NA
ZUHURA JUMA, PEMBA
WADAU
mbali mbali kisiwani Pemba wameitaka jamii kuacha kuwatupia majukumu mengi
wanawake ambayo yanasababisha kushindwa kuingia kwenye hatakati za kugombea nafasi
za uongozi.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti wadau hao walisema kuwa, si
vyema kumuachia manamke majukumu ya nyumbani pekee na badala yake wasaidiwe,
ili na wao wapate nafasi ya kuingia katika masuala ya uongozi.
Walisema
kuwa, mzigo
mzito wa nyumbani wanaoachiwa akina mama umekuwa sababu kubwa ya kuwakwaza na
kushindwa kushiriki katika shughuli za jamii, uchumi, siasa na maendeleo, hivyo kuna haja kwa akinababa
kushirikiana nao kuleketeza majukumu hayo Pamoja ili na wao wapate uhuru wa
kuingia kwenye uongozi.
“Hata
katika dini
yetu ya Kiislamu mwanamke hatakiwi kuachiwa pekee mzigo mzito wa
nyumbani, hivyo ni vyema tukawasaidia ili wapate
kufanya shughuli nyengine za kujiletea maendeleo yao, familia na taifa,” walisema
wadau hao.
Mdau
Saumu Ali Abeid, mkaazi wa Fuoni Unguja alisema, uzito wa kazi za nyumbani
unaomzunguka mwanamke ni pamoja na kupika, kushughulikia usafi wa nyumba,
malezi ya watoto, kumhudumia mume na wakati mwengine wazee wa mume na wa kwake
mwenyewe.
‘’Katika hali kama hii sio rahisi kwa mwanamke kujiingiza katika
harakati za kugombea uongozi
kwa sababu mwanamke anayezongwa na kazi nyingi za nyumbani hushindwa
kushiriki kwenye vikundi na kutoa mawazo yake ambayo yangempa ujasiri, maarifa na kujiamini
kuwa anaweza kuongoza wenzake au jamii,” alifahamisha.
Mwananchi ambae
hakutaka jina lake litajwe wa shehia ya Kipangani Wete alisema, mzigo wa kazi za
nyumbani aliokuwa nao mwanamke umepelekea kuwepo wanawake wachache katika
vyombo vya maamuzi.
“Hii
ndio moja ya sababu ya kushindwa kutatuliwa changamoto kadhaa zinazotukabili, kwani panakuwa
hakuna mtetezi wa hali ya wanawake katika vyombo vya maamuzi,” alieleza.
Kwa
upande wake Salama Mohamed wa Ole Pemba, alieleza kuwa mara nyingi mrundiko wa
kazi za nyumbani unawazuia wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi.
Mkurugenzi wa mradi wa kutoka PEGAO Pemba Hafidh Abdi Said alifafanua kuwa, kazi
nyingi za nyumbani zinasababisha wanawake wengi kutoshiriki katika uongozi na kusema kwamba iwapo kama
jamii itaendelea kuwaachia mzigo mzito akinamama basi hata maendeleo ya
nyumbani yatachelewa kupatikana.
‘’Tokea mwanamke anapoamka ni kazi mpaka jioni huwa hana hata
muda wa kupumzika au kufanya mambo mengine nje ya kuta ya nyumba yake’’,
aliongeza.
Katibu Kanda ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Pemba,
Habib Ali Khamis alieleza kuwa, wanawake wanakosa
msaidizi, hivyo hata anapokwenda kwenye vikao anachelewa na hatimae kukosa
ajenda zilizozungumzwa
na huishia kuwa msikilizaji tu.
Nae
mwalimu Saleh Nassor Juma ambae ni Katibu wa ACT Wazalendo Mkoa
wa Chake Chake kichama, alieleza
kuwa, elimu inahitajika zaidi ili akinamama wagombee na kazi za
nyumbani isiwe kikwazo kwao kuwa viongozi.
Wakati
wanaharakati wanaendelea kupigania haki za wanawake ikiwemo kushiriki katika uongozi,
bado baadhi ya wanawake wanakabiliwa na changamoto zinazosababisha kutokuingia
katika harakati za uongozi, hivyo ipo haja ya kutatuliwa kwa ajili ya
kumrahisishia shughuli zake.
MWISHO.
Comments
Post a Comment