubutu,’’anasema.
Mkuu wa wilaya ya Wete Dk. Hamad Omar Bakar, wanaotaka kuona kuwa mwanamke anaweza kuongoza katika mazingira yoyote, wafike mkoa wa kaskazini Pemba.
Kwake mkuu huyo wa Mkoa anamuona mtu wa tofauti, ambae ana nia thabiti ya kweli katika kuitumikia nafasi hiyo na wananchi, bila ya kujali mvua, usiku wala jua kali.
‘’Sisi wakati mwengine tunafikiria kwa mvua inavyonyesha jambo fulani, mkuu wa mkoa atalighairisha, lakini mara unamuona huyo amefika sehemu,’’anasifia mkuu wa wilaya Wete.
WANANCHI
Aziza Makame Abass Mkaazi wa Limbani wilaya ya Wete, anasema kuwa jitihada inazofanywa na mku huyo wa mkoa, katika kuleta maendeleo, zinaonekana.
Anasema maeneo mengi aliyarithi yakiwa na changamoto za ukosefu wa huduma za kijamii kwa uhakika, ingawa kwa sasa kila eneo hali inridhisha.
"Kwanza binafsi nampenda anavyofanya kazi nikisikiliza radio jamii nisipomsikia jioni basi asubuhi nitamsikia anazungumzia jambo lolote tunajuwa hasa wa kama tuna kiongozi sio wengine ambapo hata kuwasikia, ni shida,’’anasema.
Nassra Salum Mohamed ambae ni diwani wadi wa Kiuyu, anasema Mkuu wa mkoa wao, ni anakipaji cha uongozi, kuzungumza na hata kuamua jambo, na ni vyema wanawake wengine wakajifunza kwakwe.
‘’Hata sisi madiwani tukisikia tuna kikao na mkuu wa mkoa, inabidi kama unachangamoto unataka kuisilishwa kwa, uifanyia uchambuzi wa kina, vyenginevyo itakurudia mwenyewe,’’anasema.
Salim Ali wa Wete, anasema anazipongeza juhudi za kupata viogozi wanawake zilizochukuliwa na mashirika na asasi mbali mbali, zilizopigania nafasi ya uongozi kwa mwanamke.
‘’Nasikia kuna chama Chama Cha waandishi wa Habari wanawake Tanzania ‘TAMWA’ Zanzibar na wengine wamekuwa wakiwawezesha wanawake, nawaambia kwa mkoa wa kaskazini Pemba wamefanikiwa,’’anasema.
WANAHARAKATI
Mratibu wa TAMWA Pemba Fat-hya Mussa Said, anasema wanaijivunia mno, uongozi wa Mkuu huyo wa Mkoa hasa kwa vile alikuwa kwenye kapu la wanaharakati.
‘’Salama alikuwa anashikia bango kuwa, wanawake wanapopata nafasi za uongozi wasizibeze, na bahati nzuri imemuangukia yeye, sasa tunaona macheche yake kwenye uongozi,’’anasema.
Aisha Himid Vuia, anasema alichokifanya Dk. Mwinyi cha kuwapa nafasi nyingi wanawake, ni matokeo ya kelele za wanaharakati, ambapo hakuna mwanamke kiongozi aliyezubaa.
Khalfa Amour Mohamed, anasema wamekuwa wakishirikiana na Mkuu huyo wa mkoa katika shughuli kadhaa na hajawahi kukataa, maana anapenda kushirikiana na makundi ya kijamii.
HALI HALISI YA WANAWAKE NA UONGOZI
Zanzibar kwa sasa kasi ya wanawake kuingia katika uongozi imeongezeka ukilinganisha na miaka iliyopita ambapo TAMWA viongozi wanawake katika Baraza la wawakilishi ni asilimia 36 ambayo ni sawa na wanawake 28 kati ya wawakilishi 84 waliopata nafasi hiyo.
Ni wanawake 22 pekee ambao ni viongozi wakuu kati ya nchi na mataifa ya nchi 123 kwa idadi hiyo bado jitihada zinahitajika katika kuona mwanamke anapata fursa sawa katika vyombo vya maamuzi.
Mkuu huyo wa mkoa wa kaskazini Pemba, Salama Mbarok Khatib, aliteuliwa kushika nafasi hiyo Disemba 1, mwaka 2020 na kula kipambo Disemba 3, mwaka huo huo pamoja na wakuu wa mikoa wenzake.
MWISHO.
Comments
Post a Comment