NA HAJI NASSOR, PEMBA
KELELE zinazopigwa na Serikali na
jumuiya mbali mbali za kukemea vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa wanawake na watoto,
bado wapo wanaotia pamba za masikio.
Cha ajabu na chakusikitisha, wapo hata wazazi na walezi,
waalimu na sasa hata kumeibuka wale watoa huduma wa afya, kutajwa katika hilo.
Mwaka 2019,
kama ilikuwa kisirani kwa watoto na wanawake, kufanyiwa ukatili na
udhalilishaji na madaktari kisiwani Pemba.
Mfano Novemba
21, mwaka 2019, katika hospitali ya Chake chake, daktari wa kitengo cha
Atrasaund, alishikiliwa na ZAECA kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono kwa
mjamzito, kama sharti la kumpa huduma.
Kisha
kesi hiyo baada ya uchunguzi na kuhojiwa, alifikishwa mahakamani, ingawa Januari
1, mwaka jana aliachiwa huru, kwa sababu mbali mbali zikiwemo ushahidi
kutoumuunganisha na kesi
Aidha
Disemba 18, mwaka 2019, TBC 1 iliripoti Afisa Muuguzi msaidizi wa kituo cha
Afya Mamba mkoani Katavi kushikiliwa na Jeshi la Polisi, kwa tuhuma za kumbaka
mjamzito, wakati alipokuwa akimsaidia kujifungua.
April 21,
tena mwaka huu wa 2022, daktari mwengine anaefanyakazi kituo cha afya Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba,
Is-haka Rashid Hadid, alishikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa
kaskazini Pemba.
Nae, kama walivyokuwa kwa madkatari
wengine, wasiotekeleza wajibu wao vyema, akituhumiwa kumtorosha na kisha
kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16.
Daktari huyo miaka 35, ni mkaazi wa
Kangagani, Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo
kutoka kwa rafiki yake.
Kisha alimpeleka kwenye nyumba
anayoishi eneo la Kangagani, akidai kuwa kuna dawa alizozikosa hospitali,
anaweza kumpatia huko.
Mtoto anasema kuwa, April 21 mwaka
huu, alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya
kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu.
Ilipofika usiku, walikuwa
wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms), kwa lengo la kwenda kuchukua dawa
nyingine ambazo kwa mchana huo, alizikosa hospitalini hapo.
"Nilikwenda hospitali
kutibiwa, ugonjwa mapele sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje
daktari mwengine, kwa hiyo kesho (siku ya pili yake), atakuja kunichukua, ili
ukanipe dawa nyingine", anasimulia mtoto.
Siku ya pili wakati yupo skuli,
daktari huyo alimpigia simu na kumeleza kuwa, akirudi skuli, amsubiri kwa
rafiki yake, mpaka atakapotoka kazini daktari huyo, ili akamchukue kwa ajili ya
kumpatia dawa nyingine.
‘’Alikuja kunichukua, nikijua anaenda
kunipa dawa nyingine, kumbe alinipeleka hadi nyumbani kwake na kisha baada ya
kunipima Ukimwi alinibaka,’’anasimulia.
‘’Usiwe na wasi wasi wowote wewe
uko salama na mimi niko salama, hatuna maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, na
kisha aliniletea futari na,’’anafafanua.
Mtoto huyo alieleza kuwa, daktari
huyo (mtuhumiwa) anapokwenda kazini, alikuwa anamfungia mlango, ingawa baa ya
siku ya tano alimtoa na kuandoka eneo hilo.
Mama mzazi anaeleza kuwa, mwanawe
aliondoka kwenda skuli, ingawa alikuja kupata wasiwasi kuona ilipofika saa 9:00
jioni, kuwa hajarudi na kuanza kupiga simu kwa ndugu na jamaa wa karibu.
Aliporudi mumewe (baba mzazi wa
mtoto) akamueleza kuwa mtoto wao, hajarudi na ndipo walipochukua uamuzi wa
kwenda kituo cha Polisi Chake Chake kutoa taarifa.
"Ilipofika siku ya tano
nilimpigia simu nikampata, nikamtaka arudi, na alitii agizo hilo na alipofika
nilimpeleka kituo cha Polisi Chake chake, ambapo awali walipeleka
malalamiko,’’anasimulia.
Hakimu wa mahakama hiyo Ali Abdull-rahaman Ali, anasema hakuona kuwa kuna kesi ya kumshilikia daktari huyo, baada ya mtoto (muathirika) kumkana mahakamani mshitakiwa.
ATHARI YA MATENDO
Vitendo
hivyo dhidi ya watoto ni suala zito linalowanyima haki zao za kibinadamu ambalo
humkosesha haki zake za msingi ikiwemo kuishi, kupata elimu na afya bora.
Watoto
wanapofanyiwa vitendo vya udhalilishaji ikiwemo ukatili na unyanyasaji
hushindwa kufurahia utoto wao kwani kuwaletea madhara makubwa kiakili, kihisia
na kimwili.
Hali hii
isipokomeshwa ni wazi kuwavitendo hivyo vitaendelea kuongezeka na hata kusababisha
umasikini katika jamii zetu.
Bila shaka
kila mmoja amepitia hatuwa ya utotoni kama tafsiri ya mtoto inavoolekeza kuwa
mtoto ni mtu yoyote mwenye umri chini ya miaka 18.
Tafsiri
ambayo imetokana na mkataba wa kimataifa wa haki za watoto,mkataba wa
afrika kuhusu haki na ustawi wa mtoto
pamoja na sharia ya Mtoto nambari 6 ya mwaka 2011 ya Zanzibar.
