NA HAJI
NASSOR, PEMBA@@@@
TAASISI
ya The Foundation for Civil Society ya Tanzania bara 'FCS' imesema inaendelea
kuridhishwa na utendaji kazi wa Mwemvuli wa asasi za kiraia Pemba ‘PACSO’,
katika utekelezaji wa mradi ‘uraia wetu’ hasa kwa kule kuwanganisha wadau
husika.
Hayo yameelezwa
na mwakilishi wa taasisi hiyo Neil Ngala, wakati akitoa salamu zake, kwenye
mkutano wa siku moja, wa kuibua changamoto za kisheria na sera, zinazokwaza
wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, uliofanyika Gombani Chake chake.
Alisema
PACSO, imekuwa ikiendelea vyema na utekelezaji wa mradi huo, jambo ambalo limeanza
kutoa taswira ya mafanikio yaliyotarajiwa, ikiwa ni pamoja na kuibua changamoto
za kisheria na sera.
Alieleza kuwa,
mradi huo ambo unatekelezwa na taasisi za PACSO, CYD na JUWAUZA kama hatua ya
kitaifa, PACSO imekuwa ikifanya vyema kwa kule kuwakutanisha wadau hisika.
‘’Sisi FCS,
tumekuwa tukijivunia mno kila tunapofanyakazi na ‘PACSO’ maana kile ambacho
wanakifanya, matunda yake yanaonekana mapema hata kabla ya mradi kumalizika,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine, Mwakilishi huyo alisema, lazima asasi za kiraia zifanyekazi kwa karibu
na jamii, ikiwa ni njia mwafaka ya kufikia yale walioyaazimia kuyafanya.
Kwa upande wake, Afisa kutoka Jumuiya ya wanawake wenye ulemavu Zanzibar ‘JUWAUZA’ kupitia mradi wa ‘uraia wetu’ Suleiman Baitan, alisema moja ya jambo la muhimu, katika utekelezaji wa miradi, ni kuwa na kundi husika, wakati wa utekelezaji.
‘’Ili asasi
ya kiraia ifikie ndoto zake, isisahau kuelekeza kundi husika ‘target group’
wakati wa utekelezaji wa mradi wowote, kama inavyoonesha kwenye andiko, hii ni njia
rahisi wakati wa kufanya tathmini,’’alieleza.
Katika hatua nyingine mwakilishi huyo wa JUWAUZA, alisema wamekuwa wakifanyakazi kwa karibu mno na ‘PACSO’ katika mradi huo, na hasa baada ya kuibuliwa changamoto za kisheria.
Akizungumza kwenye
mkutano huo, Mratibu wa miradi kutoka Mwemvuli wa asasi za kiraia Pemba ‘PACSO’
Mohamed Najim Omar, alisema mkutano huo ni muendelezo wa vikao mbali mbali,
wanavyovifanya na wadau wao.
‘’Kikao kama
hichi, kilishawahi kufanyika, na kuibuliwa changamoto za kisheria zinazowakwaza
wanawake kutogombea, watu wenye ulemavu kutopata haki zao mahakamani,’’alifafanua.
Akifungua kikao hicho, Mwenyekiti wa ‘PACSO’ Nassor Salim Majid, aliwataka washiriki wa mkutano huo, kuzungumza kwa uwazi, ili malengo ya kikao hicho yafikiwe.
Alieleza kuwa,
ndani ya jamii zipo changamoto za kisheria kadhaa ikiwemo masuala ya
udhalilishaji, matunzo ya watoto, migogoro ya ardhi ambapo yote hayo yanaikwaza
jamii.
Nae Mwakilishi
wa Jukwaa la Katiba Tanzania ‘JUKATA’ Thobias Messange, alisema mbinu za
kufanya ushawishi moja wapo ni kufanya utafiti, kujua kasoro za kisheria,
kanuni na kisera kabla ya kuanzisha jukwaa la ushawishi.
‘’Mwanaharakati
anaetaka kufanya ushawishi, sio vyema kukurupuka, lazima ajue kwa upana,
anachotaka kukifanyia utetezi, na wakati mwingine hata kuwatumia wanasiasa,’’alifafanua.
Akichangia mada
kwenye kikao hicho, Mkurugenzi wa Jumuiya ya wazalishaji karafuu Zanzibar ‘ZAPCO’
Abubakr Mohamed Ali, alisema woga wa watetezi na wanaharakati huchangia kutofikiwa
mwisho kwa wanachokitetea.
‘Suala la
kufanya uchechemuzi linahitaji ujasiri, kusoma kidogo, kujua sheria na kanuni
na kujiamini na wakati mwingine, hata kuweka kando tamaa, maana kama haya yakijitokeza
hakuna uendelevu wa jambo,’’ alieleza.
Mratibu wa Chama
cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA -Zanzibar ofisi ya Pemba
Fat-hya Mussa Said, alisema bado uwanaharakati unakabiliwa na changamoto kadhaa
ikiwemo, kutokujua mbinu halisi.
Nae Dina
Juma Makota kutoka ‘PEGAO’, alishauri kuwa wakati wa upangwaji wa mikakati na
mbinu za kufanya ushawishi na utetezi, makundi maalum, yasiwekwe pembeni.
Mkutano huo wa siku moja, kupitia mradi wa ‘uraia wangu’ umeandaliwa
na PACSO kwa ufadhili wa The Foundation for Civil Society kupitia Umoja wa nchi
za Ulaya.
Mwisho
Comments
Post a Comment