NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewaagiza viongozi
wa wilaya ya Micheweni, mkoa wa kaskazini Pemba pamoja na Mamlaka ya kukuza uwezekezaji
‘ZIPA’ kuhakikisha wanawashawishi wawekezaji na kampuni za ujenzi, kushirikiana
ili kujenga viwanja vya michezo katika eneo huru la Micheweni.
Alisema, pamoja na mipango na
mikakati ya serikali, lakini ni vyema kwa viongozi wa taasisi hizo, kuhakikisha
wanawakumbusha wawezekaji na wakandarasi, kuchangia ujenzi wa viwanja hivyo.
Dk. Mwinyi alitoa agizo hilo leo April 23, 20204,
wakati akijibu hoja za Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni Shamata Shaame Khamis, alipotoa
maombi ya ujenzi wa viwanja wa michezo, kwenye hafla ya ufunguzi wa barabara za
maeneo huru.
Alieleza kuwa, serikali inayomipango
na miakakati ya haraka ya kujenga viwanja vya michezo, ikiwemo vile ya kuchezea
watoto na vya mpira wa miguu, hivyo ni vyema na taasisi hizo, kuwashawishi wawekezaji
na kampuni za ujenzi kuchangia hilo.
Alifafanua kuwa, eneo hilo ambalo sasa
linamiundombinu ya kisasa ya barabara, ni vyema sasa navyo viwanja vya michezo
vikajengwa hatua kwa hatua, ili kuibua vipaji.
‘’Kila mwekezaji, mjenzi wa
miundombinu na kampuni nyingine, lazima zile fedha ambazo ni fungu la jamii, waangalie
uwezekano wa kusaidia ujenzi wa viwanja vya michezo eneo hili,’’aliagiza Dk. Mwinyi.
Aidha Rais huyo wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, alisema suala la ujenzi wa viwanja vya
michezo, sio jambo kubwa, kwani tayari wameshaanza katika baadhi ya maeneo na
atafurahi na eneo la Michewni likijengwa.
Mapema Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni
Shamata Shaame Khamis, alimuomba rais huyo, kumpa ujumbe aliyotumwa na wananchi
wa jimbo hilo.
‘Mhe. Rais, wananchi wamenituma mambo
kadhaa, likiwemo kutaka kujengewa viwanja vya michezo katika eneo hili na hasa
vya mpira wa miguu na cha kuchezea watoto,’’alisema.
Mwakilishi huyo alisema, tayari
baada ya ufunguzi wa barabara zinazoingia kwenye la huru la uwekezaji, limeshavutia
hivyo ni nafasi kwa serikali, nayo kujenga viwanja vya michezo.
‘’Wananchi wa jimbo la Micheweni,
wamevutiwa mno na kazi yako ya kuliimarisha eneo hili, na ombi lao hasa vijana
ni kutaka viwanja viwili vya michezo na kimoja kwa ajili ya watoto,’’alifafanua.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya
Micheweni Mgeni Khatib Yahya, alimueleza Rais huyo wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuwa sikuu iliyopita ilisherehekewa
katika eneo hilo.
‘’Kwa mara hii, wananchi walifurahia
sikuu katika eneo hili, ni wazi kuwa wameanza kunufaika na eneo hili huru la
uwekezaji hapa Micheweni,’’alieleza.
Wakati huo huo, kampuni ya IRIS, iliyojenga
barabara hizo za kuingilia maeneo huru Micheweni, imeahidi kujenga kiwanja kimoja
cha mpira wa miguu katike eneo hilo.
Mwisho
Comments
Post a Comment