UTOAJI USHAHIDI
Suala la
kutowa ushahidi limekuwa kikwazo kikubwa kwa jamii zetu na ndio maana
wanaoshughulikia kesi hizo hupata mwanya wa kujificha na mwisho wa siku kufutwa
kwa kesi hizo kwa ubwete kabisa.
Tumekuwa
tukisikia ama kushuhudia mara kwa mara juu ya maamuzi mbalimbali ya kimahkama
kutupwa kwa sababu ya kukosekana kwa ushahidi ama ushahidi kutotosheleza jambo
ambalo linarejesha nyuma juhudi za mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji.
Wakati
mwengine hata mahakama za juu wakisikiliza rufaa za mahakama za chini zimekuwa
zikiyabadilisha maamuzi ya mahakama za chini kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya
kutokuzingatia taratibu za kisheria za upokewaji ushahidi.
Mkurugenzi
wa Jumuiya ya wasaidizi wa sharia wilaya ya Mkoani Nassor Hakim, anasema ni jukumu
la jamii kufanya kila mbinu kuhakikisha wanafika mahakamani kutowa ushahidi.
‘’Waliowengine
wanadhani hakimu na mwendesha mashataka, ndio wanaweza kumaliza kesi zote na
msitakiwa kufungwa, wakati sio sahihi,’’anasema.
Mwanaharakati
Omar Haji Omar Anasema si vyema kutovunjika moyo kwa kikwazo chochote kwani
kufanya hivyo ndio kutoa mwanya wa kuzizimishwa kesi hizo.
Mratibu wa
wanawake na watoto Shehia ya Mchanga mdogo Siti Khatib Ali anasema lazima jamii
iungane katika kutoa ushahidi.
Anasema
wanaotenda matendo ya udhalilishaji wamekuwa wakifuatilia watu iwapo kama
wanafika mahakamani kutoa ushahidi ,na
kama wanachoka na wao hupata nguvu ya kuyaendeleza matendo hayo.
Sheha wa
shehia ya Kiungoni Wilaya ya Wete Omar Khamis Othman, anasema ushahidi mahakamani
ndio kigezo cha mtuhumiwa kutiwa hatiani.
Anasema
katika shehia yake wanajipanga kuhakikisha wanasaidiana nauli ili kufika
mahakamani kutowa ushahidi.
Afisa ustawi
wa jamii wilaya ya Wete Haroub Suleiman Hemed anasema ni wajibu wa jamii katika
kupambana na kutokomeza udhalilishaji wa
kijinsia jambo ambalo kabla walidhani ni la kazi ya taasisi fulani tu.
Arafa Abdi
wa Mkoani anasema ni vyema kukapitiwa vyema sheria ya ushahidi, kwani haimtendei
haki mtoto aliyefanyiwa udhalilishaji kwa vile hutowa ushahidi kwa alilofanyiwa
na mwisho wa siku kesi hufutwa.
“Tena maneno ya mara ya mwanzo ya mtoto
aliyedhalilishwa ni bora yakarekodiwa kwani hakutokuwa na udanganyifu,”anasema.
WAATHIRIKA WA VITENDO VYA
UDHALILISHAJI
Baadhi ya
watoto kuanzia miaka 15 hadi 17 ambao ni waathirika wa udhalilishaji, wanasema,
elimu ya kujengewa ujasiri wa kutoa ushahidi mahakamani, imewasaidia.
Bado kundi la watoto linakumbana na kadhia
inayofanywa na baadhi ya watendaji wa vyombo vya sheria kwa kuchukuwa rushwa ya
pesa na vitu vya thamani kwa lengo la kupotosha ushahidi.
“Sisi kama
waathirika wa vitendo vya udhalilishaji hasa wenye hali ngumu ya kimaisha, hiyo
tabia imekuwa ni changamoto kubwa yenye kutupa wakati mgumu,’’anasema mmoja.
Watoto hao
walivitaka vyombo vya sheria kufanya kazi kwa uadilifu ili haki itendeke kwa
pande zote mbili ,na kuondosha tatizo
hilo katika visiwa vya unguja na Pemba.
Hata hivyo
walliiomba seikali kuwa kesi za udhalilishaji zisiwe na mawakili kwani ndio
kichaka kikubwa wanachotumia upande wa mtuhumiwa kwa wale wenye pesa zao na uwezo
fulani wa kifedha ama madaraka
fulani .
VYOMBO VYA SHERIA
Mwanasheria
dhamana ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka Pemba Ali Haidar, anasema hakuna mashitaka
ambayo mtu anatiwa hatiani, bila ya kuwepo mashahidi.
“Sisi
waendesha mashtaka ,hatufahamu lolote iwapo kuna kosa limefanyika vijijini ,sasa
kama wakija watu kutoa ushahiodi au kupinga juu ya tendo fulani ,sasa hapo ndio
ukweli hupatikana,”alieleza.
Hakimu wa
mahakama ya Mkoa Chakechake Luciano Makoye Nyengo anasema mashahidi wote wanaofika mahakamani
wamekuwa wakipewa nauli zao kama kawaida .
Anasema
kukosekana kwa nauli hiyo kusiwarejeshe nyumbani mashahidi, maana suala la kutowa
ushahidi ni haki yao, hasa katika kuusaidia
muhimili wa mahakama , kufanikisha kazi zake.
“Jamii
ijipange vyema kuhakikisha wanakuwa na hamu kufika mahakamani kutowa ushahidi
,kwani hakuna kesi ambayo itafikia tamati ,pasi na kuwepo kwa mashahidi,
”alisema.
Mwisho
Comments
Post a Comment