NA
HAJI NASSOR, PEMBA
WATAALAMU
wa malezi ya kisayansi, makuzi na uchangamshi wa mtoto katika hatua za awali āECDā
kisiwani Pemba, wametaja njia tano ambazo familia ikizifuata, itakuwa ni chachu
ya ukuaji wa ubongo kwa matoto na kuongeza ufahamu.
Moja ya njia hizo ni chakula bora ikiwa ni pamoja na
mboga mboga, matunda na samaki kwa mama mjamzito, tokea siku ya kwanza baada ya
kubeba ujazito.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema kwa
mfano katika samaki, kuna kirutubisho kinachoitwa āomega threeā ambacho
chenyewe kimebaba chembe chembe zinazoitwa āridsā ambazo kazi yake kubwa, ni
kujenga ubongo wa mtoto.
Mmoja kati ya wataalamu hao Dk. Omar Adam Mohamed anayesomea
matibabu ya watoto nchini China, alisema hatua nyingine, ni mama mjamzito
kunywa maji kwa wingi.
Alisema chumvi chumvi na kalshiam zilizomo ndani ya maji
safi na salama, humsadiai mtoto kukukua kwa haraka na kujenga ubongo wake tokea
akiwa tumboni.
Mtaalamu huyo alisema, mama mjamzito anapopuuzia unywaji
maji kwa wingi, hujikaribishia magonjwa ambayo yanaweza kusababish kusinyaa kwa
ukuaji wa mtoto na kuathiri ubongo wake.
āāSuala la lishe nzuri wala halinauhusiano na utajiri,
bali familia ni kujipanga kwa mboga za majani na matunda ya kawaida, kufanya
hivyo ni kukuza ubongo wa mtoto,āāanaeleza.
Nae Kaimu Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii Pemba Omar Mohamed Ali, alisema njia
nyengine ya kukuza ubongo wa mtoto, ni wazazi kujenga utamaduni wa
kumzungumzisha mtoto akiwa tumboni.
āāInawezekana jamii haiamini kuwa, mtoto akiwa tumboni
anaskikia sauti, milio, kelele n ahata kupata msongo, hivyo ni wajibu kufanya
hivyo ili aanze kuzoea mazingira yake mapema,āāalishauri.
Aidha Afisa huyo alisema, mara mtoto anapozaliwa katika
miezi yake mitatu ya kwanza, familia ziwe na utamaduni wa kumtolea hadithi na
kufanya uchangamshi nae.
āāHatua nyingine ni watoto kabla hawajafikia miaka minane
ā8ā jamii iwashirikishe kwa mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja kumfundisha majina ya
vitu, hasa yalio karibu nao,āāalishauri.
Aidha alifafanua kuwa, sio busara jamii kuanza kuwandaa
watoto baada ya kufikia miaka minane, na kuiacha siku moja baada ya kuzaliwa
hadi miaka minane.
āāMtoto anaanza kupata ufahamu toka akiwa tumboni mwa mama yake, na hata siku
moja baada ya kuzaliwa, sasa ni wajibu kwa wazazi, kutenga muda kila siku ili
kushirikiana na mtoto wao, hiyo itajenga ubongo wake mapema,āāalieleza.
Muwezeshaji kwenye
mafunzo ya Kitaifa ya Sayansi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto
āSECDā Everlyne Okeyo, anasema tafiti zinaonesha kuwa, mtoto akiwa tumboni
anasikia zaidi ya lugha 600.
Alisema,
watoto wanakosa ukuaji mzuri wa kutengeneza ubongo wao, kwa kule wazazi
kutowashughulika kuzungumza nao, wakidhani hawana uwezo wa kufahama lugha zao.
Alieleza
kuwa, makuzi mazuri ya awali ya mtoto, ni baina ya siku moja baada ya kuzaliwa,
hadi miaka minane, ambapo hapo huwa rahisi kwa wazazi na walezi, kuweka
mwelekeo wa maisha ya mtoto.
Katika
hatua nyingine, Everlyne alisema, ubongo wa binadamu una nyuroni bilioni 100,
na ndio maana mtoto mara anapozaliwa, huwa na asilimi 25 ya ubongo wake ni mtu
mzima.
āāMtoto
anapofikia mwaka mmoja, hufikia asilimia 60, wakati miaka miwili huwa na
asilimia 75 na kuanzia miaka minne hadi sita, hubeba asilimia 90 ya
uwelewa,āāalieleza.
Akizungumza kwenye
ufunguzi wa mafunzo hayo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na
Makundi Maalum Dk. Dorothy Gwajima, aliwataka waandishi wa habari, kuifikisha
kwa jamii, dhana ya malezi ya kisayansi āSECD.
Mzazi Mwajuma Haji
Makame wa Chake chake, ambae ameshapata watoto sita, anasema amekuwa
akiwasemesha watoto wake wachanga, ingawa sio kwa kurudia rudia.
āāNilikuwa nadhani
hadi mtoto aanze kufikia mwaka mmoja na kuendelea, ndio nianze kumfundisha na
kuchangamana naye, nikiamini ndio anafahamu,āāanasema.
Wazazi Khamis Hija
Kassim na Othman Himid Omar wanasema, wanaume waliowengi wamekuwa wakikamilisha
majukumu ya familia na yaliobakia likiwemo la uchangamshi wa mtoto ni la mama
pekee.
āāElimu ya ECD bado
haijafika kwa wananchi tuliowengi, maana wapo baadhi yetu tunadhani wajibu ni
kuakikisha milo imepatikana na sio kutenga muda kucheza na watoto na hasa mama
wajawazito,āāanasema.
Hivi karibuni
akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, Mkuu wa
mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, aliwataka wanaume kutenge muda wa
kucheza na watoto wao.
Mwisho
Comments
Post a Comment