NA JAFFAR ABDALLA, PEMBA
TIMU ya Chipukizi ya mjini Chake chake Pemba, imefanikiwa
kuwaondoa wahasimu wao wa jadi kwenuye soka, timu ya Tekeleza, katika michuano
ya kombe la FA CUP, baada ya kuwanagusha kwa mwagoli 2-1.
Kufanikiwa kwa Chipukizi kumetokana
na kuiotwanga timu hiyo magoli hayo, ni katika mchezo wa fainali ya kutafuta
bingwa wa Pemba.
Mchezo huo uliyopigwa katika dimba
la Gombani, ulihudhuriwa na washabiki wengi kiasi wa soka kutoka kila kona ya
kisiwa cha Pemba, kutokana ngebe za timu hizo.
Tekeleza ndio iliyotangulia kuliona
lango la Chipukizi, kwa bao safi lililofungwa kwenye dakika ya 34 kupitia
Khalfan Abdalla.
Licha ya Chupukizi kuongeza kasi
kwenye dakika 45 za awai, lakini timu hizo zilikwenda mapumziko ikiwa Tekeleza iko
mbele kwa bao hilo.
Ngwe ya lala salama, timu zote
zilirudi na nguvu mpya, huku kila upande ukifanya mabadiliko, na Chipukizi kusawazisha
bao hilo kupitia kwa Mundhir Iman, dakika ya 57.
Baada ya goli hilo washambuliaji wa Chipukuzi walihamia mfululizo langoni mwa wapinzani wao, hadi mchezaji Suleiman Nassor, alipoandika bao la pili dakika nne kabla ya mchezo kumalizika.
Ambapo kwa goli, timu ya Chupukizi
iliyowahi kucheza ligi kuu ya Zanzibar, wakatazwa mabingwa wa michauno hiyo
kisiwani Pemba kwa mwaka 2020/2021.
Kocha wa timu ya Chipukizi Mohamed
Ayub, alisema lengo la timu yake, ni kuchukuwa ubingwa wa michuano ya FA CUP
msimu huu.
’’Sisi lengo letu hasa ni kutwaa
ubingwa msimu huu, kwani tumepambana hadi tumefika kwenye hatua ya fainali, na
haikuwa kazi rahisi kufika hapa,’’alisema.
Kwa upande wa timu ya Tekeleza
walishindwa kutoa mashirikiano kwa waandishi, walipotaka kufanya mahojiano nao,
huku wakitoa lugha za matusi na kejeli kwa waandishi.
Mwisho.
Comments
Post a Comment