NA HAJI NASSOR, PEMBA:::-
MAHAKAMA ya Mkoa Wete, imelazimika
kumrejesha tena rumande hadi Juni 15 mwaka huu, daktari Is-haka Rashid Hadid, wa
kituo cha afya Gombani, anayedaiwa kumbaka mara tatu, mtoto wa miaka 16, baada
ya upande wa mashataka kutopokea mashahidi.
Awali daktari
huyo, alipelekwa rumade kauanzia Mei 18, mwaka huu na kutakiwa kurudi tena
mahakamani hapo Juni 1, ili kuwasikiliza mashahidi.
Ingawa
upande wa mashataka siku hiyo, haukupokea mashahidi, na mtuhumiwa huyo
kulazimika kurejeshwa tena rumande hadi Juni 15, mwaka huu.
Mara baada
ya mtuhumiwa kuwasili mahakamani hapo akitokea rumande, chini ya hakimu wa
mahakama maalum ya makosa ya udhalilishaji, Mwendesha mashataka Juma Mussa aliomba
shauri hilo kughgirishwa.
Alidai kuwa,
leo Juni 1, (jana), walitarajia kuwapokea mashahidi, ingawa hawakufika
mahakamani hapo na kuiomba mahakama hiyo, kulighairisha shauri hilo.
‘’Mheshimiwa
hakimu, tulirajia sana leo (jana), kuwapokea mashahidi, lakini hawakutokeza
mahakamani, hivyo naiomba mahakama yako tukufu, kulighairisha shauri
hili,’’alidai.
Baada ya
ombi hilo, hakimu wa mahakama hiyo Ali Abudur-haman Ali alikubaliana na ombi la
upande wa mashataka, juu ya kulipeleka mbele shauri hilo.
‘’Kutokana
na upande wa mashtaka kutopokea mashahidi wa shauri hili, mtuhumiwa itabidi
urudi tena rumande hadi Juni 15, mwaka huu, siku ambayo kesi yako
itaendelea,’’alisema.
Wakili wa
mtuhumiwa huyo, Abeid Mussa alipoulizwa na hakimu juu ya mpango huo, alidai
hana pingamizi na hilo, huku akisisitiz kuwasilishwa mashidi.
Ilidaiwa kuwa,
baina ya Aprili 21, mwaka huu mtuhumiwa huyo alimtorosha mtoto huyo, kutoka
nyumbani kwao Gombani wilaya ya Chake chake mkoa wa kusini Pemba, na kumpeleka nyumbani
kwake Kangagani wilaya ya Wete.
Ambapo baada
ya kumtorosha, usiku wake alianza kumbaka na kuendelea kumfanyia kitendo hicho
kwa siku tatu tofauti.
Kufanya
hivyo ni kosa, kinyume na kifungu cha 113 (1) (a) cha sheria ya Adhabu nambari
6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Kosa la pili
kwa mtuhumiwa huyo, baada ya kumtorosha mtoto huyo, siku hiyo hiyo majira ya
saa 3:00 usiku alimbaka, ambapo ni kinyume na kifungu cha 108 (1), (2), (e) na
109 (1) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018.
Kosa la tatu,
ambalo lilitokea Aprili 22 mwaka huu na la nne ambalo lilitokea Aprili 23,
mwaka huu pia, alilitenda kwa nyakati tofauti za usiku, ambapo alidaiwa kumbaka
mtoto huyo.
Kufanya
hivyo, ni kinyume na kifungu cha 108 (1), (2), (e) na 109 (1) cha sheria ya
Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment