NA
HAJI NASSOR, PEMBA:::-
SHIRIKA
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa āUNDPā limesema limeridhishwa mno, na mbinu
iliyobuniwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar 'ZLSC' kisiwani Pemba, kwa
kuwafuata wananchi vijijini kuwapa elimu, ushauri na msaada wa kisheria bila ya
malipo.
Kauli hiyo,
imetolewa na Mwakilishi wa shirika hilo kutoka Dar-es Salaam Apilike Gordon,
wakati akiwasilimia wananchi wa kijiji cha Tundaua, shehia ya Kilindi wilaya ya
Chake chake Pemba, kwenye mkutano wa wazi ulioandaliwa na āZLSCā kwa wananchi
hao.
Alisema mfumo
ulioandaliwa na āZLSCā unaonesha dhahiri jinsi Kituo hicho kinavyohakikisha,
hakuna mwananchi anaekosa haki yake, kwa kutokujua mfumo wa sheria.
Alieleza kuwa,
pamoja na kutoa elimu ya sheria, lakini kupitia watendaji wa Kituo hicho na
wanasheria wengine, wamekuwa wakiwapa ushauri na msaada wa sheria bila ya
malipo.
āāWananchi wa Tundaua,
nafasi mliopewa na āZLSCā itumieni kuuliza, kutaka ushauri wa msaada wa
kisheria bila ya malipo, na sisi āUNDPā tumevutiwa mno na mfumo huu,āāalieleza.
Aidha Gordon alisema,
wataendelea kufanyakazi na āZLSCā katika kuhakikisha jamii ya Zanzibar, inatapata
uwelewa wa masuala mbali mbali ya kisheria.
Akizungumza kwenye
mkutano huo, Kaimu Mratibu wa Kituo hicho Pemba Safia Saleh Sultan, alisema
pamoja na kuwepo kwa wasaidizi wa sheria majimbo yote ya uchaguzi ya Unguja na
Pemba, lakini wamemua kuwafuata wananchi.
Alieleza kuwa, ZLSC
haipendi kuona ndani ya Zanzibar, kuna mwananchi anaepoteza haki yake, kwa
kisingizio cha kuosa fedha cha kuwatafuta wakili, bali wao wapo kwa kazi ya
kuwasaidia, bila ya malipo.
Katika hatua
nyengine, ameiomba jamii kuendelea kushirikiana na vyombo vya sheria kama vile
mahakama, ili kutoa ushahidi pale wanapotakiwa kufanya hivyo.
āāInawezekana
wananchi walio wengi, wanapiga kelele kuwa wapo watuhumiwa kama wa makosa ya
udhalilisha wanaachiwa huru, lakini moja ya sababu ni kutopokelewa kwa
mashahidi,āāalieleza.
Mapema Afisa Sheria
kutoka Idara ya Katiba na Msasda wa Kisheria Pemba Bakari Omar Ali, alisema
kisheria, mtoto wa kike aliyechini ya miaka 18, hana ridhaa likitokezea kosa, hata
kama ametengeneza mazingira.
āāHata kama mtoto
huyo atamfuata mwanamme masafa ya zaidi ya kilomita 100,000 likitokezea kosa la
ubakaji, bado sheria itamkamata mwanamme kwenye kosa hilo,āāalifafanua.
Kwa upande wake
Wakili kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar āZLSCā kisiwani Pemba Siti
Habib Mohamed, wakati akijubu hoja za wananchi, alisema mwanamke anaweza
kuingia kwenye kosa la ubakaji, ikiwa atachangia kutokezea kwa kosa hilo.
āāSheria inaweza
kumtia hatiani mwanamke, ikiwa mazingira yataonesha amechangia ikiwa ni pamoja
na kutoa nyumba, kuruhusu mtoto wake kubakwa au hata mazingira mengine,āāalieleza.
Askari shehia ya
Kilindi Said Juma Khamis, aliwataka wananchi wanaofika kituo cha Polisi Madungu
na kutopata majibu yasioridhishwa na askari waliopo mapokezi, kufikisha
malalamiko yao kwa mkuu wa kituo.
āāHata baada ya
kuonana na mkuu wa kituo, kama hakukushughulikia, muone mkuu wa Polisi wilaya, nae
ukiona anakusumbua omba kuonana na Kamanda wa Polisi mkoa, ili kufikisha
malalamiko yako,āāalisema.
Akifungua mkutano
huo, sheha wa shehia ya Kilindi Nassor Mohamed Khamis, aliwataka wananchi hao,
kuhakikisha hawashiriki katika vikao vya sulhu hasa kesi za jinai.
Baadhi ya wananchi,
walikipongeza Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar āZLSCā kwa uamuzi wake, wa
kuwafuata kijijini kwao na kuwapa elimu, ushauri na msaada wa kisheria.
Juma Khamis Juma ākizitoā,
Mtumwa Abdalla Ali walisema kama sheria haijabadilishwa na mtoto wa kike,
aliyechangia kudhalilishwa kwake kutiwa hatiani, matendo hayo yataendelea.
Mwisho
Comments
Post a Comment