NA HAJI
NASSOR, PEMBA:::-
BAADA ya
Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar ‘ZAECA’ mkoa wa
kaskazini Pemba, Juni 3, mwaka huu kumshikilia Askari wa JKU kwa tuhma za kupokea
rushwa ya zaidi ya shilingi milioni 2.4, sasa ZAECA siku sita baadae, inamshikilia Askari
mwengine safari hii, ni wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo ‘KMKM’.
Askari huyo wa ‘KMKM’ anashikiliwa na ZAECA kuanzia Juni 9,
mwaka huu, akikabiliwa na tuhma tatu tofauti, ikiwemo ya ubadhirifu wa mali kwa
kuuza bati za miradi ya UVIKO 19.
Askari huyo mwenye namba K 2690 mwenye cheo cha ‘PO’ ametambulika
kwa jina la Khamis Ali Pembe miaka 45, mkaazi wa Donge Kitaruni Unguja.
Kaimu Kamanda huyo wa ZAECA alisema, kosa la kwanza
wanalomshikilia askari huyo wa KMKM, ni ubadhirifu wa mali na mapato, kinyume
na kifungu cha 42 (1) (a), kosa la pili ni kutumia vibaya mali, ambapo ni kinyume
na kifungu cha 43 (1) na kosa la tatu ni matumizi mabaya ya ofisi.
Aidha alieleza kuwa, kwa kosa la tatu ni kinyume na kifungu
cha 53 cha sheria nambari 1 ya mwaka 2012, sheria Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa
Uchumi sheria ya Zanzibar.
Mtuhumiwa huyo, ambae ni fundi Mkuu Msaidizi wa bati kutoka Unguja, akiwa na
jukumu la kutoa bati kwa ajili ya kupelekwa kwenye ujenzi wa miradi mbali mbali,
anadaiwa kutumia vibaya nafasi yake.
‘’Mtuhumiwa alishindwa uaminifu na kuamua kuziuza bati hizo kwa wananchi, na kukiuka matumizi yaliyokusudiwa kwenye miradi hiyo, na baada
ya kupata taarifa, tuliweka mtego na kunasa,’’alidai Kamaimu Kamanda huyo.
Alisema katika mtego huo, walifanikiwa kukamata bati 120 aina
ya ‘Danida’ na sasa kinachoendelea ni kukamilisha upelelezi, na utakapokamilika
hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Kaimu Kamanda huyo wa ZAECA alisema, kosa la kwanza
wanalomshikilia askari huyo wa KMKM, ni ubadhirifu wa mali na mapato, kinyume
na kifungu cha 42 (1) (a), kosa la pili ni kutumia vibaya mali, ambapo ni kinyume
na kifungu cha 43 (1) na kosa la tatu ni matumizi mabaya ya ofisi.
Aidha alieleza kuwa, kwa kosa la tatu ni kinyume na kifungu
cha 53 cha sheria nambari 1 ya mwaka 2012, sheria Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa
Uchumi sheria ya Zanzibar.
Mtuhumiwa huyo, ambae ni fundi Mkuu Msaidizi wa bati, akiwa na
jukumu la kutoa bati kwa ajili ya kupelekwa kwenye ujenzi wa miradi mbali mbali,
anadaiwa kutumia vibaya nafasi yake.
‘’Mtuhumiwa alishindwa uaminifu na kuamua bati hizo kuziuza
kwa wananchi, na kukiuka matumizi yaliyokusudiwa kwenye miradi hiyo, na baada
ya kupata taarifa, tuliweka mtego na kunasa,’’alidai Kamaimu Kamanda huyo.
Alisema katika mtego huo, walifanikiwa kukamata bati 120 aina
ya ‘Danida’ na sasa kinachoendelea ni kukamilisha upelelezi, na utakapokamilika
hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
MWISHO
Comments
Post a Comment