NA FATMA HAMAD, PEMBA
MAHAKAMA ya mkoa Chake Chake,
imeghairisha kesi ya kuingilia kinyume na maumbile, inayomkabili kijana
Khamis Abdalla Khamis ‘kirare’ mwenye miaka
[20], mkaazi wa Kangani
wilaya ya Mkoani, baada ya mtuhumiwa huyo kukataa kusomewa shitaka lake.
Mtuhumiwa
huyo wakati akiwa ametulia kizimbani hapo akisubiri kusomewe shitaka lake aliiambia
mahakama hiyo kuwa, hali yake sio mzuri, anaomba kesi ighairishwe na ipangiwe siku nyengine.
‘’Mheshimiwa
hakimu leo, (jana) ninaumwa na siwezi kukakaa, hivyo naiomba mahakama yako
ighairishe shauri langu, kwa leo na kulipangia siku nyingine,’’ alidai.
Hakimu wa
mahakama hiyo Muumin Ali Juma, alimueleza mtuhumiwa huyo kuwa, hiyo ni haki yako na inahitajika kupewa.
‘’Lakini tu nikueleze leo shahidi ambae ni
daktari amekuja wewe unasema unaumwa, ila
na siku akidharurika yeye usijekulalamika,
hivyo kwa leo tutamruhusu aendelee na majukumu yake na wewe utaridi
rumande’’,alisema hakimu huyo.
Aidha hakimu
huyo aliendelea kumtahadharisha mtuhumiwa huyo kuwa, kujichelewesha huko,
asifikirie kuwa, kuna hali ya kufutwa kwa kesi hiyo, bali ataendelea nayo hadi
mwisho.
Baada ya
maelekezo hayo, hakimu Muumin wa mahakama maalum ya makossa ya udhalilishaji,
aliliahirisha shauri hilo na kuamuru lirudi tena mahakamani hapo Julai 27,
mwaka huu.
Awali
ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Mei 28, mwaka
huu majira ya saa 2:00 usiku sokoni
Kangani wilaya ya Mkoani.
Ambapo
ilidaiwa kuwa, bila ya halali na bila ya ridhaa ya walezi wake, alimtorosha mtoto
wa miaka 10, kutoka nyumbani kwao na kumpeleka kwenye banda analoishi, na kisha
kumuingilia kinyume na maumbile.
Kufanya hivyo
ni kosa kinyume na kifungu cha 115 cha sheria nambari 6 ya mwaka 2018, sheria
ya Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment